Bunge Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bunge la Tanzania

Habari

SPIKA ZUNGU ATOA TAHADHARI UTEGEMEZI WA TEKNOLOJIA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ametoa tahadhari kuhusu utegemezi wa teknolojia kwa mataifa ya nje.

Amesema hayo Jijini New Delhi nchini India wakati akichangia mada kuhusu Akili Mnemba (AI) Bungeni; Uwiano kati ya Ubunifu na Usimamizi wake, katika Mkutano wa 28 wa Maspika na Wenyeviti wa Bunge wa Jumuiya ya Madola (Conference of Speakers and Presiding Officers of the Commonwealth).

Akielezea kuhusu uhuru wa kidijitali (digital sovereignity) Mhe. Zungu ametoa tahadhari kuwa utegemezi mkubwa kwa mataifa ya nje na kampuni kubwa za teknolojia unahatarisha uhuru wa nchi kiusalama na kiuchumi.

“Taarifa za wananchi zinapohifadhiwa na kumilikiwa na makampuni ya kigeni, nchi inapoteza uwezo wa kulinda faragha na usalama wa taifa lake” alisema Mhe. Zungu.

Hivyo, Mhe Zungu alisisitiza umuhimu wa nchi kuwa na udhibiti kamili juu ya mifumo yake ya teknolojia badala ya kuwa mpokeaji tu wa teknolojia kutoka nje.

Aidha, alihimiza kuwepo kwa mifumo ya kusaidiana ndani ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth) ili kusaidia nchi wanacham