Habari
Kamati za Kudumu za Bunge zaanza kukutana Jijini Dodoma
Kamati za Kudumu za Bunge zimekutana na kufanya uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati hizo siku ya Jummane tarehe 13 Januari, 2026 katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.
Vikao vya Kamati hizo ni kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Bunge la Kumi na Tatu unaotarajiwa kuanza siku ya Jumanne, tarehe 27 Januari, 2026.
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa wakati wa vikao vya Kamati hizo ni pamoja na kuzifahamu Wizara na Taasisi zake na baadhi ya Sera na Sheria kulingana na majukumu ya kila Kamati kama ilivyofafanuliwa kwenye Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge chini ya Kanuni ya 140 ya Kanuni za Bunge, Kamati kupitishwa kwenye majukumu yake ya msingi na Kamati ya Bajeti kufanya maandalizi ya Hoja zitakazojadiliwa na Bunge.
