Habari
Tanzia
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama, kilichotokea leo tarehe 11 Desemba, 2025 Jijini Dodoma .
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba, 2025 Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Peramiho, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.
