Habari
Mkutano wa Tano (5) wa Bunge waanza Jijini Dodoma
Mkutano wa Tano (5) wa Bunge la Kumi na Tatu (13) umeanza Siku ya Jumanne tarehe 27 Oktoba, 2026 Jijini Dodoma.
Shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huu ni pamoja na:-
Maswali
Kama ilivyo ada katika kila Mkutano wa Bunge kunakuwa na kipindi cha Maswali Bungeni kila siku ambapo jumla ya maswali 160 yataulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Mawaziri. Aidha, kutakuwa na kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu siku ya Alhamisi ambapo takriban maswali kumi na sita (16) yataulizwa na Waheshimiwa Wabunge.
Maazimio ya Bunge
Katika wa Tano (5) wa Bunge, jumla ya maazimio matatu (3) yatawasilishwa na kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kupitishwa.Maazimio hayo ni yafuatayo:-
Azimio la Bunge la Kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kuridhia na Kuwezesha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika Jijini Arusha kuanzia Tarehe 5 – 9 Oktoba 2026
Azimio la Bunge la Kuridhia Marekebisho ya Mkataba wa Kimataifa wa Sukari wa Mwaka 1992 (International Sugar Agreement of 1992).
Kamati ya Mipango
Katika Mkutano huu, Bunge litakaa kama Kamati ya Mipango kwa ajili ya kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2027/2028.
Taarifa za Kamati
Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zitawasilisha taarifa za Kamati hizo kuhusu Hesabu zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. Aidha, Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma itawasilisha taarifa ya Kamati hiyo kuhusu Uwekazaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Mkutano huu unatrajiwa kuahirishwa Siku ya Ijumaa tarehe 6 Novemba, 2026.
Ratiba ya shughuli zote zitakazofanyika katika Mkutano wa Tano (5) wa Bunge inapatikana katika tovuti ya Bunge ambayo ni www.bunge.go.tz
