Parliament of Tanzania

Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge waanza Jijini Dodoma

Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge la Kumi na Moja umeanza siku ya Jumanne tarehe 28 Januari 2020 na unatarajiwa kumalizika tarehe 7 Febuari 2020 Jijini Dodoma. Mkutano huu ni Mahsusi kwa ajili ya Bunge kupokea na kujadili Taarifa za Mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge. Shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:-

1.0 KUWAKABIDHI MAJOHO MASPIKA WASTAAFU

Katika Mkutano huu wa Kumi na Nane wa Bunge kutakuwa na shughuli ya kukabidhi Majoho kwa Maspika Wastaafu Mheshimiwa Pius Chipanda Msekwa, Mheshimiwa Samuel John Sitta (Marehemu) ambapo Joho alilotumia litapokelewa na Mke wake Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta kwa niaba ya familia, na Mheshimiwa Anne Semamba Makinda. Shughuli hii itafanyika katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge tarehe 28 Januari, 2020 mara baada ya Kipindi cha Maswali.

2.0 MASWALI

Katika Mkutano huu wa Kumi na Nane, wastani wa maswali 125 ya Kawaida yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge. Aidha, wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku za Alhamisi tarehe 30 Januari, na 6 Febuari, 2020.

3.0 MISWADA YA SERIKALI

Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.8) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.8) Bill, 2019] na Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (The Arbitration Bill, 2020).

4.0 TAARIFA ZA KAMATI

Katika Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge, Kamati za Kudumu za Bunge 15 zitawasilisha Taarifa za Mwaka za kazi za Kamati hizo kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 117(15) ya Kanuni za Bunge:-

i. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali;

ii. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa;

iii. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma;

iv. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti;

v. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira;

vi. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu;

vii. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini;

viii. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii;

ix. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji;

x. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii;

xi. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI;

xii. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo;

xiii. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria;

xiv. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa; na

xv. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Ratiba yote ya Mkutano wa Bunge inapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Suleiman Masoud Nchambi

Kishapu (CCM)

Supplementary Questions / Answers (9 / 0)

Contributions (4)

Profile

Hon. Khamis Ali Vuai

Mkwajuni (CCM)

Profile

Hon. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi

Nominated (CCM)

Questions / Answers(0 / 22)

Supplementary Questions / Answers (0 / 42)

Contributions (12)

Profile

View All MP's