Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Zungu pamoja na viongozi wengine wameshiriki katika Bunge-Azania Bonanza 2026 linalofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlini iliyopo Jijini Dodoma Januari 31, 2026. Bonanza hilo lilianza kwa matembezi kutoka eneo la Chuo cha Mipango kuelekea viwanjani hapo. Bonanza hilo limehusisha Waheshimiwa Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge, Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi ambao ni Mashabiki wa Timu za Simba na Yanga.