Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), ameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyofanyika tarehe 2 Februari, 2026 katika viwanja vya Mahakama Kuu Jijini Dodoma. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mhe. Spika alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maboresho makubwa aliyoyafanya kwenye Mahakama zote Nchini. Aidha, kupitia siku hiyo, Mhe. Spika ameendelea kutambua umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau katika utungaji wa Sheria jambo ambalo Bunge limekuwa likifanya.