Wagombea nafasi ya Spika wa Bunge wakijinadi mbele ya Wabunge wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Kumi na Tatu. Wagombea hao walikuwa ni pamoja na Mussa Zungu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Veronica Tyeah (NRA), Aniytha Mgaya (NLD), Chrisant Nyakitita (DP), Ndonge Said Ndonge (AAFP) na Amin Yango wa ADC.