Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza Bungeni mara baada ya kuthibitishwa na Waheshimiwa Wabunge kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 13, 2025. Uthibitisho huo umefanyika baada ya Mhe. Rais kumteua Mbunge huyo wa Iramba Magharibi na baadae uteuzi wake kuwasilishwa Bungeni wakati wa Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 uliofanyika tarehe 13 Novemba, 2025.