Bunge Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bunge la Tanzania

Habari

Vikao vya Kamati za Bunge vyaahirishwa kufuatia msiba wa Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi


Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb) anawatangazia Waheshimiwa Wabunge kwamba vikao za Kamati za Kudumu za Bunge vimeahirishwa kwa siku ya leo tarehe 25 Machi, 2026 kwa ajili ya maombolezo.

Vikao hivyo vimeahirishwa kutokana na taarifa za kifo cha Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi (Mb),aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani.

Shughuli hizo za Kamati zinaahirishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 176 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Agosti, 2025.

Mheshimiwa Lukuvi amefariki asubuhi tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamini Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.