Bunge Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bunge la Tanzania

Habari

SPIKA ZUNGU ASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), ameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyofanyika tarehe 2 Februari, 2026 katika viwanja vya Mahakama Kuu Jijini Dodoma. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Zungu alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa maboresho makubwa aliyoyafanya kwenye Mahakama zote Nchini.

Aidha, kupitia siku hiyo, Mhe. Zungu ameendelea kutambua umuhimu wa ushirikishwaji wa wadau katika utungaji wa Sheria jambo ambalo Bunge limekuwa likifanya.