Bunge Logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Bunge la Tanzania

Habari

NAIBU SPIKA SILLO AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU SPIKA WA KWANZA WA BUNGE LA ZAMBIA


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Sillo (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Spika wa Kwanza wa Bunge la Zambia, Mhe. Malungo Chisangano (Mb), alieambatana na ujumbe wake walipomtembelea leo tarehe 2 Februari, 2026 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Pamoja na mambo mengine wamezungumza kuhusu kubadilishana uzoefu na kudumisha mahusiano yaliyopo baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Zambia.