Parliament of Tanzania

Waziri Mkuu afuturisha Waheshimiwa Wabunge Jijini Dodoma

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameandaa futari kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Ofisi ya Bunge katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma siku ya jumatano tarehe 15 Mei, 2019.

Akizungumza wakati wa futari hiyo Mhe. Waziri Mkuu aliwashukuru wote waliojitokeza na kuwaasa kuendelea kudumisha amani, upendo na mshikamano hasa katika kipindi hichi cha mfungo.

Kwa upande wake Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alimshukuru Waziri Mkuu kwa kuandaa futari ambayo imewajumuisha pamoja Wabunge na wote waliohudhuria.

“Nawatakia kila la kheri wote ambao mmefunga muendelee kuwa salama hadi mfungo utakapoisha, kubwa zaidi tudumishe amani katika Bunge letu na nchi yetu kwa ujumla” alisema Mhe. Spika

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's