Parliament of Tanzania

SPIKA akutana na Rais Mstaafu wa Ireland

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amesema Bunge litaendelea kuungana mkono jitihada za Serikali za kuboresha afya ya jamii ikiwemo uzazi salama, afya ya mama na mtoto na afya ya wazee.

Spika alitoa kauli hiyo Ofisini kwake Mjini Dodoma jana baada ya kutembelewa na Rais Mstaafu wa Ireland Mheshimiwa Mary Robnson na Mama Graca Machel pamoja na ujumbe wao.

Alisema siku zote Bunge limekuwa likipigania masuala mbalimbali yahusuyo afya ya jamii na kwamba ipo kamati maalamu ya Bunge ya Huduma ya Jamii ambayo inashughulikia masuala mbalimbali ikiwemo Huduma za Afya.

“Vilevile tunayo Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi ambayo inashughulikia masuala mbalimbali ikiwemo suala zima la uzazi salama,” alisema.

Alisema pia wapo wabunge mmoja mmoja ambao huyasemea masuala ya afya ya jamii na kwamba wamekuwa wakiuliza maswali mbalimbali kwa mawaziri na kujibiwa.

Kwa upande wake, Mama Machel alisema wanatambua mchango wa Tanzania katika kuboresha huduma za afya na kuishauri iendelee kufanya vizuri zaidi.

“Nashauri kipaumbele kile mlichokiweke katika elimu kwa kutoa elimu bure hadi kidato cha nne mfanye hivyo pia katika sekta ya afya,” alisema.

Alisisitiza pia wabunge kuhakikisha wanatenga bajeti ya kutosha katika sekta ya afya pamoja nakupitisha sheria zitakazosaidia kuobresha sekta hiyo.

Naye Mheshimiwa Robson alisema anatambua nguvu ya Bunge katika kuhakikisha afya ya jamii inaboreshwa na kusifu juhudi za Tanzania za kuboresha elimu na sekta ya afya pia.

Mheshimiwa Robson na Mama Machel ni wajumbe wa Taasisi ya ‘The Elderes’ ya Uingereza inayoshughulikia masuala ya amani, haki za binadamu na huduma za afya.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

Hon. Kunti Yusuph Majala

Special Seats (CHADEMA)

Supplementary Questions / Answers (4 / 0)

Contributions (7)

Profile

Hon. Mboni Mohamed Mhita

Handeni Vijijini (CCM)

Supplementary Questions / Answers (6 / 0)

Contributions (2)

Profile

Hon. Khalifa Salum Suleiman

Tunguu (CCM)

Profile

View All MP's