Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Amb. Dr. Pindi Hazara Chana (26 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote, naomba niungane na Watanzania wenzangu kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa, Dkt. John Pombe Magufuli. Mheshimiwa Rais amefanya kazi nyingi kubwa na wataalam wa Kiswahili wanasema mwenye macho haambiwi tizama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi hizi zinatoka ndani ya nchi na nje ya nchi. Ukiwa nje ya nchi unaposema tu unatoka Tanzania kwanza lazima upokee salama na pongezi za Mheshimiwa Rais. Utaambiwa tunampenda sana Mzee Magufuli, anafanya kazi na amekuwa ni mfano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika na duniani kote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niwashukuru wananchi wa Njombe kwa ridhaa yao ya kunirudisha tena mjengoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kwa moja niende kwenye suala nzima la kilimo. Mikoa ya Kusini kwa asilimia kubwa sana wamejikita kwenye masuala ya kilimo na Mkoa wa Njombe kuna kilimo cha mazao mengi kama viazi, mbao zinakwenda mpaka nje nchi ndani ya Jumuiya ya Africa Mashariki ambapo kuna masoko mengi sana lakini pia kuna suala nzima la mahindi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze sana Serikali ya Awamu ya Tano eneo la mahindi na pembejeo wamefanya kazi nzuri lakini tuendelee kuangalia bei za mbolea ni namna gani tutaweza kufanya ili mbolea iendelee kuzalishwa nchini ili bei ipungue. Sasa hivi mfuko mmoja kwa mbolea ya kukuzia ni Sh.50,000 hadi tumalize kilimo, mkulima anakuwa amewekezq sana. Kwa hiyo, eneo la pembejeo za kilimo hususani zao la mahindi, naomba tuendelee kuliboresha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, nipongeze kwa masoko ambayo yako na masoko mengi sasa hivi ni soko huria lakini kwa kweli tunahitaji kuona intervention, ni namna gani tunahakikisha wananchi wakishalima zao hili la mahindi wanapataje masoko ya uhakika. Nilete salama kutoka Mkoa wa Njombe, nadhani Waziri wa Kilimo ananisikia, yupo hapa jirani yangu wanaomba mahindi yakanunuliwe. Kuna mahindi mengi sana, ili yasiweze kupotea kutokana na upotevu unaotokea mara baada ya kilimo na kwenye hotuba imesekana wakati mwingine 40% ya mahindi wakati mwingine yanapotea (postharvest) basi tuone namna ya kuyanunua mahindi haya. Kuna mahindi mengi wanaomba SGR, NFRA ikiwezekana wakayanunue na wawaunganishe wakulima wa Mikoa hii ya Kusini na maeneo mbalimbali kama World Food Program, FAO, tuna kambi nyingi za wakimbizi wanahitaji chakula cha kutosha tuone namna gani ya kuunganisha eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine naanza na pongezi ni suala nzima la elimu. Sasa hivi uandikishwaji wa watoto umetoka asilimia 93 mwaka 2015 sasa hivi tuko takribani asilimia 110. Tunapoelimisha vijana wengi maana yake wanakuwa na ubunifu, wanaweza wakabuni bidhaa na huduma mbalimbali na kuzalisha. Kwa hiyo, eneo hili ni muhimu lakini sasa tuangalie na vyuo vya maendeleo, kuna maeneo ambayo tuna miradi ya mkakati (flagship projects) tunahitaji vyuo vya maendeleo ambavyo vitasaidia ku-boost miradi ile. Kwa mfano, maeneo ya Miradi ya Mchuchuma na Liganga, Mwalimu Nyerere Hydroelectric Power, tuhakikishe tunavyo vyuo vya kutosha ili kuimarisha vijana ili waweze kupata ajira na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Ludewa mpaka sasa hawana chuo cha VETA. Nitumie nafasi hii kwenye mpango huu tuone namna gani tunaweza tukatumia force account ili waweze kuweka VETA pale ambayo ita-boost Miradi ya Mchuchuma na Liganga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nipongeze sana Mradi wa Mchuchuma na Liganga upo kwenye Ilani na pia umeelezwa vizuri sana kwenye Mpango. Pamoja na hiyo, tuangalie suala zima la fidia kwa wananchi kama tumeshalikamilisha siyo tu katika Mradi huu wa Mchuchuma na Liganga lakini na miradi mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika maeneo ya madini kuna suala la wachimbaji wadogo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kupata nafasi hii. Nianze kwanza kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Ofisi yake imefanya kazi kubwa nzuri kwenye utekelezaji wa hii Ilani kipindi kilichopita tumeona na sisi Watanzania tunamatarajio makubwa sana.

Mheshimiwa Spika, nikimpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu bila kumpongeza Mheshimiwa Rais, Mama yetu mpendwa Mama Samia nitakuwa sijakamilisha itifaki. Nichukue nafasi hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Mama Shupavu, Mchapakazi, Hodari na Watanzania tupo nyuma yako Mheshimiwa. Vilevile nitambue maendeleo makubwa ambayo yalifanyika na Baba yetu Mpendwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa ambayo ilikuwa imefanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, moja kwa moja naomba niende katika suala zima la asilimia kumi za halmashauri. Katika halmashauri zetu tumekubaliana kwamba tutatenga asilimia kumi kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu. Kwa haraka haraka zipo halmashauri ambazo mapato yake kwa mwaka yanafika bilioni tano; kwa lugha nyepesi ina maana kwa mwaka wanatakiwa watenge milioni 500. Na wakitenga ndani ya miaka mitano unapata all most 2.5 bilioni za kukopesha vijana, wanawake na wenye ulemavu. Kuna Halmashauri mapato yake tuchukulie ni bilioni mbili. Maana yake kwa haraka haraka ni kiwango kisichopungua milioni 200 kwa mwaka.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi zinarejeshwa bila riba, lakini hatujasema zile pesa zinazorejeshwa kila mwaka utaratibu wake unakuwaje. Je, zinachanganywa na zile ambazo zinabajetiwa mwaka husika? Na kama kila halmashauri inaweza ikatenga milioni 500 kila mwaka ukachanganya na zile zinazorejeshwa kutoka mwaka uliopita maana yake mfuko huu ni mkubwa sana.

Mheshimiwa Spika, tunapozungumzia uchumi wa kati, uchumi shindani hili ndilo eneo ambalo hata changamoto ya ajira kwa vijana kwa wanawake na walemavu tunaweza tukapata majibu ya kutosha. Kwa hiyo mfuko huu tuungalie vizuri sana; yale marejesho yanapoingia kwenye akaunti what next? Kila Halmashauri baada ya kutoa kwa vikundi wamerudisha, sasa sheria lazima itafsiri, pale ambapo pesa zimerudishwa zinachanganywa na za mwaka huu au utaratibu wake unakuwaje…

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, taarifa

SPIKA: Ndiyo taarifa.

T A A R I F A

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, naomba kumpa taarifa mzungumzaji kwamba…

SPIKA: Aah sawa, Mheshimiwa ni Viti Maalum Tanga Engineer

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Haya.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, naomba kumpa taarifa mzungumzaji kwamba kwa mujibu wa ile sheria iliyoruhusu kutumika asilimia kumi imeweka wazi kwamba ile pesa ni Revolving Fund and The Rollover Fund. Kwamba hata mwaka ukipituka (ukiisha) ile hela itaendelea kuwepo pale na hata marejesho ni sehemu ya mkopo unaokuja. Imeweka wazi kwamba lazima kila Halmashauri ifungue akaunti ambayo pesa zile zitawekwa zote za kwa pamoja na kila zinavyoji-accumulate inakuwa next amount ya kuweza kuwakopesha wengine. Kwa hiyo wasiokuwa wanafanya hivyo hawana akaunti na wala marejesho si sehemu ya mkopo unaokuja wanafanya makusudi kwa sababu zao, lakini ile sheria ipo wazi imeelezwa vizuri sana. Ahsante.

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Balozi Dkt. Pindi Chana unapokea taarifa hiyo?

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, pamoja na taarifa hiyo naendelea kuchangia kama ifuatavyo; na imani dakika zangu zitalindwa.

Mheshimiwa Spika, kwamba fedha hizi zitakuwa ni mkombozi sana kwa makundi haya na ni muhimu sana tukaziwekea utaratibu mzuri. Kwa tafsiri hiyo basi, maana yake halmashauri zetu zinapaswa kuwa na pesa ya kutosha sana. Hatuhitaji vijana waende benki kutafuta mikopo ya asilimia 16 au 20 kumbe kuna fedha hizi ambazo zinatengwa kila mwaka na zinatumika kukopesha pasipo riba. Hatutakiwi kuwa kilio cha kusema kwamba vijana hawana ajira, ni suala zima la Madiwani kuzisimamia hizi fedha vizuri na kuona ni namna gani tunaweza tukasaidia vijana na makundi mengine. (Makofi).

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo ningependa kulizungumzia ni suala zima la bima ya afya iliyoboreshwa. Bima ya afya iliyoboreshwa kila kaya ni elfu thelathi na wanatibiwa watu sita hii ni mkombozi mkubwa sana. Maana yake ni kwamba kila mtu ni Shilingi elfu tano kwa mwaka, hii haijapata kutokea. Hizi ni pongezi kubwa sana kwa Serikali yetu ambayo inawalinda wananchi. Changamoto iliyopo hapa mara kwa mara tunapokwenda katika hospitali kufuatia bima iliyoboreshwa kuna shida ya dawa. Eneo hili la dawa lazima tuliangalie tunafanyaje?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mara nyingi wananchi tunapozidi kuhamasisha na nimekuwa nikihamasisha mara kwa mara bima ya afya iliyoboreshwa wanapoenda katika vituo vya afya changamoto imekuwa ni dawa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo wakati umefika sasa wa kulifafanua jambo hili vizuri kwamba bima ya afya iliyoboreshwa ndani yake kuna component gani na zipi hazipo ili mwananchi anapokata bima ajue kwamba matibabu yangu yatakuwa ni haya na haya hayahusiki na bima ya afya; vinginevyo tafsiri yake inakuwa ni tofauti, wakiamini kwamba watapa huduma zote nzuri kwa wakati. Na wanapoenda wananchi wetu, na sasa hivi idadi ya watu ni milioni 60 wakakosa hii huduma hususan dawa katika vijiji vyetu, katika wilaya zetu kwa kweli eneo hili lazima tuwe na majibu. Na tunatakiwa tuwe transparent ni namna gani tunaweza kuboresha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni suala la mahindi, na wananchi wamenituma wa Mkoa wa Njombe na mikoa mingi ya kusini na Iringa. Mahindi wanasema wanalima vizuri sana, wanaweka mbolea, mbegu changamoto ni masoko. Sasa hivi tuna mahindi mengi na tutashukuru sana tukipata delegation ya NFRA hata kesho waende wakanunue mahindi kwa wakulima. Wananchi wetu asilimia sitini wamejikita kwenye kilimo, sasa wanapopata mazao lakini wakakosa masoko kwa kweli inakuwa changamoto kubwa ilhali wamegharamia mbolea. Mahindi hivi sasa mahindi haya yasiponunuliwa maana yake mavuno ya mwaka uliopita yanakutana na mavuno ya sasa kuanzia mwezi ujao mikoa hii ya kusini hadi kufikia mwezi wa sita tunaanza kuvuna mahindi. Kwa hiyo taasisi husika, Wizara husika mahindi yakanunuliwe mapema sana kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na maeneo ya kuuza mahindi yapo mengi wahusika wanajua tunakambi za wakimbizi, mashirika ya kimataifa na tuna nchi jirani wanahitaji sana chakula. Kwa hiyo suala la masoko ya mahindi isiwe changamoto. Wananchi hawa haya mahindi yanasaidia kusomesha Watoto, matibabu na kuendelea kulima.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni lumbesa, suala hili bado limekuwa ni changamoto. Kwa hiyo tuone namna kama tutaweza kuuza bidhaa zetu kwa vifungashio maalum au kwa kutumia vipimo maalum. Endapo mtu anajaza gunia basi tuseme labda viazi au maharage debe moja ni kiasi kadhaa, kilo mia ni kiasi kadhaa. Lumbesa imekuwa ni changamoto na wakati mwingine katika magunia wakiweka zipu bila lumbesa baadhi ya maeneo wanavyoenda kushusha sasa kama soko la Kariakoo wanasema pasipo lumbesa basi bei inashuka chini. Kwa hiyo eneo hili pia tutafute namna gani.

Mheshimiwa Spika, ukitokea mkoa wa Njombe bila kutaja Mchuchuma na Liganga unakuwa bado hujamaliza hotuba yako vizuri. Mradi wa Mchuchuma na Liganga bado kuna maombi kwa wananchi; tupate majibu mazuri kwamba ni lini mradi huu utaanza ku-take off tumekuwa tunapata majibu mara kwa mara kwamba linashughulikiwa, tunashukuru sana ipo kwenye Ilani lakini sasa tunataka mradi huu uanze kazi, aje Mheshimiwa Mama yetu azindue, Rais wetu, aje Waziri Mkuu na tunashukuru alifika pale Njombe, ahsante sana. Tuje tuzindue rasmi mradi huu wa Mchuchuma na Liganga.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Madiwani, bado Madiwani Wenyeviti wa Kamati za Maendeleo za Kata wanaomba waendelee kukumbukwa. Madiwani wanafanya kazi nzuri sana kusimamia utekelezaji wa Ilani. Wanasimamia ukamilishaji wa maboma, ukamilishaji wa shule, zahanati. Kwa kweli maboresho tunaomba yaangaliwe. Madiwani wanafanya kazi nzuri hivyo haki zao ziendelee kuangaliwa; ni namna gani tunaboresha haki za Madiwani. Eneo hili ni muhimu sana tuone namna ya kuboresha.

Mheshimiwa Spika, na tunaposema Madiwani timu yao inakwenda pia na Wenyeviti wa Vijiji lakini focus kubwa tuanze kwanza na kwa Madiwani. Hawa ni watu wanaokaa katika kata siku zote, wanashughulika na changomoto aina mbalimbali katika Serikali za Mitaa. Kwa hiyo Madiwani wamekuwa wanachapa kazi sana, wanawajibika sana usiku na mchana, masaa ishirini na nne wako pale na wananchi kwa hiyo Madiwani tuone ni namna gani tunaendelea kuwasaidia... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: …Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Mchuchuma na Liganga; je, Mradi wa Mchuchuma na Liganga utaanza lini? Mbona umetengewa fedha chache sana Mchuchuma na Liganga.

Kuhusu diplomasia ya uchumi (economic diplomacy) taarifa mbalimbali za biashara na viwanda ziende katika Balozi zetu ili waweze kuwajibu haraka wawekezaji huko huko Ubalozini.

Katika Balozi zetu tupeleke trade attaches na tuwape link kila Balozi ili wawasiliane na Wizara ya Viwanda kupata taarifa muhimu kwa ajili ya masoko ya korosho, chai, pamba parachichi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, parachichi Njombe; parachichi inahitaji muuzaji wa kuuza nje aje na accreditation registration na registration hii hufanyika kwa gharama kubwa sana. Wizara ina mpango gani wa kusaidia wakulima wa Njombe wa zao la parachichi.

Kuhusu mahindi; zao la mahindi Wizara iweke mkakati wa masoko ya uhakika, hivi sasa bei ya mahindi kwa debe ni shilingi 4000; pembejeo ni gharama sana, Wizara isaidie bei ya mbolea na pembejeo ishuke.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, lakini ili kutimiza itifaki nampongeza sana Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan. Kwa kweli Tanzania inang’ara, amefanya ziara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki tunamshukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu viwanja na majengo mengi yamezungumzwa; mimi nitazungumza kidogo ili ku-avoid kurudia.

Mheshimiwa Spika, umefika Nairobi kwenye ule Ubalozi tuna kiwanja kile, muda mrefu sana. Sasa hivi majengo haya ambayo Waheshimiwa wengine wamezungumza, sio lazima tujenge kwa kutumia mtaji wa Serikali, tunaweza tukajenga kwa kutumia public private partnership, unaweza ukaingia mashirikiano na taasisi mbalimbali. Nachukulia mfano, labda CRDB Bank wanataka kufungua branch pale, kwa hiyo, CRDB Bank mnakubaliana public private partnershipn sisi uwekezaji wetu unakuwa ni ile ardhi. Kwa hiyo, ningeomba eneo hilo la majengo na viwanja tuweke kipaumbele sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tujitahidi kuendelea kuwapa viwanja Mabalozi hapa Dodoma sasa hivi ndio makao makuu, tutafurahi makao makuu tuanze kuona bendera za Mabalozi zinapepea. Ubalozi wa nchi hii uko hapa Dodoma, Ubalozi wa nchi hii na tukiwapa viwanja Balozi hizi, kimsingi huwa tunabadilishana, ile good gesture ambayo sisi tumewaonesha na wao hivyo hivyo wanatupa viwanja kule katika makao makuu ya nchi zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nipongeze sana Mheshimiwa Waziri hapa mtusaidie na Naibu tuna imani kubwa sana na ninyi. Hata zile Balozi ambazo hazina ofisi hapa Tanzania, ziko Balozi ambazo zina-serve Tanzania, lakini wameweka ofisi zao katika nchi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki na hapa mimi nakuja na swali. Tunatambua kwamba tunazo Balozi takribani 30 hazina ofisi Tanzania; tujiulize kwa nini? Balozi hizi ambazo wanakuja kufanya kazi na sisi wana-present credential hawana ofisi tuwashawishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unakuta hizi Balozi nyingi zimekaa katika nchi fulani na zingine nchi fulani, sisi tujiulize tatizo ni nini hawaweki ofisi hapa? Tuwape incentive kama ni masuala ya VAT huwa wanadai tuwarudishie kwa wakati, mawasiliano, tuimarishe. Ubalozi mmoja ukiwepo hapa Tanzania wanatumia mafuta, wataajiri vijana wetu hadi wa kule Njombe, huko Ludewa wataajiriwa, kutakuwa kuna local best staff, wahudumu gardener, wale watu wa security, uchumi unaongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna baadhi ya nchi yaani wao uchumi wao unaongezeka kwa kuamua tu kuweka taasisi za Kimataifa, dola zinapita mishahara kwenye account, you see. Hizi Balozi 30 naomba tu-pay attention, hatujachelewa na Balozi zingine mpya ambazo zinaendelea kuweka mashirikiano na Tanzania, tuombe wanavyokuja kuomba kuanza Ubalozi na sisi tuombe waweke ofisi. Mzunguko wa fedha ukiwa na Ubalozi mmoja tu, matumizi ya Balozi moja kwa hizi nchi za nje zikiwa hapa kwetu, unakuta sio chini ya dola 60,000 kwa mwezi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bado hapo mishahara inapita kwenye Mabenki kwa hiyo, uchumi huu utaongezeka. Kwa hiyo, niombe sana Madame Waziri tuna imani utusaidie Naibu Waziri, Katibu Mkuu wote hawa ni wataalam ma-guru wa foreign. Balozi hizi zije na watoke Tanzania kwenda nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoa huduma, ku-serve au waende nchi za SADC kutokea Tanzania. Wanapoenda wanatumia ATC ni mfano tu, kwa hiyo, uchumi utabadilika

kwa kiasi kikubwa sana. Kwa hiyo, naendelea kuunga mkono hii hoja na hizi changamoto ndio naziweka mezani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la watumishi limezungumzwa; kuna baadhi ya Vituo hatuna Maafisa wa Uhamiaji na kuna kada zingine nyingi kwa kweli ambazo ni muhimu sana. Kada hizi za afisa wa uhamiaji pale unahitaji utoe Visa, tourist visa, unahitaji utoe business visa, unahitaji utoe multiple entry visa, sasa kada hizi wakati umefika tuone namna gani wataalam hawa wanaenda.

Katika hilo hilo eneo la visa, kuna visa inaitwa referred visa sasa hivi visa zinatolewa kwenye mtandao. Lakini hiyo referred visa mara nchi hiyo inapoomba kupata visa watu wake, lazima taarifa ziende makao makuu ya nchi na wafanyie upekuzi. Wakati mwingine suala hili mchakato wake unachukua muda mrefu, tuko kwenye uchumi shindani, tuangalie list yetu ya Referred Visa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unakuta sisi tumewekea nchi kadhaa referred visa, lakini ile nchi ambayo sisi tumeiwekea referred visa yamkini yenyewe haijaweka referred visa kwa Tanzania. Kwa hiyo, naomba tu-review list ya nchi ambazo tunazitambua kama nchi za referred visa. Leo hii mtalii anakuja anasema, nataka kuja Tanzania tunasema nchi yako iko kwenye referred visa, subiri wiki tatu, ataangalia Mlima Kilimanjaro kutokea nchi jirani, ataenda nchi jirani atasema beach ya Zanzibar inafanana na beach fulani ya nchi jirani, ata-opt kwa sababu ile nchi jirani inampa Visa on arrival, lakini sisi tunamuambia you know Sir referred visa you have to wait two weeks. Anakuambia vacation yangu imeisha, my holidays are gone I can’t wait, ataenda nchi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, twende na reforms, Waziri mtusaidie tunaomba sana. Wenzetu nchi jirani wameshabadilika hamna ma-referred visa inategemeana. Huko nyuma wakati tunapigania uhuru na nini changamoto zilikuwepo, sasa hivi kuna mitandao watu wa usalama wanajua kujua kama huyu ni criminal ama vipi?

Mheshimiwa Spika, eneo lingine kwa haraka haraka diplomasia ya uchumi, Balozi zetu nawapongeza sana Mabalozi wote, wanafanya kazi kubwa nzuri sana, diplomasia ya uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapa tuendelee kuimarisha tunahitaji masoko ya mbao za kutoka Njombe, Mufindi. Mimi nashukuru sasa hivi mbao za Mufindi, Njombe tumejitahidi zinakwenda mpaka Somalia. Lakini ili jambo hili lifanikiwe mazao kama mahindi, viazi, korosho, pamba lazima tupeleke taarifa za kutosha katika Balozi zetu kiasi kwamba mwekezaji anapokwenda pale Ubalozini anapouliza kwamba una tani ngapi za pamba, una tani ngapi za korosho isiwe tena, ngoja kwanza niwasiliane na Wizara waniletee, inachukua muda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini taarifa hizi zikiwa kwenye website za Balozi zetu e-government yaani ni haraka sana wawekezaji watakuja, tutapata masoko na watatangaza fursa mbalimbali kwa hiyo nawapongeza sana Mabalozi wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine, ambalo ni muhimu, tufungue Balozi mpya, tusiogope kufungua Balozi mpya. Hivi karibuni tumefungua Balozi Mpya takriban saba/nane ni pongezi nyingi lakini dunia ni kubwa we need to connect. tuendelee kufungua Balozi. Unaweza ukachagua nchi ukafungua Ubalozi pale unaamua kupelekea chai, unasema nchi fulani ni soko langu la uhakika la chai. Sasa hivi tunauza chai takriban dola 7 kwenye mnada wa Mombasa, lakini chai inaweza kutujengea Bandari ya Tanga.(Makofi)

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Sophia Mwakagenda nimekusikia.

T A A R I F A

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ninaomba nimpe Taarifa mzungumzaji anayezungumza sasa kwamba anachokisema ni sahihi, Guangzhou ni mji ambao ni mji wa kibiashara lakini pale hatuna Balozi mdogo ambaye angeweze kusaidia wafanyabiashara wetu wakienda wakasaidiwa kwa haraka. Ninamuunga mkono na ninampa taarifa hiyo. (Makofi)

SPIKA: Taarifa hiyo unaipokea Mheshimiwa Hazara.

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, Taarifa hiyo naipokea na nimekumbuka kuweka msisitizo chini ya Balozi kuna Honorary Consul, you see kwa hiyo tunaweza tukaweka Consular Mkuu, pia tunaweza tukaweka enhee Honorary Consul, kwa hiyo haya yote yanawezekana utakuta nchi hatuna uwakilishi, hatuna Honorary Consul, hatuna Consular Mkuu, Consular General, we need to connect, huu ni wakati Mheshimiwa Waziri tusaidie, tusaidie, tuna Balozi chache sana tukilinganisha na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za SADC. Wenzetu wanafunguka, wanafunguka wakati umefika vijana wetu hawa wakasome nje, wapate fursa mbalimbali za masomo, utaalam wa aina mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sijasikia kengele nadhani, naendelea, ahsante.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni diaspora; diaspora Watanzania waliopo nje wanarudisha fedha nyingi sana nyumbani. Wanasaidia kuongeza uchumi, duniani kote diaspora wamekuwa ni tool muhimu sana. Kwa hiyo, diaspora wetu ambao wako nje ni pongeze sana Mabalozi wamekuwa wakiwasajili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kwanza kusema kwamba naunga mkono hoja. Nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wetu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri Mheshimiwa Eng. Masauni. Kwa kweli nawapongeza sana. Ili itifaki iwe imezingatiwa, nampongeza sana Mheshimiwa Rais wetu, mama jembe, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan. Hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli bajeti hii ni bajeti ya mfano. Nina salamu nyingi kutokea katika Mkoa wetu wa Njombe. Wananchi wa Njombe wanashukuru sana, kwa kweli wanasema hii bajeti ni ya kuigwa, ya mfano, kwa sababu inakwenda kuweka pesa kwenye mifuko ya wananchi. Kumekuwa na maboresho makubwa sana upande wa kodi na sasa pesa zinakwenda kuwepo kwenye mifuko ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kwa moja naanza na suala zima la Madiwani. Suala la Madiwani nimekuwa nikiliongelea sana hapa na ninashukuru Serikali kupitia Wizara imesikia kilio hiki cha posho za Madiwani na Serikali wamesema watalipa. Tunazo Halmashauri grade A, B na C. Hapa kuna point mbili; kuna suala la Serikali kuchukua dhamana ya kuwalipa Madiwani moja kwa moja kwenye accounts zao na vile vile kuna suala la kuongeza kiwango cha posho za Madiwani. Haya ni mambo mawili tofauti. Tutaomba wakati wa kutoa ufafanuzi, haya mambo mawili yaeleweke. Tunapochukua dhamana ya kuwalipa Madiwani moja kwa moja kupitia Serikali Kuu: Je, viwango vinakwenda kubadilika au viwango ni vile vile? Kupitia ALAT, maombi ya Madiwani ni kwamba viwango pia viboreshwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyeki, eneo lingine upande wa Serikali za Mitaa ni malipo ya haki ya madaraka kwa WEO na Makatibu Tarafa. Kwa upande watendaji wetu, unakuta mtendaji mmoja ana vijiji tuseme vitatu au vine, analipwa shilingi 100,000, posho hiyo, jambo ambalo nalipongeza sana na kuliunga mkono. Katibu Tarafa, ana vijiji takribani mara nne ya yule Mtendaji wa Kata. Sasa huyu katibu wa Tarafa naye tunamlipa shilingi 100,000 na huyu WEO naye shilingi 100,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ombi kutoka kwa Makatibu Tarafa ni kwamba kile kiwango cha mafuta walichokuwa wanapewa kutoka kwa ma-DAS kibaki pale pale, waendelee kusaidiwa. Kwa hiyo, hii shilingi 100,000/=, wanayopewa Makatibu Tarafa, isiwe mbadala kwamba hawatapewa tena ile pesa waliyokuwa wanapewa kutoka Ofisi za ma-DAS, kwa sababu kazi za Makatibu Tarafa ni zaidi ya kazi ya Watendaji wa Kata. Sasa viwango hapo vinafanana. Kwa hiyo, ni ombi maalumu ambalo tunaweka mezani kwamba kuna kiwango walikuwa wanapewa kutoka ofisi ya DAS kiendelee kuzingatiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha hilo, niendelee kuomba Wizara isaidie sana mashine za ki- electronic. Watendaji wetu wa kata wote wapewe zile mashine za kukusanyia mapato za ki-electronic ili mapato yasipotee, tunapojadili bajeti, mabato yaeleweke. Baadhi ya Watendaji wa Vijiji bado wanakusanya mapato kwa mkono (manually), siyo electronic.

Kwa hiyo, tunaomba sana mashine za kukusanyia mapato za ki-electronic ziende vijijini. Katika masoko bado tunakusanya mapato kienyeji. Katika stendi zetu bado tunakusanya mapato kienyeji bila mashine. Suala hili la mashine za ki-electronic tunaomba sana lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo pia linaweza lika-boost mapato, tunayo mikoa mipya; Njombe ni miongoni mwa mikoa ambayo ilipatikana dakika za hivi karibuni; Simiyu, Geita, Katavi na mengine. Mikoa hii mipya makao makuu ya mikoa hii mipya, mpaka leo makao makuu mengi hayajawa Manispaa. Tuangalie Makao Makuu ya mikoa hii mipya kama inakidhi kuwa Manispaa. Naleta salam kutoka Mkoa wa Njombe. Njombe tunaomba iwe Manispaa. Halmashauri ya Mji wa Njombe tumeshakaa katika vikao vya DCC na tunakidhi. Tufanyie…

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Pindi Chana subiri.

Mheshimiwa Kanyasu Taarifa.

T A A R I F A

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu kumpa taarifa mchangiaji. Kwanza anachangia vizuri sana na moja ya mikoa mipya anayozungumza Makao yake Makuu ni Geita Mjini, ambayo imekidhi viwango vya kuwa Manispaa tangu mwaka 2018. Nilikuwa nampa tu taarifa tu Mheshimiwa.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naipokea taarifa hiyo na nadhani hizi salamu sasa zinazidi kukamilika kwa Serikali. Hii mikoa ni yetu, tunaweza tukasubiri vile vigezo kwamba kwa sababu tumeamua tuwe na mikoa mipya, mikoa hii mipya lazima viongozi wetu wa Kitaifa, Waziri Mkuu aende pale. Sasa mkoa mpya usipoweka airport, Waziri Mkuu anaendaje pale?

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Pindi, Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Jacqueline.

T A A R I F A

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nataka tu nimpe taarifa mchangiaji anayechangia sasa kwamba anapoendelea kuchangia, akizungumzia maslahi ya Mkoa wa Njombe asisahau kuzungumzia maslahi ya Mkoa wa Ruvuma jirani yake, kwamba Mkoa wa Ruvuma nao pia ni Mkubwa sana, unahitaji kugawika ili tuweze kupata Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Selous. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Pindi Chana, unaipokea hiyo taarifa?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni dalili kwamba upande wa Serikali za Mitaa tukiboresha mifumo mapato yanaongezeka; unapofanya Manispaa au mikoa miwili, miundombinu inaongezeka. Kama pale Njombe tunakuwa na uwanja wa ndege, bosi wetu Waziri Mkuu akija, ana-fly kutoka Dodoma. Ana-land pale, anatembelea mashamba ya parachichi, hatumtoshi by road, kwa sababu anakazi nyingi. Kwa hiyo, tunaoma Mkoa wa Njombe na mikoa ya mingine ambayo ni mipya ipewe Manispaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapokuwa na Manispaa, kuna miradi ya kimkakati. Tuchukulie mfano stendi mpya ya mabasi, ile ya pale Dar es Salaam, Mbezi Luise. Sasa mradi kama ule utawekaje mahali ambapo ni Town Council, siyo Halmashauri ya Manispaa? Maana kuna miradi inaenda kwenye jiji, kuna miradi inakwenda Manispaa na miradi inayokidhi Town Council. Hii mikoa tuliamua sisi iwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni wakati muafaka sasa tuone namna gani Makao Makuu ya mikoa hii mipya yanakuwa Manispaa kwa maslahi ya Watanzania na kwa faida ya Watanzania. Tuchukulie mfano, pale Njombe ikiwa Manispaa, unakuta bidhaa zote za kilimo kutokea Makete lazima zipite Manispaa. Viazi, chai inayotoka Lupembe, lazima ipite pale Njombe Manispaa. Kule Ludewa kuna Ziwa Nyasa, samaki lazima zipite Manispaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, inapokuwa manispaa miundombinu, barabara za lami, mabenki uwekezaji unakuwa mkubwa kule ziwani kule ni mbali na tuendelee kuwa wanachama wa maziwa makuu sisi kama nchi tuendelee kuwa wananachama wa great lakes network itatusaidia sana kuweza kufanikisha uwekezaji katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni suala zima la mchuchuma na Liganga kwa kweli nina salute Mheshimiwa Rais amezungumzia Lichuchuma na Liganga. Lichuchuma na Liganga wanasema kuna political will. Rais wetu mama yetu mpendwa amesema tatizo ni nini leo Waziri amejibu maswali vizuri sana hapa swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo kuhusu Mchuchuma na Liganga. Tunapongeza sasa tuanze madiwani wanaongelea Wabunge Mchuchuma na Liganga Mheshimiwa Rais Mchuchuma la Liganga sasa shida iko wapi? Hapo sijaelewa kwa hiyo suala hili Mheshimiwa tuimairishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TARURA naunga mkono, TARURA tumetenga hizo milioni 500 kila jimbo tukumbushane TARURA ilikuwepo ipo na itaendelea kuwepo sasa hizo pesa zinapoenda tunatoa shukrani nyingi lakini ionyeshe tofauti isiwe kama wakati ule wa mwanzo wanasema business as usually tuone namna gani pesa hizi zikienda zionyeshe tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ni muhimu ni mapato yanayotokana na uchumi wa blue. Uchumi wa blue ndani yake kuna bahari, uchumi wa blue ndani yake kuna costal area zote, uchumi wa blue ndani yake kuna maziwa Tanzania peke yake tuna maziwa yasiyopungua tisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na haya maziwa lakes great lakes ni muhimu sana haya maziwa, Mungu ametuletea bahari atulipiii hiyo bahari ina samaki tunaweza tukavua kwa wakati wowote kwenye haya maziwa tunavua. Kwa hiyo, muhimu sana tuangalie uchumi wa blue.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ya pili naunga mkono hoja; ahsante. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nianze kwanza kuwashukuru Wenyeviti wote wawili ambao asubuhi ya leo wamewasilisha Taarifa za Kamati zote mbili na taarifa hizi ni muhimu sana. Sisi Wizara tunamshukuru sana Mwenyekiti, Mheshimiwa Makoa pamoja na Mheshimiwa Kihenzile kwa sababu, Kamati hii imekuwa ikitupa mawazo muhimu sana. Tumekuwa tukishauriana namna gani bora ya kuendeleza masuala mazima ya maliasili na utalii, kwa kweli, tunaishukuru sana kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imeleta taarifa yake na kuna maeneo mengi Kamati imeelekeza tuboreshe. Kwa hiyo, moja kwa moja niseme kwamba, ushauri wote na maoni waliyotoa tunayapokea, tutayafanyia kazi na tutaendelea kuyawasilisha katika Kamati kama ilivyo ada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo moja ambalo limezungumzwa kwa mfano habari ya bajeti, kwamba, zipo taasisi zilikuwa na mbuga 16, lakini sasa hivi TANAPA inasimamia mbuga 22, TAWA, Ngorongoro, ni namna gani tunaweza tukaongeza mapato ikiwa ni pamoja na retention.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni masuala ya msingi sana, wakati mwingine kunakuwa na majanga ya moto, kwa hiyo, inakuwa ni changamoto kutegemea OC. Katika maeneo kama haya lazima kuwe kuna bajeti ya kutosha ya kuweza kuhimili mikiki. Wageni watalii wanapokuja lazima tuhakikishe madaraja yako salama na barabara ziko salama. Kwa hiyo, Kamati imekuja na ushauri wa msingi kabisa nasi Serikali tumesikia, tunasema haya waliyopendekeza Kamati ni mambo ya msingi na tutayazingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia imetukumbusha katika taarifa yake na waliochangia kwamba, zoezi la kuhamisha watu kwenye makazi bora kutoka Ngorongoro kwenda Msomera ni jambo ambalo linapaswa kuendelea. Nasi tunasema jambo hili linaendelea, mpaka sasa tumeshahamisha kaya kwa hiyari takribani 551, watu 3,010, mifugo isiyopungua 15,321 na zoezi hili linaendelea. Lengo la kuhamisha kwanza ni kuhakikisha kwamba, watu wetu wanapata makazi bora, wanapata eneo ambalo wataweza kufuga, kulima, vitu ambavyo walipokuwa wanaishi kule Ngorongoro sheria haziruhusu; haziruhusu kilimo, haziruhusu ujasiriamali, kuna vijana wanataka kufanya shughuli za bodaboda, akinamama wafungue shughuli zao, lakini Ngorongoro hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunachokifanya ni suala la haki za binadamu. Tunapozungumzia haki za binadamu ndugu zetu wanaoishi Msomera ni muhimu wakapata maeneo ambayo wanaweza kuishi kama wananchi wengine; wakaweza kumiliki bodaboda, kumiliki usafiri, kumiliki ardhi. Sasa wanapokuwa wanaishi ndani ya eneo la Ngorongoro huko kuna restrictions, lakini Serikali hii inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ikasema hawa watu lazima wapate maeneo bora, maeneo mazuri ya kuishi. Huo ndio mkakati tuliokuwa nao kama Serikali na zoezi linaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nishukuru sana maoni ya Wajumbe wa Kamati pamoja na Wabunge katika michango yao mbalimbali, kwamba, tuangalie Sheria ya Kifuta Jasho na Kifuta Machozi. Hii ni kweli kabisa, wakati umefika sasa sheria hii tuifanyie marekebisho, Wizara yangu inatambua hilo na sheria hii lazima ifanyiwe marekebisho. Tumeshazungumza pia na Attorney General, tuone namna gani ikiwezekana ije tushirikishe wadau. Hii ni sheria ya muda mrefu, kwa hiyo, ni muhimu sana sheria hii ikafanyiwa marekebisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ningependa kuzungumzia ni kwamba, tupo kwenye kuona namna gani ya kuendelea kudhibiti changamoto iliyopo kati ya wanyama wakali pamoja na binadamu. Hili ni eneo ambalo tunaendelea nalo, tmeshajenga vituo vya askari 16 na tunaendelea na sasahivi tumesema tuanze kuweka mabwawa ndani ya maeneo ya hifadhi. Kutokana na hela za UVIKO tumepata mitambo, tuchimbe mabwawa kule ndani ili wanyama hawa wanaotoka kwa ajili ya kutafuta maji waweze kukaa kule ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tumeanza kuchimba, Ruaha National Park tuna mitambo tunachimba maji yapatikane. Tunaendelea na uchimbaji wa mabwawa katika maeneo mbalimbali, lakini sasa hivi pia kuna zoezi la kuvalisha kola, baadhi ya makundi ya tembo tunavalisha GPS collar; ukivalisha collar unaweza ukaona kwamba, hili kundi sasa linatoka kwenye hifadhi, tufanyaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ya Lindi, Mtwara, tumeanza kuvalisha collar. Kulikuwa kuna tembo, kulikuwa na changamoto na tumetuma hadi helicopter kuhakikisha kwamba, wanasogeza wale tembo, warudi katika maeneo yao ya hifadhi. Kwa hiyo, haya ni maeneo ambayo tunaendelea nayo kuhakikisha kwamba, Vituo vya Askari vinaendelea kuwepo ili wananchi wetu waendelee kuwa salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ningeomba pia, kuendelea kukumbushana ni habari ya mifugo kutoingia katika hifadhi. Ndugu zangu tumekuwa na changamoto kubwa sana, tumeenda kule Usangu tumebadilisha GN 28, Kamati ya Mawaziri Nane imezunguka nchi nzima kuona nini tunafanya katika vijiji 975. Maeneo mengi tumesema tuwaachie wananchi, ili maeneo ya hifadhi yawe salama, ikiwa ni pamoja na eneo lile la Usangu tumebadilisha GN kuwaachia wananchi ili sasa maeneo ya hifadhi yabaki salama, wananchi wanahitaji maeneo ya kilimo. Tumeachia hadi ranch ya Usangu, imetoka kwenye Hifadhi ya Ruaha National Park, ili watu wapate maeneo ya kufugia, wapate maeneo ya kilimo ili hifadhi zetu ziwe salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe rai kwa Watanzania wenzangu kwamba, tujitahidi sana kutoingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi. Askari wetu wanakuwa na changamoto sana kusogeza hiyo mifugo na wanajitahidi sana kuhakikisha kwamba, wanalinda raia, Jeshi la Uhifadhi liko pale, wanalinda maliasili hizi na tuna maeneo mengi, tusipoyalinda sote tutapata changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo haya ya hifadhi, maeneo haya ya national park, misitu, ndani yake kuna vyanzo vya maji. Sasa hivi lazima tujaze Mwalimu Nyerere pale Hydro Electric Power, namna yoyote ya kuruhusu mifugo, kilimo, shughuli za binadamu, tunaweza kuwa jangwa. Kwa hiyo, nitoe rai tushirikiane Waheshimiwa Wabunge tutoe elimu, tuwakumbushe Waheshimiwa Madiwani tushirikiane kusema kwamba, maeneo ya hifadhi ni kwa maslahi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi Tanzania tuna chakula cha kutosha hadi watu wa nchi jirani wanakuja kununua, hii yote ni kutokana na mvua ya kutosha na mvua hii inategemeana na misitu tunavyoilinda. Kule juu ukienda ramani ya Afrika tayari wameshakuwa jangwa, nchi za pale juu nisingependa kuzitaja. Sasa ni namna gani tunashirikiana kulinda hizi hifadhi, maliasili hizi, maana tunasema tumerithishwa, tuwarithishe, namna yoyote ya kuachia sote tutapata kazi. Kwa hiyo, nitoe rai ndugu zangu tuangalie namna gani tunadhibiti mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemshukuru sana Waziri wa Mifugo amesema ikiwezekana sasa mifugo badala ya kuitembeza, kuchunga, tufuge. Unakuwa na eneo lako zuri, unaweka josho, unaweka sehemu ya kunyweshea maji, lakini mifugo inapozunguka nchi nzima hii ni changamoto. Tuone namna gani tunajipanga kwa mifugo yetu tuweze kuweka eneo moja, kuna watu wana viwanda vya maziwa, watu hawa wanafuga eneo moja badala ya kuzunguka nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie pia nafasi hii kuwashukuru sana Jeshi la Uhifadhi na maoni ya Waheshimiwa Wabunge kwamba, maslahi na mafao ya askari wetu wa Jeshi la Uhifadhi yaangaliwe. Waheshimiwa wamechangia akiwemo na Mheshimiwa Soud. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni kumekuwa na changamoto, askari wetu wamekuwa wakivamiwa. Kuna askari amevamiwa na mshale wenye sumu hivi karibuni, tukio hilo limetokea Serengeti. Jana kuna askari wawili Uvinza na wenyewe wamevamiwa, askari hawa wanajitoa kwa ajili ya kulinda rasilimali za nchi yetu kwa faida yetu sote, maeneo haya wanaingia majangili, wengine wanatoka nchi za Jirani, ni hatari sana. Sasa askari wanapojitoa kulinda maeneo yetu ya rasilimali wanavamiwa, wanapigwa mishale, hili ni jambo ambalo naomba nitumie nafasi hii kwa kweli, kulikemea na kulaani kwa nguvu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumbuka askari hawa wamebeba silaha, wanakuwa ni wavumilivu, wanapigwa mishale na wale askari walinyamaza kimya kumsaidia mwenzao mpaka kumfikisha hospitali na tumempoteza kijana wa miaka 42, Deus Mwajegele. Kwa hiyo, niombe sana, tuwape ushirikiano, tuwalinde askari wetu, tusichukue sheria mkononi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza kabisa, nichukue nafasi hii kushukuru maoni ya Kamati yetu ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Elimu, Utamaduni na Michezo lakini pia nitumie nafasi hii kuwashukuru wachangiaji wote. Tumepata wachangiaji takribani 16 na michango hii yote tutaiwasilisha kwa maandishi kila hoja. Tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala kubwa hapa kwenye Wizara yetu ni habari ya bajeti. Mambo mengi mazuri yamezungumzwa yafanyike, reforms na kikubwa kabisa ambacho kimezungumzwa hapa ni suala zima la bajeti. Hili ni kweli kabisa, bajeti upande huu wa masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo hii ambayo leo tumekuja kuomba Bunge letu bilioni 35. Kama alivyosema Waziri mwenzangu Mheshimiwa Mwigulu, kwamba hili ni eneo ambalo kimsingi tunaendelea kuangalia namna gani tuendelee kuliboresha kwa kushirikisha sekta binafsi na wachangiaji wengi wamesema tuone namna gani tunashirikisha sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesema tutakwenda kukarabati uwanja wetu wa Benjamin Mkapa. Hivi sasa kuna mechi ambayo tunaisubiri kati ya Tanzania na Niger itachezwa mwisho wa Mwezi wa Sita na niwatangazie Watanzania kwamba, mara baada ya mechi hii kukamilika tutafunga uwanja huu tayari kwa ukarabati. Ninashukuru sana kwa maoni ya Kamati walivyosema kwamba tubakize Benjamin Mkapa kwa ajili ya mechi kubwa tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huko nyuma tulikuwa tunautumia uwanja huu ambao una uwezo wa viti takribani 60,000 hata kwa ajili ya shughuli mbalimbali za matamasha kama vile mahubiri, sala mbalimbali tulikuwa tunatumia lakini sasa tutatumia viwanja mbadala na uwanja huu ubaki kama hazina na alama ya Taifa letu. Kwa hiyo, tutakwenda kukarabati uwanja huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kukarabati tunatarajia kujenga recreation center pale nyuma ya uwanja wa Benjamin Mkapa na recreation centre nyingine itakuwa hapa Dodoma, itakuwa ni viwanja viwili Dodoma pamoja na Dar es Salaam, kama alivyosema Naibu Waziri tayari Mkandarasi amekwisha kabidhiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunakwenda kujenga arena, wamezungumza hapa watu wanahitaji arena, haya ni maeneo ya kipaumbele, tayari tuna eneo la Kawe pale tutajenga arena pia tutajenga stadium mbili hapa Dodoma na nyingine tunatarajia kujenga Arusha ikiwa ni maandalizi pia ya kuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON 2027.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili ukidhi AFCON tunahitaji viwanja nane vya Kimataifa, lakini kwa kuwa tumeomba pamoja na Kenya na Uganda ukichanganya na wanatatarajia kuja Wakaguzi (Inspectors) kutoka Makao Makuu ya CAF hivi karibuni, tayari nimeongea na Waziri wa Michezo wa Kenya na Waziri wa Michezo wa Uganda tunaona namna gani ya kuhakikisha kwamba tunakidhi vigezo na masharti ili tuweze kufanikiwa AFCON 2027. Kwa hiyo miundombinu ya viwanja ni maeneo ya vipaumbele lazima tuone

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo nimeshawasiliana na Waziri mwenzangu wa TAMISEMI pamoja na Waziri wa Elimu. Waziri wa Elimu tumekubaliana kwamba suala la somo la michezo liwe ni miongoni mwa masomo ambayo yanaweza kufundishwa na kufanyiwa mitihani liwepo kwenye mitaala, kwa hiyo, kuna mafunzo ya amali. Suala la masomo ya sanaa, muziki iwe ni miongoni mwa masomo ambayo yako katika curriculum zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa kushirikiana na Waziri wa TAMISEMI na Waziri wa Elimu tumekubaliana kuwa, hakuna kusajili shule ya msingi au sekondari hadi watuthibitishie wana viwanja mahali hapo. Mtoto hawezi kwenda shuleni miaka saba bila kushiriki michezo, O – level miaka minne, A – Level miaka miwili bila kushiriki michezo, anakuja kukutana na michezo University, lazima tuwazoeshe wakiwa wadogo. Kwa hiyo, hiyo ni miongoni mwa mikakati ambayo tunayo kuhakikisha kwamba eneo hili la michezo linaendelea kuboreshwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa michango mbalimbali, kuna hoja hapa kwamba kampuni ya betting ili ipate leseni kigezo iwe ni kudhamini timu ya mpira na sisi kama Wizara jambo hili tunaona ni muhimu tunalichukua tuone namna gani ya kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kushirkisha sekta binafsi pamoja na CSR, tuwe na sports academy za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilithibitishie Bunge lako mpaka sasa Wizara imesajili sports academy kutoka ngazi mbalimbali 180. Hivi sasa hata wadau binafsi wanatengeza viwanja kwa mfano Azam Complex. Pale Morogoro wamekuja kuomba vibali wanaweka uwanja pale, kuna Mmasai mmoja yeye amesema anataka eneo lake litumike kwa ajili ya uwanja wa michezo na ameingia makubaliano na Italy na analeta wataalam wa kufundisha michezo kwa vijana kutoka Italy. Kwa hiyo, hii ni sehemu ambayo pia ni miongoni mwa vipaumbele vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna suala limezungumzwa hapa la Ndondo Cup. Tunaamini kwamba Ndondo Cup ni eneo la kukuza vipaji, pia kwenye mchango wa Mwenyekiti wa Kamati amesema kwamba tuone namna gani ya kurasimisha eneo hili la Ndondo Cup, nasi tunasema kwa kuwa ni eneo ambalo linarasimisha vipaji, Ndondo Cup inaendelea kuwa muhimu kweli. Kwa hiyo, tutaweka utaratibu kwa kushirikiana na wenzetu wa TFF kuona namna gani vibali vinaweza vikatolewa taratibu na wadau wanaotaka kuendesha mashindano haya waweze kushirikishwa na kutambulika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutaendelea kushirikiana na sekta binafsi kama Mabenki kuweza kuuza haki za majina ya viwanja. Kuna baadhi ya viwanja ukienda nchi nyingine unakuta uwanja una jina la benki fulani labda CRDB. Kwa hiyo, hayo ni maeneo ya kimkakati ambayo tunataka tuhakikishe kwamba tunashirikisha sekta binafsi na tuweze kuendeleza eneo hili la michezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mikoa tumezungumza hapa imeonekana kama wasanii wengi, wachezaji wengi wanatokea Dar es Salaam, niendelee kuwahakikishia Waheshimiwa kwamba katika kila Halmashauri tuna Afisa Michezo, katika kila Halmashauri kuna Afisa Utamaduni na Sanaa maeneo haya kuna Kamati maalumu za kichezo na Mwenyekiti wake kwa ngazi ya Wilaya ni DAS na kwa ngazi ya Mkoa ni RAS. Kwa hiyo, nitoe wito sasa kwamba Kamati hizi zinapaswa kukutana na kuweka mikakati ya kutosha na hivi sasa tunakwenda katika michezo mtaa kwa mtaa, tunakwenda katika suala la sanaa mtaa kwa mtaa, tumeingia makubaliano ya michezo mashuleni kwa kushirkiana na FIFA tutatoa mipira 2,000 kila Mkoa katika spirit ya kuendeleza michezo mtaa kwa mtaa. Kwa hiyo, tayari tumekwishaingia makubaliano (MOU) pamoja na FIFA kwa kushirikiana na TFF ili kuona ni namna gani tunaboresha na tunahamasisha suala zima la michezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na swali pia inakuwaje kwamba labda watu wanataka kusajili masuala ya sanaa wasafiriki kutoka mikoani? Sasa hivi kupitia Wizara tunataka kuweka utaratibu wa ku–digitalize. Kwa hiyo, unaingia kwenye www.sanaa.basata.go.tz mahali hapo unaona taratibu zote za kusafiri hauhitaji kusafiri. Unaweza ukawasiliana na Maafisa wetu walioko katika ngazi za Serikali za Mitaa, kila halmasahauri tuna Maafisa Michezo, Maafisa Utamaduni, tunataka kuendeleza eneo hili kwa sababu tunajua linaajiri vijana wengi kabisa na baada ya sensa vijana wapo takribani zaidi ya milioni 30, kati ya idadi ya watu milioni 61 zaidi ya 51 percent ni vijana, ni lazima tuweke mikakati ya kuhakikisha kwamba vijana hawa wanashirikishwa na wako imara kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hayo, tunao Mfuko wa Utamamduni, na mfuko huu kazi yake ni ku-support kutoa mikopo. Tumeshatoa mikopo takribani shilingi 1,077,000,000. Sasa tunaangalia namna gani ya kufika nchi nzima. Mikopo hii wanapewa watu wote; awe ni msanii maarufu, hata asiye maarufu, wote wana haki pale ambapo vigezo na masharti vimezingatiwa. Kwa hiyo, tunaendelea na mazungumzo na Mabenki yetu na taasisi za kifedha. Lengo ni kwamba hizi benki zina branch katika kila wilaya na kila mkoa. Tumeshaanza mazungumzo na benki mbalimbali ikiwa ni pamoja na National Bank of Commerce kuona ni namna gani tunaweza tukaingia makubaliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokuwa na fedha ya kukopesha, tunaipeleka benki, tunasema sasa wewe benki utoe kwa niaba yetu. Huu ni mkakati ambao tumeujadili hapa Bungeni kwa pamoja, pia kuona ni namna gani tunawezesha vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Kwa hiyo, huo ni mkakati ambao tunao, tunataka kila mwenye uwezo wa kupata fursa, kupata mitaji ya kuendeleza masuala ya utamaduni, sanaa na michezo, waweze kupata mitaji. Kwa hiyo, Wizara imedhamiria kuleta mageuzi na tuko imara kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la vazi la Taifa, niwahakikishie Kamati kwamba suala hili ni jambo ambalo tuko makini, tuko serious. Mchakato huu ulishafanyika hapo awali na ulienda hadi ngazi za Wizara, lakini Wizara tulitoa maelekezo mengine kwamba warudi kupata maoni mengine. Wameshamaliza kukusanya maoni Visiwani na Bara na hivi karibuni watakwenda kuwasilisha ripoti maalum kabisa. Tumeshawapa deadline, wahakikishe kwamba suala la vazi la Taifa linakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mdundo wa Taifa, tayari tuna Producer’s Kit ili mtu anapotaka kuweka nyimbo, aweke nyimbo yenye Mdundo wa Taifa. Kwa hiyo, hili la vazi la Taifa tunaelekeza Kamati kwamba wahakikishe wanakamilisha suala hili mapema kabisa liweze kukamilika kwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine kama nilivyosema, maoni yote tunachukua, lakini tunaendelea na suala zima la kubidhaisha Kiswahili. Tunataka Kiswahili kiwe na manufaa, vijana wetu waweze kufundisha Kiswahili, waweze kutoka nje ya nchi, na waweze kuwa Wakalimani. Tuna ushirikiano na nchi mbalimbali kama tulivyosema awali, Ujerumani na hata Spain tayari wameshatuomba tuwapeleke walimu wetu kujifunza Spanish. Kwa sababu ukijua Kiswahili lazima ujue na lugha ya pili ili kuweza kutafsiri; kama ni Kiarabu, kama ni Kifaransa, au lugha nyingine. Maana ukijua tu Kiswahili peke yake, bado, lazima tuwe na lugha ya pili. Kwa hiyo, tunaendelea na mkakati wa kubidhaisha lugha yetu ya Kiswahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye mara kwa mara amekuwa akitoa hotuba hata ngazi ya AU kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo, Watanzania wenzangu, Waheshimiwa Wabunge, tuendelee kutumia lugha yetu hii ya Taifa. Mataifa mengine wanathamini sana lugha zao, wanajali lugha zao. Tumeshatoa kamusi, tuendelee kutumia lugha yetu, tufurahie lugha yetu. Vilevile tunazo filamu kwa lugha ya Kiswahili. Tuwe tunapenda kuangalia sanaa zetu na utamaduni wetu, tuufurahie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kulikuwa na hoja kwa upande wa filamu kuhusu vibali. Vibali vya Filamu tunaendelea kuvitoa kupitia Bodi ya Filamu na sasa hivi mambo mengi tunafanya online, haihitaji mtu kusafiri. Pia tunatoa documentary, siyo tu filamu za kawaida, documentary za kufundisha, Historia na documentary mbalimbali. Huo ni mkakati ambao tunao. Huko nyuma tulikuwa tunatoa filamu 200 kwa mwaka hivi sasa niwahakikishie Wabunge tunakwenda mpaka filamu 2,000 kwa mwaka. Kwa hiyo, hili ni eneo ambalo limechukua vijana wengi na vijana wengi wanakuwa maarufu ndani na nje ya nchi. Kwa hiyo, hii ni mikakati ambayo tunaendelea nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia, nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kweli yeye amekuwa ni chachu upande wa michezo, amekuwa ni kinara kabisa upande wa michezo. Taifa letu leo linajulikana ndani na nje ya nchi. Tumeendelea kupata maombi mbalimbali. Hivi sasa timu ya cricket Taifa wana mashindano yao ya kimataifa, wameshaleta maombi, tunaomba Tanzania mtu-host. Hii yote ni kutokana na uongozi bora wa Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha kabisa anapenda michezo, lakini siyo tu michezo, hata masuala ya utamaduni na sanaa. Watu wa utamamduni na sanaa tunamtambua kwa jina la Chifu Hangaya. Tuko naye, yuko vizuri. Mheshimiwa Rais ameacha alama maeneo yote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya, sasa naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwanza kwa kuwapongeza sana Waziri, Naibu Waziri wa Wizara hii ya Utumishi, lakini kwanza niendelee pia kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu, mama yetu shupavu, Mama Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jana ametufundisha hapa, ametuelekeza masuala ya nidhamu na uwajibikaji katika kazi. Kwa hiyo, mengi yamezungumzwa kuhusiana na upungufu wa watumishi katika Halmashauri, Wizara naongeza na katika Balozi zetu. Kwa kweli eneo hili tuangalie, wakati mwingine, wakati tuna-solve suala upungufu tuangalie pia namna ya kutumia wanao-volunteer. Zipo idara zinaruhusu volunteers ambazo haziratibu nyaraka ambazo ni confidential, kule wanakoruhusu tuanze hata kutumia volunteers. Kuna wakati wananchi wetu wanakwenda katika ofisi unakuta ni muda wa kazi wakati mwingine maafisa hawapo ofisini. jukumu la utumishi wa umma ni kuhudumia wananchi. Wananchi wanafika katika ofisi zetu, unakuta watu hawapo na wakati mwingine mwananchi anaulizwa, una appointment? Sasa hii appointment niiombee wapi? Sijapewa email, sijapewa form ya kujaza appointment.

Tunaomba watumishi wa umma sekta zote na taasisi tunapoimarisha utumishi wa umma maana yake utawezesha hata uwekezaji. Anapokuja mwekezaji anahitaji ardhi, maji, masuala ya umeme, vibali mbalimbali, tunaposema tunakwenda kwenye uchumi wa kati basi kitu ambacho kinaimarisha ni pamoja na public service. Huduma hizi za Serikali tunaomba sana tubadilike, change of attitude, tunavyofika katika ofisi zetu wananchi wakija wale ndiyo mabosi wetu na sio sisi ambao tuko utumishi ndiyo mabosi. Tuwapokee wananchi vizuri. Ni mbaya sana mwananchi ana shida katika ofisi fulani anauliza, je, kuna mtu unamfahamu? Niepeleke ofisi fulani, no! wananchi wanapoenda katika ofisi za Serikali, wasikilizwe, waelekezwe na waoneshwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa lazima tubadilike unaenda kwenye ofisi unaambiwa mhusika huyo hayupo. Sasa lazima tujue kama mhusika umetoka kwa ruhusa umemuachia nani maana hizi ofisi tumetoa dhamana na tumeahidi wananchi tutawahudumia, leteni kero, msiwe na wasiwasi, sasa tunapokwenda katika hizi ofisi iwe ni halmashauri, iwe ni mikoa, iwe ni wizara, taasisi yaani hapa lazima tubadilike, tuwahudumie wananchi kiasi ambacho kinastahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo naomba pia nilizungumzie, nipongeze sana PCCB., PCCB ina-fall chini ya Wizara hii wamefanya kazi kubwa sana. Wameokoa mabilioni katika uchunguzi, takriban bilioni 96 katika mifumo wameokoa takriban bilioni 11. Bado PCCB tunaomba mtusaidie katika miundo. Ni namna gani miundo hii kwanza tunaweza tukaokoa hizi fedha, lakini pia miundo mingi PCCB washauri iwe transparent. Upande wa TASAF, PCCB wamefuatilia masuala ya kaya na kuhakikisha maeneo yote kwamba hakuna kaya hewa, maana ziko kaya zingine zinaingia katika mfumo wa TASAF yamkini ni hewa.

Kwa hiyo, PCCB wafuatilie, kuhakikisha kwamba fedha tunazopeleka TASAF zinafika kwa walengwa kwa wakati unaostahili. Kwa hiyo, napongeza sana kazi nzuri, lakini bado kibarua cha kuboresha ili maendeleo yaweze kufika kwa wananchi yafanyike kwa ufasaha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni Serikali Mtandao. Serikali Mtandao ni eneo muhimu sana, niombe Serikali Mtandao tuweke taarifa muhimu. Sasa hivi watu wengi kutokana na hii changamoto ya Covid–19 mara nyingi sana wanatafuta taarifa katika mtandao. Kuna taarifa mbalimbali za Wizara mbalimbali; taarifa za masoko, bidhaa ambazo Tanzania tunauza katika Wizara zetu, kwa hiyo, wanapoingia wawekezaji na sisi wenyewe kupata taarifa fulani katika Wizara fulani tunaomba taarifa hizi ziwepo maana ni ngumu sana mwananchi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda Makao Makuu ya Wizara wakati taarifa zingine unaweza ukapata katika mitandao.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kwa kupitia e- government tuzidi kuweka ushirikiano na mahusiano ya Wizara mbalimbali na balozi zetu. Wakati mwingine kunakuwa kuna maswali mbalimbali katika Balozi zetu wanahitaji taarifa. Kwa hiyo, e–government tuone ni namna gani tutaweza kujitahidi kuweka taarifa stahiki zinazopaswa katika mtandao. Isiwe kwamba ah website haijawa updated tangu kipindi fulani. Katika eneo hili tuzidi sana kuboresha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine kama tulivyoambiwa nidhamu na uwajibikaji katika kazi ni suala zima la kupata mafunzo. Wakati umefika sasa watu wanaoajiriwa katika nafasi mbalimbali wapate mafunzo, the do’s and the don’ts, maana sasa hivi wakati mwingine katika ajira zetu unakuta bado taratibu zingine za kuhudumia wananchi watu hawajapata kuzielewa ipasavyo.

Kwa hiyo, Chuo cha Utumishi wa Umma nakipongeza sana na Kamati tulifanya ziara pale ya masuala ya Serikali za Mitaa, imefanya kazi kubwa, nzuri lakini tuendelee kuomba watoe mafunzo kwa taasisi mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo nalo ningependa kulizungumzia ni kuendelea kupongeza ujenzi wa Ikulu ya Dodoma. Ujenzi huu wa Ikulu ya Dodoma ni muhimu sana. Kwa hiyo, ujenzi huu utakapokamilika tuombe sana ujenzi wa Ikulu ya Dodoma uende sambamba na huduma. Maana tunaweza tukajenga vizuri sana, lakini ziwe ni zile huduma zinazopaswa kuwemo mle. Tunaita huduma za first class, hata Mheshimiwa wetu anavyofanya kazi Ikulu afanye kazi akipatiwa huduma za kutosha, stahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba riba ya kodi ya viwanja kwa wale wanao delay iangaliwe, ni kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, kwanza naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iwekeze kwenye uchumi wa bahari yaani uvuvi, usafirishaji wa mizigo baharani, magari, makontena na kadhalika. Cruse tourism, utalii wa bahari, uuzaji wa mapambo ya bahari, uvuvi kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, naonga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maliasili na Utalii
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kupata nafasi hii ya kutoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo. Nianze pia kwa kukushukuru wewe mwenyewe kwa kutuongoza vema, lakini pia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa kuchambua na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti yetu vizuri na ushauri waliotupa kwa kweli tutaendelea kuuzingatia.

Mheshimiwa Spika, tumepata wachangiaji takribani 36 na kati yao waliochangia kwa kuongea ni takribani 26 na pia waliochangia kwa maneno takribani wachangiaji 10.

Mheshimiwa Spika, nami niungane na Waheshimiwa wengine wote na Mheshimiwa Naibu Waziri kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Mheshimiwa Rais ametuonesha dira, ametuonesha njia juu ya suala zima la uhifadhi na masuala mazima ya utalii hususan suala zima la Royal Tour. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli nichukue nafasi hii kumshukuru sana sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kutuongoza vema katika kutukumbusha kwamba masuala haya ya utalii tujue na kutambua kwamba yanachangia pato la Taifa lisilopungua asilimia 17 na tuna maelekezo kwamba ifikapo mwaka 2025 tuendelee kuongeza pato la Taifa hadi kufikia dola za Kimarekani zisizopungua bilioni sita na watalii takribani milioni tano. Hivyo ni jukumu letu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuona ni namna gani eneo hili tunaliboresha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vile vile nishukuru sana kwa michango ya Waheshimiwa Wabunge wote Waheshimiwa Wabunge wamechangia michango mbalimbali na sisi Wizara tuseme tu kwamba michango hiyo tunaichukua tunaifanyia kazi na tutaleta majibu hayo kwa maandishi kwa michango yote tutaleta kwa maandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikienda haraka haraka katika eneo la udhibiti wa wanyama pori wakali na waharibifu nianze kwa kutoa pole kwa changamoto hii kwa wananchi kutokana na adha ya wanyama pori wakali na waharibifu.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo Wizara yangu imeendelea kuchukua hatua za muda mrefu na muda mfupi kukabiliana na changamoto hii. Suala la wanyama hawa limekuwa ni changamoto iwe ni tembo na wanyama wengine na tumelizungumzia sana na kwa kweli tunaafiki kwamba eneo hili tuone namna gani ya kuboresha na tukiboresha ndipo sasa tutaweza kuwalinda wananchi wetu wasipate madhara na maumivu yoyote, lakini pia tukizidi kuboresha tutaona jinsi gani ya kulinda hata hifadhi zetu.

Mheshimiwa Spika, hatua za muda mfupi zinajumuisha kuanzisha ujenzi wa vituo 19 vya kudumu kwa ajili ya askari wa Jeshi ya Uhifadhi na kizimba kimoja kwenye maeneo yafuatayo; Wilaya ya Meatu - Kijiji cha Malwilo kutakuwa na kituo; Rufiji katika Kijiji cha Ngarambe; Busega katika Kijiji cha Kigereshi; Lindi katika Kijiji cha Milola; Tunduru katika Kijiji cha Milonde; Mwanga katika Kijiji cha Kwakoa; Iringa katika Kijiji cha Itunundu; Songwe katika Kijiji cha Udinde; Nzega katika Kijiji cha Ndala; Mvomero katika Kijiji cha Lubungo; Chamwino katika Kijiji cha Ilangali; Mpwapwa kutakuwepo na kituo pale Mtera; Nachingwea tutaweka kituo pale Nditi; Liwale Ng’ungu kutakuwa na kituo; Kondoa katika Kijiji cha Mkungunero; Malinyi kutakuwepo na kituo pale Kwa Kilosa Mpepo na Karatu kutakuwepo na vijiji vya Kambi ya Nyoka, Oldeani na Kambi ya Simba na kujenga kizimba kimoja cha mamba katika Jimbo la Buchosa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vituo hivi 19 vitajengwa kwa bajeti ya mwaka huu 2021/2022 ambapo ndani ya mwezi Juni, 2022 ujenzi utaanza rasmi. Aidha, katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Wizara itajielekeza kujenga vituo vingine hivi ni vya mwanzo kutakuwa na vituo vingine tena 13 kwenye maeneo mengine yenye changamoto. (Makofi)

Vilevile hatua za muda mrefu ambazo zinajumuisha kuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi kwa kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta nazo zitakuwepo kutoa elimu za uhifadhi kwa jamii zinazoathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu; kuendelea kuwadhibiti tembo, mamba, viboko, fisi na wanyamapori wengine ambao ni hatarishi kwa njia tofauti kwa lengo la kumaliza madhara haya; kutumia njia mbadala za kielektroniki kwa mfano kuwafunga wanyama GPS Collar na kuona ni namna gani tunaendelea kudhibiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini hata hivyo niendelee kutoa rai kwa wananchi kuona namna gani tunaweza tukajiepusha na kuvamia maeneo ya hifadhi kwa shughuli za kibinadamu ambayo hupelekea wanyamapori kusababisha migongano baina ya wanyama na binadamu. Kwa hiyo, tuendelee kushukuru sana kwa maoni ambayo tumepata namna ya kuendelea kuboresha maeneo haya ya hifadhi.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni suala zima la Royal Tour na eneo hili ambalo linachangia sana pato la Taifa tumepata ushauri wa aina mbalimbali hapa umetokea ushauri wa jinsi ya kuratibu ziara za mafunzo kwa wakala wa utalii na hilo tutalizingatia na kuendelea kutumia watu maarufu na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza vivutio vyetu. Wizara imeendelea kutumia watu maarufu na Wizara imetumia watu maarufu mfano mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa Mamodou Sakho; msanii maarufu wa filamu ya Nolly Wood kutoka Nigeria Gimy Aik; msanii maafuru wa filamu Will Smith wa Marekani pia amewahi kufika katika hifadhi zetu; mchezaji wa Klabu ya Real Madrid Vallejo Jesús; na mchezaji maarufu wa timu ya PSG Andrea Herrera, hii yote ni mikakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mnamo mwezi wa 10 tutaendelea kuwa na mkutano mkubwa sana pale Arusha hii yote ni katika kutangaza masuala ya utalii, huu ni Mkutano wa 65 wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia utalii duniani Kamisheni ya Afrika utafanyika nchini mwezi Oktoba, 2022 Jijini Arusha na utakuwa na takribani washiriki wasiopungua 500. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii ukiwa na watalii tuseme 1,000 wamelala Tanzania chukua mfano watalii wote hawa 1,000 kila siku asubuhi wanakula mayai mawili maana yake utalii huu unaongeza tija na sekta mbalimbali za uchumi maana yake yule mjasiriamali ambaye anafuga kuku, analima mchicha na mazao mengine ataongeza kipato na ndiyo maana tunasema suala hili la utalii tuone namna gani ya kuendelea kuliimarisha. Lakini pia tunaendelea kushirikiana na ofisi zetu za ubalozi kote duniani kuendelea kutangaza vivutio hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia tumeona kwamba upo umuhimu wa kutumia digitali katika kutangaza utalii, kwa hiyo, tunaimarisha utangazaji wa utalii kupitia vituo maalum vya kidigital cha kutolea taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu idadi ya vitanda kwa mwaka 2021 Wizara ilifanya utambuzi na uhakiki wa huduma za malazi katika mikoa 26 nchini ambapo jumla ya huduma za malazi 10,432 zilipatikana zenye jumla ya vitanda 122,532 na vitanda 132,684. Hata hivyo tunaendelea kuhamasisha wadau mbalimbali waendelee kuwekeza katika huduma za malazi nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu mapitio ya sheria na kanuni; Wizara inafanya mapitio na sheria mbalimbali na kanuni na kuona kama kuna umuhimu wa kufanya maboresho ya tozo zilizopo. Sambamba na hatua hizi Wizara inaendelea kuboresha miundombinu ya utalii nchini ili kuimarisha kufikika kwa vituo vya utalii mbalimbali. Aidha, Wizara inatoa elimu kwa wadau mbalimbali wa utalii ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watalii ambao wanatarajia kuongezeka kutokana na programu hii lazima tuwaandae watu wetu tutoe elimu na vyuo vyetu vya utalii vinaendelea kutoa elimu hiyo.

Mheshimiwa Spika, Wizara pia inaendelea kuimarisha ulinzi na kuendeleza rasilimali wanyamapori, misitu, nyuki na malikale kwa kufanya masuala mbalimbali ikiwa ni kuendeleza, kuimarisha kwa mfano Jeshi la Uhifadhi la Wanyamapori na Misitu na kuongeza vitendea kazi na idadi ya watumishi na kuwajengea uwezo kwenye nyanja mbalimbali. Hivi sasa tumeomba kibali cha kuweka askari 600 ambao askari hawa watasaidia pia kudhibiti wanyama wakali katika maeneo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya nikushukuru sana kwa nafasi hii naomba kutoa hoja. (Makofi)

(Hoja imetolewa Iamuliwe)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 2) wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Awali ya yote naunga mkono hoja. Nampongeza Mwanasheria Mkuu kwa kutuletea Muswada huu. Moja kwa moja naenda kifungu kinachohusu Amendment of the Advocates Act. Kuna neno “Ethics” kwamba Regional Advocates Ethics Committee. Kamati inasema wanaweza wakaliacha neno “Ethics” au wakalitoa neno “Ethics” Kamati itakuwa comfortable.

Mheshimiwa Spika, binafsi neno “Ethics” lina umuhimu wake. Ethics is concerned with what is good for individual and society. Kwa hiyo, hizi Kamati za Mawakili za Mikoa ziitwe Kamati za Maadili na kama ile ya Kitaifa National Advocates Committee haina neno “Maadili” binafsi napendekeza basi na kule tuongeze. Kwa hiyo, tunapotoa neno “Ethics” tunataka kutengeneza nini? We need to have ethics. Ethics is very important to individual, our society and our country. So, naomba ni-submit haya mapendekezo kwamba neno “Ethics” kwenye Regional Advocates Committee; kwa sababu pale tunaunda hiki chombo kuangalia maadili ya hao wanasheria. Lazima akichukua kazi ya mtu awajibike kwa wakati, a-appear na kadhalika na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, neno “Ethics” naunga mkono, kama lilivyoletwa na Serikali katika Muswada, lakini endapo ile Kamati ya Kitaifa haina neno “Ethics”, ili lifanane, basi tuone namna ya pale juu kuweka neno “Ethics”.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine…

SPIKA: Kwa hiyo, isomekeje?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, isomeke “The Regional Advocates Ethics Committee” for (a) pale Kifungu cha 4(1) “there is established in each region, the Regional Advocates Ethics Committee which shall, compose of…” inaelezea.

SPIKA: Kwa hiyo, itakuwa ni Kamati ya ku-deal na ethics only? Au huenda hiyo Kamati ina mambo mengine?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, inakuwa na mambo mengine ambayo yameelezwa kwenye sheria, lakini neno “Ethics” naomba liendelee kuwepo.

SPIKA: Ahsante, endelea.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Eneo lingine ni Kifungu cha 2 ambacho kinasema: “The Regional Advocates Ethics Committee may appoint any public officer.” Itamchagua mtumishi yeyote wa Serikali to be the Secretary of the Regional Advocates Ethics Committee. Kumekuwa na maoni mbalimbali, wengine wanasema badala ya kumchukua labda huyu Afisa wa Serikali, labda itangazwe na kadhalika. Nilikuwa naangalia tuna mikoa mingapi haraka haraka, labda mikoa 26 maana yake nafasi 26 Sekretarieti ya Ajira au Tume ya Mahakama ikatangaze, yamkini inaweza ikachukua muda, tukaambiwa bajeti haitoshi.

Mheshimiwa Spika, binafsi naomba niunge mkono kwamba tuwe na huyu public officer. Tunachoweza kufanya, huyu public officer tuseme awe na qualification zipi? Je, awe ana degree ya sheria au degree yoyote? Kwa hiyo, binafsi nadhani hapa ni vema...

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Tupokee taarifa kutoka wapi?

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Spika, niko huku.

SPIKA: Endelea Mheshimiwa Salome.

T A A R I F A

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa dada yangu Mheshimiwa Dkt. Balozi Pindi kwamba alikuwa anasisitiza suala la kuweka neno “Ethics” lakini kwa sasa hivi inavyosomeka kwenye sheria Kifungu cha (7) kinaongezeka Kifungu cha (4) (A): “there is established in each Region the Regional Advocates Ethics Committee.” Kwa hiyo, Ethics bado ipo. Nampa taarifa hiyo. (Makofi)

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa endelea.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Utazingatia taarifa hiyo.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, sawa. Kwa hiyo, neno “Ethics” kwa kweli kama tulivyoona ni la msingi sana na ni muhimu, ahsante kwa maelezo hayo. Kwa hiyo, pale kwenye eneo la any public officer, naunga mkono awe ni public officer lakini tuongeze tu qualification.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine naungana pia na maoni ya Kamati kuhusiana na cheti cha kifo, kwamba cheti cha kifo endapo umetokea msiba, aruhusiwe kuchukua spouse (mke au mume) au mtoto, lakini vile vile next of kin. Huyu next of kin, huyu ndugu asiruhusiwe tu pale ambapo mke au mtoto hawapo. Ninao mfano, ofisi yangu ya Mbunge Viti Maalum Njombe nimetumika maeneo mengi kama next of kin, wakati mke wa marehemu yupo na pia mtoto wa marehemu yupo. Huyu mke wa marehemu anatokea Kijiji cha Manga wilaya ya Ludewa, ni mama mkulima. Ukimwambia bee, kachukue cheti cha baba, anakwambia, kah, ndibite kweyo? Haelewi. Incapable kutokana na sababu moja au nyingine. Mtoto under 18, lakini wote wapo.

Mheshimiwa Spika, sasa tukisema ni lazima mke akiwa hayupo ndipo next of kin aende au mtoto akiwa hayupo; kuna mazingira, mke yupo lakini incapable. Yaani hata hiyo ofisi inatakiwa moli moli (pole pole). Mtoto yupo under 18 sheria under 18 huwezi kwenda, kwa hiyo, next of kin aruhusiwe pale ambapo hata mke yupo, hata mtoto yupo lakini they are incapable. Kuna mazingira incapable. Wakati mwingine kuna suala la ufahamu wa akili, wapo lakini kidogo inabidi kumwongoza pole pole. Kwa hiyo, kutokana na ushuhuda huu, nimetumika maeneo mengi kadhaa kisheria kwenda kuwachukulia vyeti.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba iwe kwamba “notwithstanding subsection (1) a death certificate “may” (siyo “shall”), may be collected by the surviving spouse or child or next of kin if for any reason the spouse or child is incapable of collecting the certificate.” Wanaweza kuwepo lakini hawana uwezo.

Mheshimiwa Spika, pia ni vizuri kuweka kifungu caveat, endapo ndugu, jamaa na marafiki wa ile familia ya marehemu wana pingamizi ya huyu next of kin wanayo haki ya kwenda kupinga, huyu bwana hapana. Sisi hata kama fulani anasema kamchukulie cheti cha kifo, aah lakini sisi tunachoona bwana, hapana. Kunakuwa na caveat.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, “propose addition of another subsection which defines the right of lodging a caveat to the person who is collecting the dearth certificate.”

Mheshimiwa Spika, ahsante. Najua Ofisi ya AG tuko pamoja. Kifungu cha (30) under Amendment of the Companies Act, naungana na maoni ya Kamati na niwapongeze sana Kamati, Mwenyekiti big up. Pale Na. 5 “notwithstanding subsection (1), a person shall not be eligible to incorporate a company if such person is reported by competent authorities to have been convicted or associated with instances of or related to money laundering”, masuala ya terrorism hawezi kuwa sehemu ya shareholders wa Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Kifungu hiki naungana na Kamati. Wao wamesema tutoe lile neno “associated with instances”, maana mtu anaweza akawa associated kwa namna nyingi. Pia wamesema related; neno “related” pia litolewe. Ila hiki Kifungu ni muhimu.

Mheshimiwa Spika, suala la madawa ya kulevya ni changamoto. Tanzania sasa hivi tuko katika SADC tunashirikiana na nchi mbalimbali Seychelles, wapi kuangalia madawa ya kulevya yanapita kwenye Indian Ocean, lazima tuweke vidhibiti, watu wasije wakafanya madawa ya kulevya, money laundering, baadaye anakuja anafungua Kampuni, anasema anatusaidia, kumbe ana changamoto kama hizo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hiki Kifungu nakiunga mkono kisitoke, lakini tuki-draft tu properly. Naunga mkono kifungu hiki. Juzi juzi hapa tunaona mtu anaua watu na bunduki Selander, ugaidi kwenye mitandao; kwa hiyo, lazima tudhibiti hii mianya.

Mheshimiwa Spika, kifungu kingine ukurasa wa 24 Part (11) “Amendment of National Assembly Act.” Kimekuja Kifungu kinasema “upon the dissolution of Parliament, all powers and functions of the commission shall be vested to the chairman of the commission until new members of the commission are elected or appointed.”

Mheshimiwa Spika, naunga mkono kwa sababu, pale ambapo hatuna Wabunge limevunjwa, maana yake makamishna hawapo. Katika Bunge hili tuna kazi nyingi, utekelezaji wa masuala mengi ambayo yako chini ya Tume. Sasa tukisema tunasubiri Tume, Wabunge waapishwe, hapa tunamwachia Mwenyekiti. Functions and powers to be vested. Bunge ni mhimili. Tuna Mhimili wa Mahakama, Mhimili wa Bunge. Bunge ni mhimili muhimu na kunakuwa na kazi nyingi hata kama makamishna hawapo. Huwa tunavunja Bunge hapa mwezi wa Sita, mpaka watu wakaapishwe, warudi, ziundwe Kamati, wachaguliwe, yamkini inachukua muda kadhaa.

Mheshimiwa Spika, tukiacha kusema hizi functions and powers zisiwe kwa Mwenyekiti, itakuwa ni changamoto. Huu mhimili unakuwa haupo. Wanakuja viongozi wanataka kuonana na Bunge…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Ah, kengele ya pili?

SPIKA: Ndiyo.

MHE. BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA: Hee! Mengine nitawasilisha kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza naunga mkono hoja. Nampongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa kazi kubwa na nzuri ambayo wanafanya sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, moja kwa moja nakwenda kwenye kilimo cha kisasa. Kilimo cha kisasa hatuwezi tukafanya kwa kutumia jembe la mkono. Sisi wengine tumesomeshwa kwa jembe la mkono na sasa siyo sawa kusomesha watoto wetu kwa jembe la mkono, tunahitaji vitendea kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miaka 50 baada ya Uhuru Tanzania lazima tuulizane viwanda vya matrekta viko wapi? Wizara itusaidie, Serikali itusaidie tupate viwanda vya matrekta vya kutosha. Leo hii nina invoice hapa, nilikuwa na-compare trekta moja bila jembe siyo chini ya shilingi milioni 50; trekta aina ya Ford, Valmet na hizi zote zinatoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, ni kweli tumetoa ushuru, lakini haiwezekani mkulima wa Makete, Njombe akanunua trekta kwa shilingi milioni 50 bila jembe na kadhalika. Tunahitaji viwanda vya power tiller vya kutosha. Pia Halmashauri zetu zisaidie kuona katika kila Halmashauri kuwepo na wawekezaji wa masuala haya ya kilimo cha kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana, wakati umefika; kama tulivyosema kwenye Ilani kwamba tunataka kwenda kwenye kilimo chenye tija, kilimo cha kisasa cha kuongeza kipato kwa mkulima, lakini leo hii kwa mkulima imekuwa ndiyo changamoto. Yaani mtu ukimwuliza profession, katika kazi mbalimbali; wewe una taaluma gani? Ukisema mkulima, mtu anageuka pembeni. You see!

Mheshimiwa Spika, kwa kweli lazima kilimo kiwe cha kuvutia, chenye tija. Watoto wanapokwenda kusoma University anaulizwa unataka combination gani? Yaani mtu akichagua agriculture wanamwangalia mara mbili; why not business, why not finance? Agriculture, are you serious? Kwa hiyo, lazima tubadilike kwa kweli kilimo hiki kiwe ni chenye tija. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara ifuatilie takwimu kwa kila Halmashauri kuna matrekta mangapi? Mtashangaa kuna baadhi ya Halmashauri matrekta ya kuongeza tija kwenye kilimo cha kisasa hazipo; ziwe ni mbovu au mpya, hazipo. Hapa tunahitaji Government intervention. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo nimetumwa na wananchi wa Mkoa wa Njombe ni lumbesa katika mahindi na viazi. Unakuta magunia mawili yanashonwa linatafsiriwa ni gunia moja. Eneo hili pia imekuwa ni changamoto ya kutosha.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo limezungumzwa hapa ni suala zima la masoko. Kwa kweli masoko ni changamoto. Naipongeza Wizara, imeshirikisha sana balozi zetu mbalimbali, kwa hiyo, katika balozi zetu tuwape takwimu za kutosha. Hizi balozi zetu, hususan zinazozunguka mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nchi zinazotuzunguka wanahitaji sana bidhaa za mazao; maharage, mbao, viazi, chai, alizeti na kadhalika. Mara nyingi wanauliza, mna tani ngapi ambazo tunaweza tuka-import kutoka Tanzania. Yaani Tanzania inakuwa ina- export.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, takwimu lazima ziwepo na ziwe zinapatikana mara moja. Unakuta hizi takwimu mpaka taarifa itoke ubalozini iende Foreign, ikitoka Foreign iende Kilimo, tena itoke Kilimo irudi Foreign ifike kule; huyu mwekezaji hawezi kusubiri, ataenda Brazil kuchukua mahindi. Kwa hiyo, taarifa hizi za kutafuta masoko ziwepo na tushirikishe taasisi binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna taasisi kama East Africa Grain Council, wao wanachukua takwimu kwamba nafaka ziko wapi; mahindi, maharage, njegere na nani anahitaji? Wanachofanya ni kuwaunganisha kwenye mtandao, you see! Kwa hiyo, lazima sasa tushirikishe sekta binafsi katika suala zima la utafutaji wa masoko na uwekezaji katika kilimo.

Mheshimiwa Spika, tuwe na masoko ya mipakani. Wakati mwingine wakulima wetu wakipeleka mazao nje ya nchi, wanasumbuliwa sana na madalali, hawapati haki zao kwa wakati. Kwa hiyo, tukiwa na masoko haya katika mipaka ya nchi zetu mbalimbali, wanaweza wakapata mazao haya kiurahisi zaidi. Kwa hiyo, nchi mbalimbali ambazo ni nchi jirani haziwezi kuhangaika kusafiri kwenda mpaka mikoa ya kusini; pale pale mpakani anapata anachohitaji.

Mheshimiwa Spika, parachichi ni zao muhimu sana. Mkoa wa Njombe wamenituma, iko changamoto ya madawa ya parachichi, iko changamoto ya cold rooms za kuhifadhia parachichi. Pia hii parachichi inatakiwa iwe certified. Ili mkulima auze nje lazima u-certify zao la parachichi.

Mheshimiwa Spika, zile taasisi zinazo-certify zinatoka nje ya nchi…

T A A R I F A

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Taarifa, Mheshimiwa nimekuona.

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, mzungumzaji anayezungumza, mimi Mbunge mwenzake wa Njombe, pia tumetumwa kwenye suala la pamba, kwa sababu miche ya michikichi inatolewa bure, mbegu za pamba zinatolewa bure na mbegu za mazao mengine tofautitofauti Serikali imekuwa ikitoa bure. Je, ni lini Serikali itaanza kutoa mbegu za parachichi bure?

Mheshimiwa Spika, hii ni taarifa ambayo wamenipa wananchi wa Njombe nije niulize Bungeni. Ahsante. (Kicheko)

SPIKA: Chief Whip, inabidi uandae semina, maana mambo haya ya Wabunge wako. (Kicheko)

Mheshimiwa mchangiaji, endelea.

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naendelea. Hiyo taarifa naikubali kwamba mbegu ya parachichi ni lazima itolewe bure. Kwa hiyo, eneo hili ni muhimu liangaliwe kinagaubaga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Makete kwa kweli tunalima viazi, lakini jembe la mkono linamtoa mkulima. Leo hii ukiangalia mikono yetu sisi wakulima wa Njombe tunatumia jembe la mkono. Wananchi wa Makete, akina mama wa Njombe wamenituma, wanasema haiwezekani tukapata vitendeakazi vya kulima viazi hizi kwa mashine? Miaka 50 baada ya Uhuru, kweli jembe la mkono! Kwa hiyo, tupate vitendeakazi. Kuwe na mashine maalum ya kuweka matuta tuachane na jembe la mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, akina mama, wananchi wa Lupembe kwa kweli wanafanya kazi kubwa sana ya kuzalisha chai, lakini msimu wa kiangazi kutokana na upungufu wa maji, unakuta mazao yanapatikana machache. Kwa hiyo, tunahitaji umwagiliaji katika chai na wakulima walipwe kwa wakati. Kuna wakati viwanda vya chai vinachelewa kuwalipa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kilimo kinakwenda sambamba na miundombinu, barabara. Naungana na Taarifa ya Kamati ya Kilimo, imesema TARURA waongezewe fedha. Sisi pale Njombe pia tuna uwanja wa ndege, kuna wawekezaji wanatoka nchi za jirani wanakwenda Njombe, wanahitaji kusafiri kwa haraka…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, naomba kukumbushia baadhi ya Kata katika Wilaya ya Ludewa ambazo hazina umeme, kama Kata ya Ibumi, vijiji 28 Wilaya ya Ludewa havina umeme. Kata ya Milo, Ibumi, kilondo, Ludende, Lumbila, Mkongobaki na Munford Wilaya ya Ludewa hakuna umeme. Tarafa ya Mangali Ludewa kwa baadhi ya maeneo hakuna umeme.

Mheshimiwa Spika, tunaomba Serikali ilione hili, ituletee umeme Ludewa maeneo yote. Wilaya ya Ludewa Kata ya Lugarawa vijiji 20 havina umeme; na Kata ya Mawengi vijiji vinane havina umeme. Tunaomba umeme.

Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kuwasilisha.
Azimio la Bunge la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nimesimama kwa heshima zote na taadhima kuunga mkono hoja iliyopo mbele yetu ya Kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika. Naunga mkono na ninaomba nianze na historia. Naipongeza sana Serikali, Waziri, Naibu Waziri kwa kutuletea mkataba huu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika historia nakumbuka Mwalimu Nyerere ilikuwa ni ndoto yake kuona Afrika ni moja, masuala ya Pan-Africanism. Hivi sasa chini ya AU tumefanikiwa kufanya masuala mengi, kwa mfano tayari tunalo Bunge la Pan-African, pamoja na Bunge hili Mwalimu alitamani sana Afrika iwe moja. Alikuwa anashirikiana na Mzee Mandela na akina Mzee Mugabe na wengine wote. Kwa kweli eneo hili liligawanyishwa na wakoloni. Wakoloni ndiyo walikuja wakafanya kutugawanyisha ili kututawala, lakini sasa wakati umefika wa kuwa na eneo huru la biashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu Europe wamefanikiwa, European Union, mpaka wamekuwa na fedha inayofanana inaitwa Euro kutumia ndani ya Europe, hawatumii tena pesa za nchi nyingine. Sasa sisi tumefanikiwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ni eneo la kujifunza, wengi wamesema, tulikubaliana kuwa na Common Market, Custom Union, Monetary Union, ultimately tulisema tunakwenda kwenye kitu kinaitwa Political Federation.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo common market hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni eneo zuri la sisi kulielewa vizuri kwa sababu tunapokwenda sasa kwenye eneo huru hapa tunazungumzia masuala ya mahindi, huku ndiko maeneo hasa ya kupeleka mahindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ziko nchi ndani ya Afrika wao kutwa ni kupigana, mara wamefanya mageuzi, mara wanapigana, sisi ni kisiwa cha amani. Kwa hiyo hiyo kwetu sisi tayari ni strength. Na upande ule sasa wana hizo weaknesses ni eneo sasa la kujikita na kuelewa ni namna gani sasa tunatchukua hizo fursa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tuna watu takribani milioni 60 na sasa tunakwenda kwenye soko la takribani bilioni 1.2, mazao tunazalisha ya kutosha, mambo kama mahindi. Sasa lazima tuone kuwalinda wakulima wetu, wazalishaji wetu. Kwa mfano, tunataka tuagize labda mafuta ya alizetu, lazima tujiulize haya yaliyopo mafuta ya kula tumenunua kiasi cha kutosha? Tunaweka threshold kwamba kabla ya kuagiza ngano au mafuta, lazima ya kwetu tuwe tumechukua a hundred percent ndipo sasa tunaweza tukaagiza vitu vya nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimi ninaunga mkono hoja hii kwa asilimia mia, na kwa kweli imekuja wakati muafaka, tuchape kazi. Soko hili la pamoja ni letu na bidhaa za kupeleka kwa kweli tunazo. Sisi ni wazalishaji wazuri sana wa mazao (raw materials), sasa tuone namna gani ya kuongeza thamani ili mwananchi anapoenda hata dukani akiona chai ya Tanzania na chai ya nje, akiona bidhaa nyingine aseme hapana sasa nachukua hii ya Tanzania. Wakati mwafaka sasa wa kulinda, kuangalia kodi zote ambazo siyo za lazima tuziondoshe (non-tariff barriers).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimesimama kwa heshima zote kuunga mkono, ilikuwa ni ndoto ya Mwalimu Nyerere, wacha Afrika tufanye kazi kwa pamoja ndipo sasa tutaweza hata kujadiliana na Mabara mengine. Afrika tukiwa pamoja tutaweza kujadiliana na Marekani, tutaweza kujadiliana na Ulaya na nchi zingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli Waziri nakupongeza sana, Kamati imefanya kazi nzuri sana, ninaunga mkono hoja. Tuombe tu TIC wajitahidi kusaidia kuungana na TIC za maeneo mengine tuone namna ya kuboresha.Naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nianze kuungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu na Watanzania kutoa pole kwa mwenzetu ambaye ametangulia mbele ya haki.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kwa moja nianze kwa kuunga mkono hoja. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, hivi karibuni katuonyesha mfano wa umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika maamuzi ya Mahakama. Mheshimiwa Rais amempandisha cheo Mheshimiwa Jaji aliyetoa hukumu kwa lugha ya Kiswahili. Kwa kweli huu ni mfano wa kuigwa na ni maboresho ambayo ni muhimu sana. Nami najiuliza, ilikuwaje siku za nyuma hili hatukuliona? Kimsingi jambo hili lilipaswa kuja mapema, lakini sasa limekuja wakati muafaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Nina sababu nyingi kwa nini naunga mkono kwamba lazima sasa tutumie lugha ya Kiswahili. Tunapotumia Kiswahili, hiki kifungu cha 84 kama kinavyoeleza katika Muswada huu wa Marekebisho kimesema pale, “The language of the laws of the United Republic of Tanzania shall be Kiswahili.” Napigia mstari neno “shall” and not “may”. Ni muhimu sana tuzungumze Kiswahili. Watanzania takribani milioni 60 lugha yetu ya Taifa ni Kiswahili. Wanawake katika idadi ya watu ni takribani asilimia 51 ya idadi ya watu na vijana ni takribani asilimia 60, wote hawa wanajieleza vizuri sana kwa lugha ya Kiswahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo faida za kutumia Kiswahili. Unapotumia lugha ya Kiswahili, kuna sheria, kwa mfano, tunapoambiwa huruhusiwi kushika nyara za Serikali halafu nyara zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza, masuala ya Government trophy, unaambiwa ngozi ya nguchiro ni nyara za Serikali, hiki na hiki ni kosa la jinai, halafu iko kwa Kiingereza. Hivi hawa wananchi wa kule Njombe, Iringa, Ludewa wanaelewa? Kwa hiyo, hili ni jambo la kupongezwa sana kutumia lugha ya Kiswahili. Hii lugha ya Kiswahili kwanza itapunguza hata uhalifu kwa sababu mtu akisoma anajua kumbe hii ni nyara ya Serikali. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani ni kengele ya msemaji aliyepita ya kwangu bado.

NAIBU SPIKA: Ni ya kwako mwenyewe Mheshimiwa.

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ya kwangu? Naunga mkono hoja. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Viwango vya Afya ya Mimea, Wanyama na Usalama wa Chakula
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Serikali bila kuisahau Kamati kwa kutuletea Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya viwango vya afya ya mimea, usalama wa wanyama na chakula. Tunashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Njombe, hususan wakulima, specific wanawake, natoa shukrani za dhati kwa kutuletea itifaki hii. Wananchi wa Njombe wamekuwa wanasafirisha sana mazao yakiwemo viazi, mahindi, parachichi na mazao mengine mengi kama mbao na kadhalika, kwenda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wananchi wa Njombe na wengine kwa kweli walikuwa wanapata changamoto za aina mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeshuhudia watu wanapeleka mahindi nchi za jirani wakifika kwa wale wanaosaga mahindi millers inaweza ikawa ni maize or wheat wanaambiwa kwamba mzigo wako una sumu kavu. Mtu amekuja na semi-trailer mbili hana mahali pa kula, hana mahali pa kulala, tukisingizia aflatoxin na mzigo unakuwa ushaingia nchi za jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, eneo hili imekuwa ni changamoto ya kutosha, na baadhi ya maeneo kumekuwa na madalali, mara mzigo unapofika nje ya boarder madalali wanakuwa wanawasumbua wakulima wetu kwamba wacha nichukue mzigo nitakutafutia soko, wanakuwa wanakosa pesa zao kwa wakati. Kwa heshima na taadhima niipongeze Serikali kwa kweli kwa kutuletea Itifaki hii, ku-ratify hii protocol kwa sababu sasa itaokoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, na nikienda Ibara ya 2 kwenye malengo ni pamoja na kuhamasisha biashara ya kilimo. Asilimia 60 ya Watanzania tumejikita kwenye kilimo kwa hiyo hii Itifaki iko mahali sahihi kabisa na imekuja wakati muafaka. Kwa hiyo, kupitia Itifaki hii, Ibara ya 2 pale tunaambiwa promote trade in food and agriculture commodities. Niombe sana sasa tuendelee kuwa na masoko ya mipakani, mipaka yetu yote ya Tanzania, nchi zote tunazopakana nazo, wilaya muhimu tuweke haya masoko.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nizidi kupongeza Ibara ya 4(2)(a) kinasema katika masuala ya plant health, harmonize the inspection and certification procedure of plant and plant product. Yaani sasa tunakwenda kulinganisha, kufanya ukaguzi uwe unafanana. Sasa tunapoambiwa na nchi jirani kwamba hapa kuna sumu kuvu (aflatoxin) kwa sababu sasa viwango vinakwenda kulingana, hakuna kudanganyana na kubabaishana kwamba akipima TBS ndio sasa itatambulika certificate yake na Kenya Bureau of Standards (KBS); huku kuna TBS kule kuna KBS.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati mwingine tunachukua mfano kuna kampuni mbalimbali ambao wana counterpart wao…

MHE. NUSRAT S. HENJE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Pindi Chana kuna taarifa.

T A A R I F A

MHE. NUSRAT S. HENJE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpe taarifa mzungumzaji kwamba aflatoxin ni sumu kuvu sio sumu kavu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Pindi Chana unapokea taarifa hiyo?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaendelea na hoja yangu kuhusiana na suala zima la aflatoxin na sipingani na tafsiri kwa hiyo, tunaendelea na hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, aflatoxin ni jambo ambalo linaleta changamoto na mara mizigo inapokwenda tunapoambiwa kwamba kuna aflatoxin au aina nyingine ya chemicals ambayo haifai/sumu inaleta changamoto sana kwa wakulima wetu.

Kwa hiyo, hili ni eneo ambalo Itifaki hii inakwenda kuboresha maana kuna watu wanyalukolo kuna namna yetu ya kutamka na watu wa maeneo mengine kila watu na namna yao, kwa hiyo, bora tutumie kiingereza ili kuweka muafaka. Kwa hiyo, nazungumzia suala zima la aflatoxin.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kuna maeneo ya kubadilishana information. Katika Ibara ya 9 inazungumzia suala zima la sharing of information. Tumekuwa na changamoto nyingi sana kwenye masuala ya kilimo kwa mfano masuala mazima ya nzige namna gani tunakabiliana na changamoto ya nzige.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ambalo naunga mkono ni Ibara ya 11 harmonization of policies, laws and regulations; hili pia ni eneo ambalo muhimu sana tuka harmonize kwa mapema.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 8 inazungumzia boarder post control. Naomba kushauri kwamba katika suala zima la boarder post control sasa tuhakikishe boarder post zote ni one stop boarder post. Baadhi ya maeneo bado hatuna one stop boarder post, kunakuwa na boarder mbili; mtu ana-clear upande wa Tanzania na nchi inayofuata. Lakini tunapokuwa na one stop boarder post kwanza inapunguza kupoteza muda kwa hiyo, muda haupotei na mzigo unakuwa cleared kwa haraka na mara mzigo ukiwa cleared kwa haraka, maana yake ni kwamba time is money anaweza kwenda kuchukua mzigo mwingine kupata kupeleka kule kunakostahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni suala zima la Ibara ya 16 ambayo inatueleza wazi kwamba this protocol shall enter into force upon ratification and deposit of instrument of ratification with the Secretary General by all the partner states. Mara leo baada ya kuridhia na tunaunga mkono wote hapa kuridhia Itifaki hii, niombe sana tusichelewe ku-deposit with the Secretary General wa East Africa Community. Secretary General who shall transmit certified true copies of the Protocol and Instruments of ratification to all the partner states.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naunga mkono na nampongeza sana Waziri kutuletea Kamati naunga mkono na kwa kweli kwa niaba ya Wananchi wa Njombe naunga mkono hoja ya kuridhia Itifaki hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naanza na pongezi kwa Rais wetu, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, kumshukuru sana Waziri na Baraza zima la Mawaziri kwa kutuletea mapendekezo haya ya Mpango na vile vile naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi wa Njombe, kwa kweli wanatoa shukrani nyingi sana kwa mambo mengi makubwa ambayo Serikali hii imekuwa ikiyafanya, hususan suala zima la ununuzi wa mahindi na kuboresha upande wa kilimo. Wananchi hawa pamoja na shukrani hizi, jana na juzi nimekuwa naongea nao wa Makete, Ludewa, Wanging’ombe, Njombe Mjini, Lupembe, Makambako, wanasema Mheshimiwa pamoja na mambo mazuri haya, hivi kwa nini bei ya mbolea ipo juu? Nikawa nawaelezea kwamba mbolea hii inaagizwa kutoka nje. Wakasema bee Mheshimiwa, yaani mpaka leo tangu Uhuru karibia tunakwenda miaka 60 ya Uhuru bado tunaagizaga tu mbolea Nje! Kwa nini tusizalishe wenyewe mbolea?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mjumbe hauawi, nafikisha. Wananchi wanauliza, lini tutazalisha mbolea ya kujitosheleza? Wanasema siyo tu mbolea, zana zote za kilimo; iwe ni majembe, power tiller, iwe ni trekta, wakati umefika sasa Tanzania tuzalishe bidhaa zetu. Maana asilimia 60 tumejikita kwenye kilimo, sasa utaratibu huu wa kuagiza zana za kilimo nje watakuwa wanatupangia bei na tutakuwa tunaendelea kusema bei imekuwa kubwa, bei imekuwa kubwa. wa kweli tuzalishe zana zetu za kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyo viwanda mbalimbali vya mbolea. Tukae nao tuwaambie, mahitaji ni haya, sasa hapa tunasaidiana vipi wazalishe mbolea ya kupandia, mbolea ya kukuzia ya kutosheleza? Kwa hiyo, naomba nilete salamu hizi kutoka Mkoa wa Hunzombe, wanaomba sana hili suala la mbolea tuone jinsi ya kuzalisha na litosheleze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima niendelee kumpongeza sana Rais wetu, Mheshimiwa mama Samia Suluhu Hassan. Upande wa Diplomasia, ziara za Mheshimiwa Rais zimeijengea heshima sana nchi yetu. Mheshimiwa Rais amefanya ziara katika Mkutano ule wa United Nations General Assembly na alihutubia pale Marekani na vile vile Mkutano wa Cop 26. Mikutano hii, imekuwa inazaa matunda mengi sana. Tanzania tunaendelea kuwa kwenye ramani ya Kimataifa, kwa kweli niendelee kushukuru sana, ziara hizi zinasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mapendekezo haya ya Mpango tumeona kwamba baadhi ya Balozi zimeendelea kufunguliwa na last time wakati nachangia niliomba sana tuendelee kufungua Balozi pale Vienna tumefungua, tumefungua pia pale China, Guangzhou na maeneo mengine.

Sasa wakati ni huu wa kuendelea kufungua Balozi. Tuendelee kuwaalika nchi nyingine pia waje wafungue Balozi hapa Tanzania na kutokea Tanzania waendelee kuhudumia nchi za SADC na Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mchuchuma na Liganga kwa kweli ni la kulitia maanani. Wengi wamesema, lakini hivi karibuni tumeanza kupeleka Makaa ya Mawe India. Ninaipongeza sana Serikali kwa kuanza kupeleka Makaa ya Mawe India kupitia Bandari yetu ya Mtwara. Nasi wananchi wa Njombe, Ludewa tunasema na Ludewa Makaa ya Mawe tuone jinsi gani ya kuendelea kuyakuchukua na kuendelea ku-export, na ule mradi uendelee kuwekewa vipaumbele vya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, salamu nyingine kutoka Njombe hususan wanawake, wanashukuru vifo vya vya akina mama wajawazito na watoto vimeendelea kupungua. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Kengele bado eeh!

MWENYEKITI: Malizia dakika moja.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa hiyo, wanaomba Bima kwa wote, wanapiga na magoti. Bima kwa wote itaongeza muda wa maisha, lifespan ya Watanzania. Bima kwa wote itasaidia, tutakuwa tuna afya nzuri, kwa hiyo, tutachapa kazi zaidi. Ofisi yangu pale Njombe nimeanza pilot kuwakatia akina mama Bima. Wanaishukuru sana Serikali, wanashukuru Bunge kwa kupitisha Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe mwenyewe wamekushukuru sana, wanaomba uje kule Njombe ufanye ziara ukiwa kama Spika kuangalia utekelezaji wa sheria mbalimbali zinazotungwa na Bunge. Kwa hiyo, wanaulizia Sheria ya Afya kwa Wote (Universal Health Care) inakuja lini? Kwa hiyo, mpango huu ukizingatia, tutashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2022
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuunga mkono hoja, lakini pia kuwashukuru wachangiaji wote. Tumepata wachangiaji takribani wanne na kimsingi wote wanaungana na marekebisho haya ya Sheria hii ya Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, naomba nichangie sehemu mbili, kwanza kuna Sheria ya Malikale, Sura ya 333. Eneo la pili, ni Sheria ya Makumbusho ya Taifa, Sura 281. Nashukuru sana maoni ya Kamati wanaunga mkono marekebisho haya. Reform kubwa ambazo tunakuja nazo Wizara ya Maliasili na Utalii ni madhumuni ya kusajili makumbusho. Tunasema sasa hivi kuna madhumuni ya kusajili makumbusho ambazo zinaanzishwa na taasisi, asasi au watu binafsi. Huko nyuma makumbusho zetu nyingi zilikuwa ni za umma, ni za kitaifa, Makumbusho ya Taifa, lakini sasa tunakwenda na reform, tunasema tunaweza kuwa na makumbusho za taasisi na lazima zisajiliwe, lakini pia tunaweza kuwa na makumbusho za asasi mbalimbali lakini pia watu binafsi. Kwa hiyo hata mimi mwenyewe naweza nikaanzisha makumbusho ya Pindi Chana. Watu binafsi ruksa, kazi ulizofanya taasisi kwa maslahi ya kuelimisha umma, kwa maslahi ya mafunzo na tafiti.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo haya ni mazao mapya ya utalii na hususan baada ya uzinduzi wa ile program ya Tanzania, The Royal Tour. Huko tunakoenda lazima tuongeze watalii tumesema ifikapo takribani 2025, tupate watalii milioni tatu sasa lazima tuje na mazao mapya. Kwa hiyo sasa Watanzania milango iko wazi tunajua tuna Watanzania milioni 61 ruksa kuanzisha makumbusho za Taasisi, za Asasi na za watu binafsi lakini lazima zisajiliwe. Katika kusajili tulisema kwamba endapo mtu hajasajili itakuwa ni kosa na kama hajasajili ikiwa ni kosa atatozwa faini au kifungo. Tunashukuru maoni ya Kamati wametuambia kwamba badili ya kutoza faini ni 5,000,000 hadi 20,000,000 tupunguze iwe ni 1,000,000 hadi 5,000,000 na katika Kamati tumelijadili tukiwa na Mwanasheria Mkuu na hili tumeafiki Serikali tumekuja na marekebisho.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni kuhusu kifungo kwamba eneo hili pia tuanzie mtu akienda kinyume adhabu yake iwe ni kifungo cha miezi mitatu hadi mwaka mmoja na tumelichambua vizuri tunaafiki. Kwa hiyo tunakubaliana na Kamati na wadau waliochangia hapa .

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni kuhusiana na Bodi. Kwenye Kamati tulijadiliana vizuri kwamba kutakuwa na bodi ambayo itateuliwa na Waziri mwenye dhamana. Bodi ya kuteua Wajumbe wa Bodi ya Makumbusho na tumeshauriwa vizuri kabisa kwamba ni vizuri wakati wa kuteua tuzingatie gender. Ukweli ni kwamba wakati wa uteuzi suala hili la kuzingatia gender ni moja ya kigezo muhimu, lakini Kamati ikashauri pamoja na kwamba tunatekeleza lakini kiandikwe bayana na sisi hatujaona changamoto ya kukiandika bayana. Kwa hiyo tunakubaliana na maoni ya Kamati kwamba wakati wa kuteua gender izingatiwe na hasa tukizingatia idadi ya watu ni milioni 61 na 51% ni wanawake.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge na Mkutano wa Nne wa Bunge pamoja na Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nianze kwa kupongeza Kamati kwa uchambuzi wa taarifa yao ambayo imesomwa hapa leo. Pia nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana kwa kazi nzuri ya kusimamia masuala haya ya sheria ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kabla ya kuchangia nilikuwa naongea na wananchi wangu, nikawaambia kule Njombe nakwenda kuchangia masuala ya by-laws. Sasa wakaniuliza sisi watu wa Makambako, Makete, Njombe, Ludewa, Lupemba hizo by-laws, yaani unaposema kwamba zinapaswa kuwa gazetted, hizo Government Gazettes tunazipata wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nikiwa kama mwakilishi wa wananchi naomba nililete swali hili; wananchi wa kule Ludewa na maeneo mengine, hizi Government Gazettes wakitaka kuziona, ku-access wanazipataje? Maana zinatolewa kwa Government Printers, labda zinapelekwa halmashauri; je, kule ngazi ya chini, siku hizi tumeshasomesha, Bodi ya Mikopo inatoa watoto wengi, wasomi wengi, sasa wakitaka kuziona wanazipataje? Kwa hiyo nitashukuru nikipata maelekezo, wananchi wakitaka kuzisoma zinapatikanaje kwenye ngazi ya chini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli napongeza sana hizi sheria ndogo, zina faida sana; kudhibiti magonjwa mbalimbali, mambo ya kipindipindu, kutotupa taka ovyo, ukataji miti; kwa hiyo hizi sheria ndogo zina manufaa makubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo ambalo naomba kusisitiza tu ni suala zima la ushirikishwaji wa wananchi. Tunapowashirikisha wananchi, kwa mfano, tunasema tusikate miti ovyo, kutakuwa na jangwa; tusitupe taka ovyo, kutakuwa na kipindupindu, kwanza tuwape uelewa, tukishawapa uelewa ile awareness creation wao wenyewe watatusaidia kuelimisha jamii na watoto na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusipowapa uelewa, ukamwambia mwananchi usikate miti, atakuuliza sasa nitapata wapi kuni za kupikia na huku vijijini; Ludewa, Makete, tunatumia kuni? Bado masuala mengine ya umeme na gesi baadhi ya vijiji hatujaboresha kupata gesi na umeme kwa sasa, viko kwenye mpango. Kwa hiyo ni muhimu sana kutoa elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yale makatazo yote, by-laws zinazohusu kuacha kutupa taka ovyo, lazima tumwambie mwananchi usitupe taka, dampo hili hapa, au ukitaka kutupa taka dustbin hili hapa, lakini tukiwa tunasema tu labda usitupe taka, lakini hatuwaoneshi mbadala; usikate miti lakini hatumwoneshi kuni atachukua wapi; hayo ni maeneo ambayo ninaomba tuone namna ya kuboresha.

Kwa hiyo ushirikishwaji una faida na wao wenyewe wataendelea kuhubiri hiyo Injili kwa jamii, kwamba hapana, ni marufuku kutupa taka, ni marufuku kukata miti na maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni kuhusu suala zima la kupishana ambalo Kamati imeelezea vizuri, wakati mwingine sheria ndogo inapishana na ile sheria mama. Unakuta wakati mwingine sheria mama labda inasema faini isizidi laki moja na kifungo labda cha miezi sita, lakini sheria ndogo inaweza ikasema faini isizidi laki moja na nusu, kumbe sheria kubwa yenyewe inasema faini isizidi laki moja na ile ndogo imekwenda zaidi. Kwa hiyo hilo ni eneo ambalo ni muhimu tukaliangalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kupongeza maeneo yote wanakotunga sheria ndogo, Serikali za Mitaa (Local Government) wanafanya vizuri sana na kwa kweli sheria hizi zina manufaa sana kwa wananchi wetu. Kwa sababu inategemea na culture ya hilo eneo, inategemea na jiografia ya hilo eneo. Kwa hiyo zile sheria ndogo zinasaidia kuratibu eneo hilo husika kutokana na jinsi wananchi wanavyoishi katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni kuhusiana na suala zima la muda. Wakati tunapitisha hizo sheria, kwa kawaida, tuchukulie mfano za halmashauri zinapaswa kwenda mkoani na baada ya mkoani kwa kweli zinaenda ngazi ya Taifa. Kwa hiyo, wakati mwingine zikifika pale mkoani ninaweka ombi tu kwamba zisikawie, ule uchambuzi na kupitishwa. Kwa sababu zinapochelewa unakuta sasa utekelezaji wa hiyo sheria pia unaweza ukacheleweshwa. Kwa hiyo, niombe sana, zinapotoka halmashauri zinapokwenda mkoani, zisicheleweshwe, zikienda TAMISEMI pia zisicheleweshwe, zipate kurudi kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nichangie maeneo hayo ambayo nimeya-table na nitashukuru kupata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niunge mkono hoja. Ahsante. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli zake kwa Mwaka 2021
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa nami ni mara yangu ya kwanza kuongea kwa kuchangia katika Bunge hili kwa leo, naomba nianze kwa kumshukuru sana Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa imani kubwa aliyonipa mimi na Naibu Waziri Mheshimiwa Ummy Nderiananga. Tunamuahidi hatutamwangusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi huu, kwa mara nyingine tena niendelee kumpongeza sana Spika wetu, Mheshimiwa Tulia Ackson, kwa kupita kwa kishindo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesimama kuunga mkono hoja zote mbili ambazo zimewasilishwa kutoka Kamati ya Katiba na Sheria na Kamati ya USEMI. Naunga mkono mambo yote yaliyoandikwa na yaliyochangiwa kwa mdomo. Masuala yote ni ya msingi na niwahakikishie kwamba tutayachukua na kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya utangulizi wangu huu, ninaomba nizungumze point mbili kwa haraka sana. Kamati ya Katiba na Sheria imezungumzia juu ya suala zima la Sheria ya Maafa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nizungumze pointi mbili kwa haraka sana, Kamati ya Katiba na Sheria imezungumzia juu ya suala zima sheria ya maafa. Tunayo sheria ya maafa sheria hii ya maafa tulikuwa nayo mwaka 1990 ilikuwa ni Sheria Na. 9 na tukafanya maboresho makubwa sana mwaka 2015 Sheria Na. 7 ya maafa na kamati imesema tuendelee kuiboresha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Bunge lako hili la sasa session hii tutaisoma sheria hii kwa mara ya kwanza inakuja na maboresho makubwa sana sheria ya maafa. Kwa hiyo, nakubaliana kabisa na kamati juu ya maboresho katika sheria ya maafa na maboresho ambayo kamati wamesema kwanza wamesema ni muhimu kuwa na mfuko maalum wa maafa. Mfuko huu utaweka utaratibu wa namna gani ya kuchangia fedha za maafa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Waheshimiwa Wabunge wamezungumza umuhimu wa kuwa na Waheshimiwa Wabunge ndani ya kamati za maafa. Muundo wa kamati tutakuwa na kamati za maafa ngazi ya Taifa, ngazi ya mikoa, wilaya kata hadi ngazi za vijiji kuona ni namna gani tunaratibu suala zima la maafa. Maana maafa yanatugusa sisi wenyewe ni jambo ambalo linatokea katika jamii zetu. Kwa hiyo, tutakuwa na hizi kamati, kwa hiyo Wabunge watakuwa ni sehemu ya hizi kamati za maafa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ni muhimu sana kamati wamezungumzia kuhusu elimu juu ya maafa. Nikuhakikishie kwamba sasa hivi katika mitaala ya shule zetu za Msingi, za Sekondari wanatoa elimu juu ya maafa kuna masomo mbalimbali pale katika shule zetu ni namna gani kujilinda na maafa kwa mfano janga la njaa tunafanyaje udhibiti wa mafuriko tunafanyaje kutokata miti namna gani ya kudhibiti namna gani ya kukabiliana na suala zima la maafa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili suala la elimu ni jambo la msingi sana, hadi Vyuo Vikuu kuna taaluma za degree zinazohusiana na masuala ya maafa masuala ya disaster management, kwa hiyo, sasa hivi tumepiga hatua suala hili la maafa linapewa kipaumbele cha hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo kamati pia imezungumza ni suala zima la utekelezaji wa mapendekezo ya kamati. Kamati mara nyingi inatoa maelekezo mbalimbali mapendekezo kwa hiyo, zinatoa kwa niaba ya Bunge na sasa kamati imeshauri kwamba Serikali kupitia Wizara na Taasisi zake kuendelea kupokea na kutekeleza ushauri na mapendekezo mbalimbali ya kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri huu upo katika ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo nanukuu “kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwamba Bunge ndicho chombo cha kuishauri”. Sasa kwa kuwa kamati hii ya Katiba na Sheria inasimamia pia masuala ya sera, uratibu na Bunge imeshauri kwamba tuone ni namna gani mapendekezo haya yanazingatiwa. Suala hili pia ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli amekuwa akituelekeza kwamba ushauri unaotolewa na Bunge Serikali lazima tuuzingatie. Utakumbuka bajeti iliyopita kuna ushauri wa aina nyingi sana ulitolewa na Bunge na ushauri ule wote kwa kweli ulikuwa umezingatiwa na Serikali. Kwa hiyo, suala la Bunge kuishauri Serikali katika taasisi na Wizara ni jambo la kikatiba ni jambo la msingi lakini pia siyo tu kutekeleza ule ushauri, baada ya utekelezaji wa ule ushauri pia Serikali tunakuja kutoa majibu ni namna gani imetekelezwa, na ndiyo maana katika kupitisha bajeti kila tunapoenda kwenye kamati tunasema utekelezaji wa maagizo ya kamati unawekwa pale na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili ni jukumu la kikatiba na kwa kweli tunashukuru na tunaunga mkono suala hili na ni suala ambalo lipo tumekuwa tukifanya hivyo mara kwa mara lakini kamati imefanya vizuri sana kukumbusha kwamba tunaomba tuendelee suala hili kulizingatia na kama nilivyosema kwa kweli ni maelekezo ya Rais wetu mpendwa kwamba suala hili ni lazima tupate kulizingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya maoni yote ambayo yametolewa na kamati zote mbili tunakwenda kuzingatia na vile vile tunakwenda kufanyia kazi na kama tulivyosema kwenye ibara hii ya 63 na majibu yanakwenda kuwasilishwa kwenye muhimili huu wa Bunge naomba kuunga mkono hoja nasema ahsante sana. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi ya Mwaka 2004
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesimama hapa kwanza kuunga mkono Itifaki hii ya Mkataba wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi ya mwaka 2004.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maliasili na Utalii ni mdau mkubwa sana katika masuala haya. Ninampongeza sana kaka yangu Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri lakini pia niishukuru Serikali kwa kutuletea Itifaki hii. Itifaki hii haijachelewa imekuja wakati muafaka, kwa kawaida kabla ya kuridhia huwa tunakuwa na mambo mengi sana ya kuangalia na kujiridhisha kwa hiyo, niseme tu kwamba imekuja muda muafaka na muda muafaka ni sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tumepata watalii wengi sana, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Amiri Jeshi Mkuu kwa kutuongoza vyema na amani ndani ya nchi hadi sasa tunapata watalii wengi. Nimekuwa nikisema kwamba watalii hawa wanakuja Tanzania siyo tu kwa kuwa tupo kwenye ramani ya dunia lakini kabla ya watalii kufika wanaangalia vigezo vingi. Kuna suala la uongozi bora, siasa safi na political stability ni miongoni mwa vigezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo nchi zingetamani sana kupata watalii lakini watalii kabla ya kwenda wakiona nchi labda ina vita, ina machafuko wanasema huko hatuwezi kuenda. Sisi tumeingia kwenye rekodi ya dunia kama kisiwa cha amani, tuko kama kisiwa cha amani kutokana na uongozi bora wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ndiyo maana hivi leo unakuta watalii wanaingia kupitia mipaka yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Iwe ni mipaka ya nchi kavu wengine wanatumia njia mbalimbali za ndege na kadhalika lakini tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais pamoja na uzinduzi wa ile program ya Tanzania (The Royal Tour) na sasa tutakwenda awamu ya pili ya uzinduzi wa (The Hidden Tanzania) tunamshukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Itifaki hii yako maeneo ya kubadilishana taarifa, yako maeneo ya mashirikiano imeeleza vizuri sana Itifaki hii. Inasema kwamba we are determined to ensure Africa active participation, corporation and coordination with the international community in its determine efforts, combat and to eradicate masuala ya ugaidi. Haya ni masuala muhimu sana na niombe Bunge hili turidhie kwa kauli moja kwamba, Itifaki hii ya kupambana na kuzuia ugaidi ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepewa dhamana pia ya kulinda na kuendeleza misitu, lazima tuwahakikishie Watanzania wasiopungua takribani Milioni 55 tunasubiri takwimu za sensa, kwamba misitu yetu iko salama. Katika Itifaki hii imesema tutaendelea kubadilishana taarifa. Iko misitu ambayo inafanana na kushirikiana katika nchi zetu za SADC. Kwa mfano kuna misitu inaitwa Miombo hii ni misitu ambayo iko maeneo yetu ya Nyanda za Juu Kusini na inakwenda hadi nchi za SADC. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako maeneo mengi sana ya misitu tunapakana na nchi mbalimbali, hasa misitu hii kama jinsi ambavyo misitu yetu ndani ya Jamhuri ya Muungano iko salama ni lazima tubadilishane taarifa, kwamba hii misitu ya nchi jirani na kwenyewe kuko salama au kuna changamoto? Kwa hiyo, Itifaki hii inapokuja itatusaidia kutoa mashirikiano kati ya nchi zetu, nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, nchi za SADC kuona kwamba maeneo yetu ya maliasili na utalii yapo salama. Kwa hiyo, Itifaki hii ni muhimu, kupitia Itifaki hii itatusaidia kwanza kukabiliana na masuala ya ugaidi, kukabiliana na masuala yote ya machafuko lakini kikubwa kama nilivyosema hapo awali ni suala zima la kubadilishana uzoefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ugaidi kwa kawaida unakuwa ni planned and organized, sasa tukiweza nchi za Afrika kuja pamoja kuelimishana, kukumbushana namna bora ya kudhibiti masuala haya ya ugaidi itatusaidia sana. Kwa hiyo, nimesimama hapa kuunga mkono hoja hii, kuunga mkono Itifaki hii na niombe kwamba Itifaki hii imekuja wakati muafaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa utalii unachangia takribani asilimia 17 ya Pato la Taifa. Utalii unatoa ajira takribani milioni 1.5 na fedha za nje takribani asilimia 25, nusu ya eneo letu la Jamhuri ya Muungano ni misitu. Maeneo haya ya misitu mazingira ya utalii, lazima tuwahakikishie umma na Jumuiya ya Kimataifa kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo salama karibuni katika masuala yote ya utalii. Iwe ni utalii katika fukwe, utalii katika hifadhi mbalimbali katika mapori yetu na Ikolojia zote kwamba Tanzania tuko salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha jambo hilo hivi sasa tumekuwa na mikutano mingi sana na haya ni mazao mapya ya utalii, mwezi wa Oktoba tutakuwa na mkutano wa United Nations World Tourism Organization, huu ni mkutano ambao utaleta wadau wasiopungua 600. Miongoni mwa checklist ambazo wanakuwa nazo ni kujiridhisha kwamba huko tunakokwenda wako salama? Kwa hiyo, kwanza wameshajiridhisha tuko salama lakini Itifaki hii itakuwa ni moja ya silaha ya vitendea kazi ambavyo tutaweza kulinda na kuendeleza usalama wetu ambao tunao. Kwanza, kwa kuwaelekeza nchi nyingine ni namna gani unaweza kufanya kudhibiti masuala haya ya uhalifu na wao wawe salama kama Tanzania tukitambulika kama ni kisiwa cha amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Tanzania tumekuwa mfano wakati wa kupigania uhuru katika nchi za Kusini mwa Afrika, kupitia Baba wa Taifa Mheshimiwa Nyerere alikuwa akitoa maelekezo kwa nchi zote za Kusini na hapa tulikuwa tunaweka makambi ya usalama. Kwa hiyo, suala hili la ugaidi kukabiliana nalo tumekuwa tukilidhibiti tangu wakati wa uhuru Tanzania imekuwa ni sample ndani ya Afrika, Tanzania imekuwa ni mfano bora. Kwa hiyo, leo tunapopitisha Itifaki hii ni wakati muafaka na ninaomba nichukue nafasi hii kwa kweli kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja hii. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa Bungeni kwenye Mkutano wa Kumi na Mkutano wa Kumi na Moja pamoja na Uchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Sheria Ndogo zilizowasilishwa Bungeni kwenye Mkutano wa Nane na Mkutano wa Tisa
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata nafasi hii. Nianze kwa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani ambayo ameendelea kunipa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Nashukuru sana. (Makofi)

Mheshimwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Naungana kabisa na maoni mazuri ya Kamati ambayo yametolewa na sisi tumeyapokea na tunaendelea kuyafanyia kazi. Nitumie nafasi hii kusema kwamba majukumu ya Bunge kwa mujibu wa Katiba yetu Ibara ya 62, 63 na 64 ni pamoja na kuisimamia Serikali, kupitisha bajeti na kutunga sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaposema kutunga sheria ni majukumu ya Bunge, ndani yake ni pamoja na kurekebisha sheria mbalimbali. Hivyo, sheria zinavyopita hapa kuja kutungwa, kurekebishwa ndiyo majukumu ya msingi ya Bunge letu. Nalishukuru sana Bunge letu kuwa na Kamati maalumu ya Sheria Ndogo. Kamati hii maalum ya Sheria Ndogo ni muhimu sana, inatupa maoni mengi mazuri ya kuboresha ya sheria mbalimbali. Kwa hiyo, nilitaka tu kwanza tukumbushane kwamba suala la kutunga sheria ni na kurekebisha sheria ni majukumu ya msingi hivyo. Hivyo, sheria imnaweza ikaja hapa kufuta sheria ya nyuma, kurekebisha, kuongeza na kuboresha. Ndiyo majukumu ya msingi kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepokea maoni mbalimbali na hivi sasa tunakwenda kuboresha Sheria ya Tume yetu ya Kurekebisha Sheria. Tunakwenda kurekebisha sheria hii, tunataka sheria zote za Bunge zinazotungwa, kabla ya kutungwa tupitishe Tume ya Kurekebisha Sheria (Law Reform Commission). Lengo la kupitisha, ni kwamba zifanyiwe tafiti kuona kama sheria hii inafaa, ipo kwa muda muafaka na kama itasaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni haya yanatokana na Kamati zetu ikiwa ni pamoja na Kamati ya Sheria Ndogo. Tunaposema tuziangalie hizi sheria vizuri, kwa hiyo, tunakuja na maboresho, na huu ni mwanzo. Maoni mengi mazuri yametolewa, tutaendelea kuboresha. Kwa hiyo, lazima sheria iendane na Katiba, lazima tufanye tafiti. Tumesema sasa sheria hizi wakati wa marekebisho lazima zipitiwe na tume yetu ya kurekebisha sheria, kufanya uchambuzi na tafiti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama hapa kuunga mkono hoja na kuendelea kukumbushana kwamba jukumu la Bunge ni kutunga sheria na kurekebisha. Pia tuzazo halmashauri zetu ambao pia wanalo jukumu la kutunga sheria ndogo kutokana na eneo lenyewe. Kama eneo lina changamoto ya kipindupindu basi watu wasitupe taka hovyo. Kama kuna changamoto ya masuala mbalimbali, nakumbuka wakati wa Covid nchi nyingine walisema lock down lakini sisi tulisema tunafanya kazi. Kwa hiyo, badala ya lock down wengine wanasema basi kutembea iwe mwisho saa fulani ili kudhibiti masuala ya magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Covid.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja na kuipongeza sana Kamati ya Sheria Ndogo ambayo inafanya kazi nzuri na maoni mliyotoa tutayachukua na kwenda kuyafanyia kazi tukianza na marekebisho ya Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria. Zitapitiwa, zitafanyiwa uchambuzi, zikija huku zinaendelea kuwa vizuri na zitapita katika Kamati zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO. 4) ACT, 2021
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nianze kwa kuipongeza Serikali na Mwanasheria Mkuu kwa kutuletea haya maboresho ambayo ni muhimu sana. Moja kwa moja naenda kwenye Ibara 10, 15A pale inaelezea kuhusu Waheshimiwa Majaji Wastaafu kwamba watakuwa wanalipwa kupitia Mhimili wa Mahakama; na pale tumesema Chief Court Administrator. Naunga mkono hiyo na napendekeza, kwa kuwa hapo tumesema Chief Court Administrator, Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

Mheshimiwa Spika, vile vile ukurasa wa 17 pale amendment of political service retirement benefits ambapo inazungumzia retired Speaker or retired Deputy Speaker and their representative spouses, their entitlement shall be paid through the Office of the National Assembly. Napendekeza neno “Office the Clerk of the National Assembly.” Kwa sababu huku tumesema Chief Court Administrator, so napendekeza iwe “the Clerk…”

SPIKA: Ni ngapi Doctor?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 17 kwenye Muswada wa Serikali, Kifungu cha 49.

SPIKA: Ndiyo.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: mbili pale!

SPIKA: Hebu anza tena.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Ehee! Sentensi ya last but one inasema, “Retired Speaker or Retired Deputy Speaker and their respective spouses are entitled; Eh, imeandikwa “are entitled” sijui kama grammar ni sawa, lakini nasoma kama kilivyoandikwa, nadhani ni their entitlement shall be paid through the Office of the National Assembly. Mimi napendekeza iwe “the Clerk of National Assembly.”

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Sababu?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, sababu hapa kwenye Chief Court Administrator hawajasema through the Office of Chief Court Administration, wameshema Chief Court Administrator. Kwa hiyo, huku napendekeza iwe Clerk of the National Assembly, lakini naona wataalam watatufafanulia.

SPIKA: Umeeleweka, endelea tu.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Atatufafanulia Mwanasheria Mkuu.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Eneo lingine kwa haraka sana, ni kuhusu ukurasa wa 8 Ibara ya 17, inasema, “the principal Act is amended in section 6 ina-delete hiyo and substituting for it the following: inaweka wale wadau wa kuingia kwenye hicho chombo, one representative from the Ministry, one representative from Ministry responsible for Regional Administration.”

Mheshimiwa Spika, sasa hawa watu ambao huwa wanaingia kwa Mujibu wa nafasi zao, unakuta hapa kuna Wajumbe takribani nane; kwa kuwa wanaingia kwa mujibu wa nafasi zao kwamba mtu mmoja atatoka BRELA, mtu mmoja atatoka Authority responsible for medical device, mwisho wa siku wanajikuta wote ni Me. Kwa hiyo, naomba wakati hawa watu wanakwenda kuchukuliwa, tuzingatie gender, Me na Ke. Tukiacha hivi hivi, unakuta Bodi fulani wote ni Me. Ukiuliza mbona Bodi hii wote ni Me? Wanasema tumeingia kwa mujibu wa nafasi zetu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. Kwa hiyo, wataalam tuongeze labla kifungu kinachosema gender should be considered. Mtaweka grammar vizuri.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ukurasa wa 9, Kifungu cha 23 amendment of the Mining Act. Kifungu cha 23 kinatafsiri pale gross value means the market value of mineral or mineral at the point of refining or sale in case of consumption within Tanzania.” Sasa mineral, kuna diamond, gold, gemstone na kadhalika. Nilitaka kujua tu sisi watu tunaotoka Mchuchuma na Liganga, Makaa ya Mawe humu yamo au kwenye hii tafsiri haimo, nayo yamekuwa treated humu Pamoja? Ni ili kupata kufahamu.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine, kwa haraka sana ukurasa wa 13, Kifungu Na. 23(b) pale kinaelezea kuhusu general penalty. “A person who commits an offence under this Act, in respect of which no penalty has been specifically provided, shall be reliable on conviction to fine not exceeding three million.” Haitazidi shilingi milioni tatu, lakini hawajaweka minimum.

SPIKA: Fungu lipi?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 13, Section 34.

SPIKA: Endelea.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 23(b), pale wameweka tu kwamba faini kiwango cha juu ni shilingi milioni tatu (three million) au Kifungo; imprisonment for not exceeding three months or both, lakini minimum penalty haipo. Kwa hiyo, nashauri tuweke na minimum penalty. Kama maximum ni three million, minimum ni ngapi? Shilingi elfu hamisini, laki moja au milioni moja. Nashukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, ukurasa wa 14, tumerekebisha National Health Insurance Fund. Huko nyuma mtoto alikuwa anatafsiriwa mwisho miaka 18.

Mheshimiwa Spika, tuna Wabunge wengi,

SPIKA: Ukurasa wa…?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 14.

SPIKA: Kifungu…

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, kifungu 36.

SPIKA: Mh!

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, “amendment of the National Health Insurance.”

SPIKA: Mh!

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: pale 37 imetoa tafsiri ya mtoto sasa haitaishia miaka 18, inaenda miaka 21. Natoa shukurani kwa Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Samia kwa sababu watoto wetu wengi wakiwa na umri wa miaka 18, 19 bado wako chini ya uangalizi wa mzazi, wapo shule. Sasa unaenda kusema insurance ya mtoto, unaambiwa aah, huyo mwisho ni miaka 18. Miaka 21 bado yuko Chuo, bado yupo University ananitegemea, unaambiwa hamna Bima.

Kwa hiyo, Serikali imejirekebisha, Bima sasa itamtambua mtoto hadi miaka 21. Katika hili, napongeza sana. Naomba maelekezo wakati Mwanasheria Mkuu ana wind-up hapo: Je, ni kuanzia lini? (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa makofi hayatoshi hayo jamani. (Makofi)

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, tunamshukuru sana Mheshimiwa Mama Samia, kwa kuliona hili. Serikali ya Awamu hii hadi Wafanyakazi Serikalini, wafanyakazi katika Taasisi, watoto wao chini ya miaka 21 watakuwa wanapata Bima. Shukurani nyingi sana. Kama tunavyotambua, asilimia 50 ya idadi ya watu bado ni watoto.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tungependa maelekezo yako, sisi kuanzia lini twende pale National Health Insurance tulete Watoto wetu? Kuanzia kesho ruksa au mpaka isainiwe au nini? Hiyo ni ya kwako Spika. Wabunge na Watendaji kuanzia lini tuanze kupeleka zile Birth Certificate za watoto tupate zile Bima? Maana wengi tunao miaka 20 na 21 hapa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana wewe, naishukuru sana Kamati, imefanya kazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
MUswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wa mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru sana nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kutuletea maboresho haya na Serikali, haya ni maboresho muhimu sana na nipongeze Kamati kwa maoni yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kwa moja ukurasa wa sita kifungu cha 6(1) actually ni kifungu cha 5(1) kwa mujibu wa muswada; the principal Act is amended by repealing section 6; pale section 6 inasema kwamba; the Minister shall appoint the Executive Director of the Board on such terms and conditions as he may determine. Napendekeza badala ya neno as he may determine tuweke as per public service guidelines.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine kifungu cha 6(2)(d) inasema kwamba wale watu watakaochaguliwa pale kwenye (d) has at least ten years work experience out of which, eight years being in managerial position. My question is has at least ten years work experience; which experience? I think it should experience on the relevant field, kwa sababu mwingine anaweza akawa ten years experience but experience ya lawyer and not as accountant, so kama wataalamu wa uandishi wanaweza wakaangalia at least ten years work experience may be on the relevant field, isiwe open.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine sana sana napongeza kwenye sanction na penalty ndiyo nita-focus sana, naenda ukurasa wa 10 wa muswada ambapo ukurasa wa 10; oh my God, kuna page nyingine haijatoka page nine, ukurasa wa 10 hapa kifungu cha 11 cha muswada ambacho kina kinazungumzia establishment of accounts and auditors; section 24 kwamba; there is hereby established an appeals board to be known as Accountants and Auditors Appeal Board which shall consist of; pale kwenye (b) yake kuna (i), (ii), wameelezea a lawyer, a law officer, one senior member from Ministry responsible for finance, one senior member from Bank of Tanzania and one senior member from TRA.

Mheshimiwa Naibu Spika, napendekeza hapa baada ya (b)(v) kuwepo immediately adding (vi) ambayo itasema hivi; “The Minister shall have regard to the gender balance,” kwa sababu hawa wanaoingia by virtual of their post sometimes wote wanaweza wakawa “me” au “ke,” kwa hiyo tuongeze tu pale (b) itakuwa (vi) baada ya (v) mapendekezo yangu. Minister shall have regard to the gender balance at all times the number of female members shall not be below two, it can be three, four but not below two.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante eneo lingine ...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Pindi Chana umepeleka marekebisho? Umepeleka Jedwali la Marekebisho?

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, jedwali lilikuwa linachapwa, sijui kama litawahi. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Haya endelea na mchango wako.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nadhani watu wa printer wanaweza wakananilii, haya ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ukurasa huo, huo section 12, hiki kifungu cha 12 naipongeza sana Serikali kutuletea haya marekebisho, kwamba hiki Kifungu sasa kinafutwa, kwa kweli nitumie nafasi hii kupongeza, lakini pia kwa ruksa yako nitumie nafasi hii kukumbashana kwamba hata kama hapa mwisho ilisema; “and shall not be subject to review by any court.” Kwa mujibu wa Katiba kwamba Katiba ni sheria mama hata kama hiki kifungu kilikuwepo haizuii mtu kwenda Mahakamani kudai rights zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hata kama kilikuwepo mtu ana rights zake Mahakamani kwenda ruksa. Kwa sababu tunajua nini maana ya Katiba, lakini napongeza kabisa kifungu hiki kufutwa, lakini haki ya wananchi ilikuwa haijazuiliwa, walikuwa wana haki kwenda kudai their right in any court kwa sababu wanakwenda kwa mujibu wa Katiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haraka, haraka kule kwenye vifungu ukurasa wa 12, section 16, ninaposoma mimi section 16 pale kuna 16(b)(6)(a) inasema; “in the case of an individual person, to a fine not exceeding ten million shillings or to imprisonment for a term not exceeding two years,” naona kama minimum sanction haipo, kwa hiyo naomba tu wataalam watuwekee minimum. Naona hapa kuna maximum, minimum haipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine pale 17(6)(a) in the case of individual personal to a fine not exceeding ten million shillings or imprisonment for a term not exceeding two years naona kama minimum haipo, tuweke minimum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ukurusa wa 13, section 18(d) nadhani hiki kifungu sijui kimeondolewa, kuna maneno yapo pale sikuwa nimeyaelewa, haya maneno yanasema hivi (d) in sub-section (2)(b), by deleting the words…, kwa hiyo napongeza kwa sababu haya maneno yalikuwa hayajaeleweka na Waziri ametuletea yawe deleted; fifty thousand million shillings nikawa sijaelewa, fifty thousand million, lakini ndiyo yanakuwa deleted yaani ndiyo inaboreshwa hivyo, pongezi zangu zipo hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, enelo lingine ukurasa wa 14, kifungu cha 30B(3) page 14; “A person who refused to produce further information under this section, commits an offence and shall, on conviction, be liable to a fine not exceeding twenty million, minimum haipo, au tunaenda na maximum bila kufunga chini kwamba Hakimu, Jaji ataamua kama ni shilingi kumi, shilingi ishirini, thelathini, laki au ni vizuri kufunga na chini not less than.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine nitaji-focus sana kwenye masuala ya fine. Ukurasa wa 15 hiki ni kifungu cha 30C maximum fine ipo, minimum again haipo. Hiyo ni 30C(2); A registered member who refused to provide information or clarification sought under this section commits an offence and shall, on conviction, be liable to a fine of not exceeding five million shillings or to imprisonment; minimum haipo na hii sheria inarekebisha sana maboresho haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 16 kifungu cha 40, napongeza kifungu cha 23 kina amend kifungu cha 40 annual performance ambapo kifungu cha 40(2) inasema na nianze na 40(1) The Board shall prepare and submit to the Minister within four months after the close of each financial year the annual report on the performance of the Board during the financial year. (2) The Minister shall, at the earliest available opportunity, cause a copy kuwa submitted before the National Assembly.

Je, kuna haja ya kuweka muda au tuache earliest available opportunity. Tunaweza tukakopa ile ya juu within four months na yeye akipokea within four months ailete Bunge maana within four months lazima kuna kikao cha Bunge, lakini itategemea kama ni cha bajeti au cha Miswaada any way ndiyo najiuliza tu kuna haja ya kuweka muda.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kengele ya kwanza au ya pili?

NAIBU SPIKA: Ya pili.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
THE WRITTEN LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) (NO. 5) ACT, 2021
MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Kwanza nampongeza Mwanasheria Mkuu na Serikali kwa kutuletea haya maboresho, naunga mkono hoja. Naenda ukurasa wa tano wa Muswada, pale kwenye tafsiri; na ninaanza na ile tafsiri ya neno “forced begging.” Hii iko kwenye Kifungu cha 4 cha Muswada ambapo imeongeza Tafsiri ya maneno mbalimbali, lakini nitajikita kidogo pale kwenye “forced begging.” Naunga mkono forced begging. Kuna begging na forced begging.

Mheshimiwa Spika, forced begging ni pale ambapo mtu analazimishwa kwenda kuomba. Nimewahi kusimamia baadhi ya kesi na nitaitaja mojawapo; kuna mama mmoja alikuwa anakusanya watoto walemavu, anasema anakwenda kuwasaidia. Anawachukua vijijini, mikoani. Mbaya zaidi alikuwa anawachukua kwenda kwenye nchi nyingine kutoka kwenye nchi yetu. Naihifadhi hiyo nchi kwa ajili ya usalama. Katika ile nchi nyingine, wale watoto takribani 10 na kitu, walikuwa wanachukuliwa na taxi asubuhi, wanashushwa kwenye vituo mbalimbali wawe beggars. That is forces beggars under eighteen. Jioni anahesabia kila mtoto amepata shilingi ngapi katika omba omba. Alikuwa anapata takribani kwa siku shilingi 300,000/= ya Tanzania. Sasa naafiki kabisa kuongeza maneno tunapozuia usafirishaji haramu wa watu, neno “forces begging” liwepo. Naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine, kwa sababu nimesema kuna watu wametumika kwenye ku-force beggars, kwenye kifungu cha 10 ambacho kinarekebisha Kifungu cha 26, sheria hiyo hiyo, trafficking in person, yenyewe inasema the sale proceeds of any property, Kifungu cha 10 (2) itakuwa confiscated or forfeited under this Act na subject to approval of the Minister responsible itakwenda to be deposited kwenye fund. Sasa kama kuna mali imepatikana, itataifishwa. Nilikuwa nauliza: Je, fedha zinazopatikana kotokana na trafficking in human na zenyewe zimo hapa, tunaziweka? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine kwa haraka sana kutokana na muda, hii Immigration Act inakuwa ni point yangu ya mwisho kumalizia. Naomba pale Kifungu cha 30, 10A Amendment of the Meat Industry Act, inasema “recommendation by the Registrar and after consultation with the Minister delegate some of the function to a Local Government Authority.” Sasa nilikuwa naomba neno registrar lipewe tafsiri, maana tuna Ma-Registrar wa aina nyingi. Baada ya hapo, kifungu hiki kinasema: “The Board may upon recommendation by the Registrar and after consultation with the Minister delegate some of the functions to the Local Government Authority.” Naafiki, baadhi ya shughuli watazipa Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Spika, hata nikasema tukiafiki hii, lazima Local Government Authority Act (Na. 8) na (Na. 7) pia tukaangalia namna ya kuziboresha ili ziweze kupokea hiyo mamlaka ya Waziri. Maana kule inatambua Waziri wa TAMISEMI, lakini hapa atakuwa Waziri responsible for masuala ya meat.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine naungana kabisa na Mwanasheria Mkuu, Kifungu cha 44, hii ni Sheria ya Amendment of Tanzania Wildlife Research Institute Kifungu cha 44 (c) ambapo pale wamesema: “to a person convicted under this Act may be withdrawn.” Inazungumzia masuala ya permit inaweza kuwa withdrawn. Badala ya neno “withdrawn”, naomba litumike neno revoked. Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu alisema nadhani wakati anawasilisha, hilo jambo limezingatiwa.

Mheshimiwa Spika, sasa nakwenda kwenye Amendment of Immigration Act kwamba Uhamiaji sasa inakuwa jeshi. Kwanza naunga mkono hoja, ni sawa kabisa uhamiaji kuwa jeshi. Kwanza tumechelewa kusema uhamiaji kuwa Jeshi, ilipaswa tufanye maamuzi haya muda mrefu. Idara hii ya uhamiaji inasaidia katika mipaka masuala mbalimbali. Katika mipaka yetu lazima tujiridhishe watu wanaoingia ndani ya nchi kuangalia alama za vidole (finger print), kuna masuala ya Visa na ndiyo maana kuna baadhi ya maeneo mtu akiomba Visa, tunamwambia Visa yako itakuwa ni referred, hadi tukaangalie kama wewe ni mtu salama, huna makosa ya jinai, you are not a criminal. Kwa hiyo, haya yote yanafanyika na masuala ya Uhamiaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kitendo cha kusema Uhamiaji iwe jeshi, ninaafiki. Vile vile Uhamiaji wanashughulika na mambo ya passport. Kupitia Passport tusipokuwa salama, nchi yetu inaweza ikatumika kufanya ubadhirifu. Tanzania kuna maneno hatujui jinsi ya kuyatumia, tunayasikia tu kwa wenzetu. Kuna maneno kama terrorist, Ugaidi kuna maneno kama Boko haramu, hatuyajui sisi ni kisiwa cha amani; kuna maneno kama Al-Qaida hatuyajui, ni kisiwa cha amani; tunapoona amani Tanzania ipo, tusione vyaelea, vimeundwa na wanaoundwa ni pamoja na Uhamiaji. Kwa hiyo, kitendo cha kusema leo kwamba Uhamiaji iwe jeshi, naunga mkono, ninaafiki na kwa kweli kwa namna moja au nyingine naweza nikasema kwanza tumechelewa ilipaswa ije kabla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza kwa mujibu wa Sheria; na hii leo ndiyo tumeletewa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali; na leo tumeona Jeshi la Uhamiaji sasa itakuwa ni force and not department, kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Uhamiaji tuna nchi; boda ya kwetu na nchi moja ni kilometa takribani 900. Hiyo ni boda tu. Kilometa 900 kwenye barabara ni sawa sawa na kutoka Dar es Salaam - Iringa mpaka Makambako, hiyo ni boda tu. Sasa maeneo haya wanaweza wakaingia wahalifu. Kwa hiyo, hawa watu wa Immigration kwenye boda wanasaidia sana kuhakikisha wanaoingia ni salama na wanaoingia ni sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni muafaka kabisa iwe jeshi, wapewe bajeti ya kutosha na vile vile kama inavyoelezwa, “the department established under subsection
(1) shall be a force within the Ministry and in the capacity, it shall be governed in the manner and style similar to other force within the Ministry. Vile vile lazima wapewe rights na privilege kutokana na utaratibu wa jeshi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. BALOZI DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)