Parliament of Tanzania

Rais azindua mpango wa ugawaji wa Madawati yaliyotengezwa na Ofisi ya Bunge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amezindua mpango ugawaji wa Madawati yaliyotenegnezwa kutokana na fedha zilizopatikana baada ya Ofisi ya Bunge kubana matumizi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Mhe Rais alimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Azzan Zungu (Mb) madawati hayo kwa niaba ya Wabunge wote

Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza Wabunge na Ofisi ya Bunge kwa ujumla kwa kutikia wito wa kuchangia upatikanaji wa Madawati katika Shule za Msingi na Sekondari kwa ajili ya kuondoa adha ya Wanafunzi kukaa chini.

Aidha, Mhe Rais amelitaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza kuongeza kasi ya utengenezaji wa Madawati yaliobakia ili yakamilike kwa haraka na yaanze kutumika.

Awali akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mhe Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson alimshukuru Mhe. Rais kwa kukubali kwake kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji wa madawati.

Naibu Spika alisema kuwa kuwa mnamo Aprili 11, 2016 Ofisi ya Bunge ilimkabidhi Mhe Rasi hundi yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kwa ajili ya kutengeneza madawati.

Dkt Tulia aliendelea kusema kuwa Fedha hizo zilitokana na mpango wa Serikali wa kubana matumizi mabapo Katika kutekeleza agizo hilo, Ofisi ya Bunge ilitoa kiasi hicho kutoka kwenye Mfuko wa Bunge (The National Assembly Fund) ikiwa ni mchango wa Wabunge katika jitihada za Serikali za kuhakikisha madawati ya kutosha yanapatikana kwenye Shule za Msingi hapa Nchini.

Naibu Spika aliongeza kuwa Kazi ya utengenezaji wa madawati imetekelezwa na Jeshi la Magereza na SUMA JKT kwa makubaliano kuwa ikamilishwe kwa awamu mbili.

Mbali na hayo Dkt Tulia alisema kuwa katika awamu ya kwanza tayari jumla ya Madawati 53,450 yamekamilika na kwamba Tume ya Utumishi wa Bunge imeandaa utaratibu na vigezo vya ugawaji wa madawati hayo. Vilevile, Tume imeandaa idadi ya mgao wa madawati katika Mikoa itakayopata katika Awamu ya Kwanza na Mikoa itakayopata katika awamu ya pili.

Mikoa ilitakayohusika kwenye awamu ya kwanza ya ugawaji madawati ni pamoja na Pwani, Morogoro, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Iringa, Njombe, 8. Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Visiwa vya Unguja, Pemba Tanga na Dar es Salaam.

Katika awamu ya kwanza jumla ya madawati 61,385, yatagaiwa katika jumla ya Majimbo ya Uchaguzi 155 kati ya Majimbo 264.Kiuwiano wa majimbo ni sawa na Asilimia 59 wa madawati yote 120,000.

Aidha, ugawaji wa madawati katika awamu ya pili ambayo JKT na Magereza yanatarajiwa kuwa tayari ifikapo tarehe 30 Septemba, 2016, utahusisha kanda zingine mbili za mikoa ya kanda ya Kaskazini na Ziwa na Kanda ya Kati na Magharibi.

Pamoja na Viongozi wengine wa Kitaifa hafla ya Ugawaji wa Madawati ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mawaziri na Wabunge mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Makamishina wa Tume ya Utumishi ya Bunge.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's