Parliament of Tanzania

Naibu Spika akagua ukarabati wa ukumbi wa Bunge siku moja kabla ya kuanza kwa Bunge la Bajeti

Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amefanya ukaguzi wa ukarabati wa ukumbi wa Bunge uliokamilika hivi karibuni, siku moja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Bunge la bajeti unaotarajiwa kuanza tarehe 19 Aprili hadi 01 Julai, 2016 Bungeni Mjini, Dodoma.

Ukarabati wa ukumbi wa Bunge ulianza kufanyika mara baada ya mkutano wa Pili wa Bunge. Ukarabati huo pamoja na mambo mengine ulihusisha ukarabati wa paa la ukumbi huo pamoja na uwekaji wa meza.

Ukaguzi huo ulienda sambamba na utengengezaji wa Studio za Bunge. Studio hizo ambazo nazo zimekamilika zitatumika katika urushwaji wa matangazo ya vikao vya Bunge na vipindi vingine vinavyohusu Bunge kupitia Chaneli Maalumu ya Televisheni na Radio ya Bunge.

Akizungumzia ukarabati huo Naibu Spika amelezea kufurahishwa na kuridhishwa nao huku akisema kazi hiyo uliofanyika kwa muda mfupi ni ya uhakika na sasa ukumbi wa Bunge upo tayari kwa ajili ya mikutano ya Bunge.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's