Parliament of Tanzania

LAAC yaishauri Halmashauri ya Jiji la Arusha kufanya tathimini ya vyanzo vya mapato

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) , imetoa ushauri kwa Halmshauri ya Jiji la Arusha kufanya tathimini upya ya vyanzo mapato kwa lengo kuongeza vyanzo hivyo.


Ushauri huo ulitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Abdalla Chikota wakati Kamati hiyo ilipokuwa ikiihoji Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhusu hesabu za mwaka wa fedha 2014/15.


Mheshimiwa Chikota alisema Kamati inaona kwamba Jiji hilo lina fursa nyingi za biashara na linategemewa katika kuongeza Pato la Taifa.


“Kamati inaliagiza Jiji la Arusha kufanya tathimini upya ya vyanzo vyake vya mapato, kuongeza vyanzo vipya pamoja na kudhibiti mapato ya vyanzo vya zamani ili kutoikosesha Halmashauri ya Jiji fedha za kutosha,” alisema.


Mbali na kutoa ushauri huo, pia Kamati hiyo iliiagiza Halmshauri ya Jiji hilo irudishe Sh. Milioni 39.7 ambazo zilitakiwa ziende kwenye Mfuko wa Afya na kwamba vielezo vya matumizi ya fedha hizo vipelekwe kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili afanyie uhakiki.

“Kamati pia inaitaka Halmashauri ya Jiji la Arusha iwasilishe vielelezo vyote vya mradi wa Sh. Milioni 740 kwa CAG kabla ya Novemba 30 mwaka huu ili aweze kufanya ukaguzi,” alisema.


Alisema Kamati yake pia haijaridhishwa na maelezo ya fedha kiasi cha Sh. Bilioni 1.9 za Mfuko wa Wanawake na Vijana ambazo zimechukuliwa na kuelekezwa katika matumizi mengine na kwamba Kamati inaagiza fedha hizo zirejeshwe mara moja.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Arusha,Mheshimiwa Kalisti Bukhay aliishukuru Kamati hiyo kwa kumualika katika kikao hicho na kuahidi kutoa ushurikiano katika kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Kamati.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's