Parliament of Tanzania

Hatimaye Marehemu Sitta azikwa huko Urambo huku, Mhe Spika akiungana na Viongozi wengine katika mazishi hayo

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai ameungana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Watanzania kwa ujumla katika mazishi ya aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa marehemu Samuel John Sitta yaliyofanyika nyumbani kwake Wilayani Urambo, Tabora.

Marehemu Sitta aliaga Dunia tarehe 7 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Aidha kabla ya kusafirishwa kwenda Urambo kwa ajili ya mazishi Bunge lilipata fursa ya kutoa heshima za mwisho katika tukio ambalo ni la Kihistoria na ambalo halijawahi kutokea ambapo mwili wa Marehemu Sitta uliingizwa ndani ya ukumbi wa Bunge na Waheshimiwa Wabunge wote wakapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa pamoja.

Akitoa salamu za rambirambi wakati wa Mazishi ya Marehemu Sitta nyumbani kwake Urambo, Spika Ndugai aliwaambia Wanaurambo na Watanzania kwa ujumla ambao walikuja kumuaga kiongozi wao kuwa daima Bunge litamkumbuka Mhe Sitta kwa mchango wake uliotukuka wakati akiwa Spika wa Bunge la Tisa.

Kwa upande mwingine akizungumza kwa niaba ya Wanadodoma Mhe Ndugai aliwashukuru Wanaurambo kwa Uongozi wa Marehemu Sitta kutokana na mchango wake mkubwa katika kufikisha Dodoma mahali ilipo sasa wakati akiwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao makuu Dodoma (CDA).

Mhe Ndugai aliongeza kuwa wakati Serikali kwa sasa ikitekeleza adhma ya kuhamia Makao Makuu ya nchi ambayo ni Dodoma, kuna kila sababu ya kukumbuka mchango wa Marehemu Sitta katika kuendeleza Mji wa Dodoma na hivyo kwa niaba ya Wanadodoma wote anashukuru kwa Uongozi wa Marehemu Sitta katika suala hilo.

Pamoja na hayo Mhe Spika pia aliwapa pole Mjane wa Marehemu Mama Magreth Sitta (Mb), pamoja Mama wa Marehemu Hajjat Zuwena Fundikira na Familia nzima kwa msiba uliowapata huku akiwatia moyo kwamba wanapaswa kuendelea kumtumainia Mungu hasa katika kipindi hichi kigumu.

“Ninapende kuwahakikishioa Wanaurambo kwamba yale yote aliyoyafanya Marehemu Sitta na atakayoyafanya Mbunge wenzetu Mhe Magreth tutashirikiana naye katika kuyaendeleza na kuyatekeleza kwa manufaa ya Wanaurambo wote,” alisema Mhe Spika.

Viongozi wengine wakiwemo Mawaziri na Wabunge pamoja na Mhe Spika waliungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ambaye aliwaongoza mamia ya Wanaurambo na Watanzania kwa ujumla katika kumpumzisha Spika huyo wa Bunge la Tisa ambaye alijuliakana kama ‘Spika wa Kasi na Viwango’ katika nyumba yake ya milele.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's