Parliament of Tanzania

Dkt. Tulia achaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12

Bunge limechagua Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12.

Akitangaza matokeo hayo mara baada ya uchaguzi kufanyika, Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema Dkt. Tulia amepata kura 350 kati ya kura 354 zilizopigwa.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, aliwashukuru Wabunge wote kwa ushindi huo wa kishindo na kuahidi kufanya nao kazi bega kwa bega bila kujali tofauti za kisiasa.

“Naahadi nitawatumikia, nitafanya kazi kwa ufanisi katika kazi zangu kama Naibu Spika, msisite kuniletea hoja zenu pale mnapukuwa nazo,” alisema

Aidha, alisema atamshauri vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumkia uzoefu alionao ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's