Parliament of Tanzania

Wabunge watoa posho yao kama Rambirambi kwa wafiwa wa Ajali ya Arusha

Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekubali kwa kauli moja kutoa posho yao ya siku moja kama rambirambi kwa wafiwa wa ajali iliyosababisha vifo vya Wanafunzi 32, Walimu 2 na Dereva 1, wa Shule ya Msingi Lucky Vicent ya Mkoani Arusha, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo la Rhotia Marera, Wilayani Karatu Mkoani Arusha.


Kufuatia uamuzi huo jumla ya shillingi milioni mia zitatolewa kama rambirambi ambapo shillingi milioni 14 zitatolewa na Ofisi ya Spika na shillingi Milioni 86 zitatokana na posho za Waheshimiwa Wabunge.


Akielezea utaratibu huo baada ya Wabunge kusimama kwa dakika moja kuwakumbuka wanafunzi na wafanyakazi walipoteza maisha katika ajali hiyo, Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amesema fedha hizo zitapelekwa moja kwa moja kwa wafiwa hao kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Mrisho Gambo.


“Tumekubaliana kwa kauli moja humu Bungeni, tutoe posho ya siku moja kamarambirambi yetu, posho hiyo tutaipeleka mara moja kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na itagawiwa sawa sawa kwa wafiwa wote,Alisema Mheshimiwa Spika.



Aidha kufuatia ajali hiyo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alimtumia Salam za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo


“Mhe Mkuu wa Mkoa nakupa pole sana, nimepokea kwa mshtuko taarifa hii ya ajali iliyogharimu maisha ya watoto wetu, hakika hili nipigo kwa taifa zima, na muomba Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi.” alisema Mheshimiwa Ndugai.


“Natoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu, vile vile ninawaombea majeruhi wote wa ajali hiyo wapate uponyaji wa haraka” aliongeza Mheshimiwa Ndugai.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's