Parliament of Tanzania

Kamati ya Bajeti, Uongozi zakutana na Serikali kufanya majumuisho ya uchambuzi wa Bajeti

WAZIRI Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa amesema Serikali itayafanyia kazi maboresho yaliyopendekezwa na Kamati za Kudumu za Bunge kuhusu bajeti za Wizara mbalimbali wakati wa uchambuzi wa bajeti hizo uliofanywa na kamati za kisekta .

Mhe. Majaliwa alitoa ahadi hiyo Mjini Dodoma jana baada ya kusikia maoni ya baadhi ya wenyeviti wa Kamati za Bunge kuhusiana na mapitio ya bajeti katika wizara wanazozisimamia kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti walipokutana na serikali kwa lengo la kupokea mapendekezo na maoni mbalimbali ya Kamati za Bunge baada ya kamati hizo kumaliza kazi ya uchambuzi wa bajeti.

Waziri Mkuu alisema Serikali imesikia maoni yote na kwamba bado ipo nafasi kwa kamati hizo kukutana na Kamati ya Bajeti kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo yao baada ya kuchambua bajeti ya kwa wizara wanazozisimamia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mh. Hawa Ghasia alisema Kamati yake imeshapokea maoni ya baadhi ya Kamati na imeanza kuyafanyia kazi. Aidha, alisema yapo mapendekezo ambayo bado hayajawasilishwa katika kamati yake na kwamba bado Kamati yake ina nafasi ya kukutana na kamati hizo.

Awali akifunga kikao hicho, Spika wa Bunge, Job Ndugai alizipongeza Kamati za Bunge kwa kazi nzuri walizozifanya wakiwa Dar es Salaam na kuzitaka kutekeleza majukumu yake hata katika kipindi hiki ambacho wajumbe wapo Mjini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya bajeti.

Mhe. Spika pia aliitaka Kamati ya Bajeti kuendelea kufanya kazi na kwamba wasikatishwe tamaa na ufinyu wa bajeti. Awali wakiwasilisha taarifa za mapitio ya bajeti katika kamati zao, baadhi ya wenyeviti wa kamati walieleza mapendekezo yao ya kutaka baadhi ya maeneo yaongewe fedha katika bajeti ili yaweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwemo miradi yamaedeleo.

Bajeti hizo za wizara zinatarajiwa kuanza kuwasilisha kuanzia Aprili 24 katika Mkutano wa Bajeti wa Bunge la 11 unaoendelea Mjini Dodoma .

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's