United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
All Contributions |
---|
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017MHE. LAMECK O. AIRO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia kama ifuatavyo: Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa kuwa na aina nyingi za matunda. Ninaishauri Serikali kama bado wataruhusiwa wafanyabiashara kuingiza powder ya kuchanganya na maji na kutoa juice, hapo itafanya wawekezaji wa viwanda vya kutengeneza juice kushindwa kuwekeza, kwa sababu kijiko kimoja cha powder kinachanganya lita tano za maji na kutoa juice. |