Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Eliezer Mbuki Feleshi (15 total)

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa Bungeni kwenye Mkutano wa Sita na Mkutano wa Saba wa Bunge pamoja na Uchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Sheria Ndogo zilizowasilishwa kwenye Mkutano wa Tatu na Mkutano wa Nne wa Bunge
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nikushukuru wewe kwa kunipatia fursa hii, pia napenda sana kuishukuru na kuipongeza Kamati ya Sheria Ndogo ikiongozwa na Mheshimiwa Jasson Samson Rweikiza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapongeza sana uchambuzi ambao umefanywa na Kamati pamoja na maazimio ambayo yametolewa. Sisi tunafarijika kwamba katika sheria mama nyingi tulizonazo takribani 446 na sheria ndogo zaidi ya 40,000; dosari ambazo zimeendelea kujitokeza zinaendelea kupungua kadri ya hatua mbalimbali zinavyozidi kuchukuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo kwa ushahidi ambao Kamati inapochambua inakutana nayo, inatufanya sisi Serikali/Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuona bado tunao wajibu wa kuhakikisha kwamba sheria zetu zinazotungwa kwa mujibu wa Katiba yetu na sheria zetu zinakidhi yale matakwa na malengo ambayo pale zimetungwa. Kwa hiyo, tutaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba dosari ambazo zimetajwa, zinaendelea kupungua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Chamuriho katika mchango wake amedhihirisha hii kwa kueleza kwamba wamepitia sheria ndogo nyingi lakini dosari zikawa chache. Kwa hiyo, kati ya mambo ambayo Serikali inayafanya kwa sasa mojawapo ya Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inakamilisha mwongozo ambao utatumika kuongoza mamlaka zinazotunga sheria ndogo katika ngazi ya halmashauri, Mawizara na mamlaka zingine kwa wote ambao walio na dhamana tunaamini mwongozo huu pamoja tunaamini mwongozo huu pamoja na mambo mengine utajaribu kutoa maelekezo kwa mambo yale ya msingi ambayo kwayo wote walioko na dhamana wanatakiwa kuyazingatia, hili nafikiri mwongozo ule.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili utaendana na jitihada za Serikali za kuona jinsi ambavyo tutaendelea kutoa elimu kwa wote ambao walio na dhamana ya kutunga sheria ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaelewa kwamba sheria yoyote sheria mama nyingi mchakato wake unahusisha tafiti na mawasilisho katika hatua mbalimbali kitu ambacho ni tofauti kidogo na sheria ndogo, kwa hiyo tunaona upo umuhimu kama Waheshimiwa Wabunge walivyochangia kuona kwamba umuhimu wa kutoa elimu, lakini na hata kutafuta utafiti ni jambo ambalo litahitaji kuachwa nyuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, ofisi yangu kwa sasa na Waheshimiwa Wabunge inamalizia kufanya usajili wa wanasheria wote walio kwenye huduma ya umma na mpaka kufikia sasa tuna wanasheria 2,550 na hawa wamo pamoja na hizi waliomo kwenye halmashauri na mwezi huu tutazindua Public Bar Association (Chama cha Mawakili wa Umma Tanzania). Lengo lake moja wapo ni kuhakikisha kwamba wanasheria wote tulionao kwenye huduma umma wanakuwa na kiwango kwa maana ya kuwa na elimu na kuongeza stadi zao za kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kupitia hatua tunazozichukua tunaamini tutaendelea kujitathimini jinsi ambavyo hatua tunazozichukua kwa kuhakikisha wanasheria walioko kwenye Halmashauri, walioko kwenye Mamlaka za Mikoa na walioko kwenye Mawizara pamoja na hata zile taasisi kubwa, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (Solicitor General) na Ofisi yangu kwa pamoja tuhakikishe kwamba kila mmoja wetu anatimiza wajibu wa kuhakikisha kwamba sheria zinazotungwa na Bunge hili basi ziwe zile zile na zenye ubora lakini na sheria ndogo zinazotungwa ziwe zinaendana na masharti mama yaliyo kwenye sheria kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda pia nitoe rai ofisini kwangu kuna mfumo wa kieletroniki ambao ukiingia kuna sehemu ya mrejesho, ningefikiri hili ni eneo mojawapo la kusaidiana kwa wale wote ambao wanahusika na kazi za kisheria na huduma za kisheria na changamoto za kisheria mambo mengine si ya kusubiri yakaenda na urasimu mrefu, haihitaji kuweka neno la siri yaani password kuingia kwenye ile fomu ya mrejesho na sehemu ya mwisho ya ile fomu ofisi yetu inapenda kujulishwa jambo lolote na maoni yoyote ambayo mtu anaweza akaandika na akapata mrejesho.

Kwa hiyo, hizi ni njia ambazo naamini nazo tutajaribu kuona, tunaamini sisi kwamba tukizitumia vizuri zitaongeza thamani ya huduma ambayo inatolewa na Serikali upande wa sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna jambo lingine ambalo nifikiri halijazoeleka sana kwa hizi sheria ndogo; kwa sheria mama mara nyingi mnaona Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge tunakuja na sheria na miswada ya sheria mbalimbali. Kwa sheria ndogo marekebisho mengi au kufuta sheria ndogo zilizokwisha kutungwa ni zile nyingi tulizopokea hasa kwenye Mawizara, naona kutoka halmashauri ni mara chache sana, basi ningetoa rai tu kwamba tusisubiri na kuelezea sana maumivu yanayotokana na dosari zile za msingi ziko kwenye sheria ndogo taratibu zingine za kufahamisha ofisi yangu, Wizara ya Katiba na Sheria na mamlaka zingine nafikiri zichukuliwe haraka kama walivyo madaktari wowote wanaotibu binadamu tusisubiri ugonjwa mpaka unakuwa mkubwa au kuna kuwa na madhara haki za watu kupotea bila kuchukua hatua ambazo kumbe tungepata taarifa tungechukua hatua ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naishukuru na kuipongeza Kamati kwa mapendekezo yake na mimi kama sehemu muhimu katika utekelezaji wa maazimio haya upande wa Serikali nitashirikiana na wenzangu wote wa Serikalini kuhakikisha huo muda walioutoa tutafanya linalowezekana kupunguza dosari zilizojitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianze kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutuweka hai na kutuwezesha kuwepo kwenye majukumu yetu.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru pia wewe binafsi kwa jinsi ambavyo umeendelea kuongoza shughuli za Bunge hili. Aidha, nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kuendelea kusimamia Utawala wa Sheria na vile vile naamini kazi inayofanyika kwenye Mkutano huu hasa kwa hizi siku nne, ni matokeo ambayo ni ya kazi ya Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo kwa mujibu wa Ibara ya 153(4) kila anapokabidhiwa basi inawasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu. Ndio msingi kwa mujibu wa Nyongeza ya Nane ile, Sehemu ya Nne ya Kamati hizi tatu zilizowasilisha taarifa hii kuweza kuwasilisha taarifa zao pamoja na kuwezesha mjadala ambao unaendelea.

Mheshimiwa Spika, niwashukuru sana Wenyeviti wa Kamati pamoja na Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao na vilevile niendelee kuwashukuru sana Wabunge kwa yote ambayo wamechangia. Vile vile niwashukuru Waheshimiwa Mawaziri na nikimaanisha Mawaziri kwa maana yangu na kwa maana ya sheria zetu na Katiba hasa kwa mujibu wa ile Ibara ya 54. Wao ni sehemu ya utendaji kazi zinazoongozwa na mamlaka inayotawala chini ya Mheshimiwa Rais. Kwa hiyo Waheshimiwa Mawaziri nawapongeza sana.

Mheshimiwa Spika, zaidi ya wachangiaji 70 wameshiriki kuchangia hoja ambayo iko mezani na mambo kadhaa wa kadha yamejitokeza. Wapo ambao wameeleza ni vizuri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aongezewe mamlaka na hata ikiwezekana kuendesha mashtaka ya wale ambao wanabainika kuwa wamekinzana na sheria. Pia wapo wale ambao wameona kwamba sheria zinazotolewa kwa wahusika hazifai kabisa na wengine wamependekeza adhabu za kunyongwa na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, vilevile wako ambao wameshangazwa na kuona watu ambao kwa njia moja au nyingine wameonekana kwenye taarifa kwa kipindi husika wakiwa bado kwenye utumishi wa umma. Pia wapo ambao wameona kipindi kichotolewa kujadili taarifa hizi ni kifupi mno na hakitoshi na muda unastahili kuongezwa. Wapo vile vile ambao wamesema Halmashauri za Wilaya zifutwe na wapo ambo wametaka kuwe na list of shame.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na hili la mamlaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ningependa tu kurejea kwamba nchi yetu inaongozwa kwa utawala wa sheria na misingi ya utawala bora, ambapo kunakuwa na mgawanyo wa majukumu, lakini vilevile ni kitu ambacho Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amepungukiwa. Tukiangalia mamlaka aliyonayo chini ya ibara ya 143, bila shaka wengi watakubaliana nami kwamba Katiba imempatia mamlaka yanayojitosheleza kwa sababu hata kama taarifa yake isingeletwa na Serikali, yeye kwa mujibu wa ibara ya 143(4), angekuwa na mamlaka ya kuileta.

Mheshimiwa Spika, vilevile tukisoma Katiba pamoja na ile Sheria anayoifanyia kazi Public Audit Act, kifungu cha 27, 28 na 29 vimempa wigo mpana kufanya Forensic Audit, Performance Audit na other audits. Sasa tunapofika hapa ndipo tunaona uwajibishwaji wa watu wale ambao wamepewa dhamana ya kutekeleza majukumu ya Serikali na mashirika yake wanavyowajibishwa kwa njia mbalimbali kwa kufuata misingi yetu ya utawala bora na vilevile kwa kuzingatia nchi yetu ina mgawanyo wa madaraka. Wapo ambao wanatuhumiwa ambao wamebainika na wakachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi ambapo kifungu cha 6(1) kinagatua mamlaka ya kinidhamu kwa Accounting Officers. Kwa hiyo tunapofika mahali hapa mamlaka haya yako mpaka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, yawezekana baadhi ya michango watu wanashangaa kuwaona watu mtaani, lakini yule mtu tayari shauri lake lilishachunguzwa na tayari lilishafanyiwa kazi na mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU, kwa mfano kwa 2020/2021, kati ya taarifa walizopokea wao kufanyia kazi kutoka kwa taarifa ya CAG ni 533, taarifa 110 zilifungwa kwa kukosa mashiko. Hii maana yake ilikuwa ni kutekeleza yale majukumu ambayo yapo kisheria, vyombo chunguzi vinapopokea taarifa vinachunguza.

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna hatua za kidhamu katika taarifa 102 zilichukuliwa. Kwa hiyo nalisema hili ili kutuhumiwa ni jambo moja, kuthibitishwa na ukosaji au hatia ni jambo lingine na mchakato wa kusikiliza mashauri yenye tuhuma umegatuliwa kikatiba, mahakama kwa upande mmoja kama chombo na mhimili unaosimamia haki wa ngazi ya juu.

Mheshimiwa Spika, vilevile kwa mujibu wa Ibara yetu ya 13(6) tunajua kuna vyombo vingi pamoja na hao Accounting Officers, hivyo, ningependa ieleweke kwamba tuhuma ni jambo moja na mchkato wa kuthibitisha ni jambo lingine. Mijadala kama hii inavyoendelea inawezekana watu wakaonekana mitaani na ndiyo hao wanasema kwamba ni vizuri waorodheshwe ikibidi waletwe au wakutwe Gerezani kesho, lakini yule mtu kwa mujibu wa Sheria zetu ameshafikishwa mbele ya Mwajiri ambaye ndiye disciplinary authority, akasomewa mashtaka wakaleta utetezi na akatiwa hatiani kwa mujibu wa zile taratibu zilizopo kwenye Sheria ya Utumishi wa Umma pamoja na Public Finance Act.

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo ningependa kuchangia ni kuhusu habari ya kuongezewa muda, nafikiri hili ni jambo ambalo mimi sioni kama ni baya, kwa sababu hata kwa mujibu wa Ibara ya 143 (3), CAG anachotakiwa ni kuandaa taarifa walau afanye mara moja na kuwasilisha taarifa sasa akiongezewa inakuwa vizuri zaidi, lakini Kamati hizi nazo zikiongezewa muda ni jambo la heri. Pia kuna jambo lingine ambalo limenivutia sana la wale Wabunge wenye kusema Halmashauri zifutwe, ninatambua Waheshimiwa Wabunge wao ni sehemu ya Mabaraza ya Madiwani na wao wapo kwenye Planning and Finance Committees. Kwa hiyo, ningependa ieleweke kwamba ni vizuri sana chochote kinachoazimiwa hapa, vilevile labda na waliohusika kwenye Halmashauri zile kwa ujumla wao, ni vizuri tusiangalie in isolation.

Mheshimiwa Spika, jambo hili ningetamini ingelikuwa ni mimi, Bunge hili lilivyo - live na yale Mabaraza au ngazi ya chini yangekuwa live. Yawezekana ndugu zangu wengine mmeongea hapa, msingeweza kuyaongea kama mlivyoyaongea. Ninapenda kuomba na kuungana na baadhi ya Wabunge wengi ambao wamesema ni vizuri sheria zetu tuendelee kuzihuisha na nipende tu kutoa taarifa kwamba Sheria ya Public Procurement Act tayari inafanyiwa review na wakati wowote kwa mujibu wa taratibu zetu za mkondo wa kutunga sheria na marekebisho, itawasilishwa kwenye Bunge lako kila kitu kitakapokuwa kimekamilika, ni pamoja na sheria zingine ikiwemo ile ya PPP na zinginezo.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mikataba, vilevile Serikali imeendelea kuchukua hatua ambazo ni mahsusi na nafikiri tumejitahidi kuwa wawazi sana, mmeona tarehe 29 Mwezi wa Tisa mwaka 2022, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo yake kuhusiana na Watendaji ndani ya Serikali kuhakikisha kwamba mikataba yote iingiwe kwa kufuata miongozo pamoja na taratibu ambazo inatuwezesha kama Taifa kuwa na mikataba bora.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naomba niendelee kupongeza chochote kilichoendelea katika mijadala hii ni ombi langu kwamba nia njema iwepo ili tuweze kufikia maendeleo mazuri. Mheshimiwa Shigongo ameelezea yale mafanikio ambayo nchi yetu inaangaliwa na nchi zingine na inavyopimwa, sasa tukisema kwamba hatuna mchango mzuri kama Serikali, Mawaziri hawa hawachangii chochote kidogo inashangaza! Siyo kutetea kwamba kule ambako kuna udhaifu vilevile ni vizuri ukashughuliwa kwa nafasi ile inayokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, mwisho kwa kumalizia, Bunge hili katika majukumu yale tuliyonayo ile Ibara ya 63, mojawapo ni kutunga sheria. Kwa hiyo, ninaomba sana mijadala yote tunayoitoa humu ambayo imekwenda kinyume na sheria zetu wenyewe tulizotunga, unaposema mtu anyongwe na unajua Bunge hili halijatunga sheria ya kunyonga mtu kwa makosa ambayo yapo humu. Nafikiri iwe ni uamsho kwamba tujitahidi sana kuelewa mipaka ya sheria zetu, inatoa nini. Vilevile kuangalia namna ambavyo tutatekeleza majukumu ambayo tunayo, kila muhimili ukitekeleza majukumu yake ili mwisho wa siku wananchi ambao tunawatumikia basi waweze kunufaika na utumishi wetu. Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (no. 2) Act, 2022
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kushukuru tena kwa kunipatia fursa hii kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.2 wa Mwaka 2022.

Mheshimiwa Spika, tumepata jumla wa Waheshimiwa Wabunge 11 ambao wamechangia Muswada hapa na Waheshimiwa hawa ni pamoja na Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama, Mheshimiwa Yahaya Massare, Mheshimiwa Luhaga Mpina, Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mheshimiwa Salome Makamba, Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani, Mheshimiwa Zainabu Katimba, Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mheshimiwa Ng'wasi Kaman, Mheshimiwa Abdallah Ally Mwinyi na Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete kwa sababu mimi ni Wakili namba moja sasa kwa seniority ya Wanasheria katika kazi zetu mara nyingi Senior Counsel anakuwa na mwingine ambaye anakuwa pembeni kwake. Nikutoe wasiwasi Ridhiwani Kikwete pamoja na nyadhifa nyingine yeye ni wakili ambaye amesajiliwa kwa namba 1582. Nilisema vile vile chochote tunachofanya hapa kama Serikali tunafanya vilevile succession plan kuhakikisha tunawajengea uwezo wote ambao wanafanya kazi kwa niaba ya Serikali kuwatumikia wananchi.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri, tumepokea maoni mazuri sana ambayo yamelenga kuboresha sio Muswada tu bali ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni ushahidi tosha kabisa kwamba suala ambalo limekuwa mbele yetu ni suala ambalo lilihitaji sisi kama Serikali kuwasilisha Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, niishukuru sana Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, nafikiri kwa jinsi ambavyo wewe mwenyewe umeshuhudia michango yao bora lakini vile vile na ufafanuzi walioutoa kulinda integrity ya Kamati yao imeonesha jinsi ambavyo Serikali na wao tulipata muda wa kutosha kujadili Muswada huo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo yapo mambo kadha wa kadha ambayo yametolewa yale ya ushauri, kwa ufupi tu niseme kwamba, yote kama Serikali tumeyapokea kwa sababu lengo la Serikali siku zote ni kuhakikisha kwamba tuna mifumo mizuri zaidi ya sheria na tuna sheria ambazo ni bora kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanalindwa na sheria, lakini vile vile wanakuwa na fursa nzuri ya kushiriki katika shughuli zao za kimaisha na kiuchumi. Nchi yetu inafuata vile vile utawala wa sheria.

Mheshimiwa Spika, nigusie baadhi ya mambo kadhaa lakini nikishukuru sana maelezo ya utangulizi ambayo Mheshimiwa Kikwete ameyatoa.

Nitapenda nieleze kwa dhana za kisheria na mustakabali wa nchi yetu hasa kuhusu vyombo vinavyosimamia sheria. Kuja na Muswada huu hakukuwa na maana ya kuonesha kwamba vyombo vingine vya kisheria havitekeleza majukumu yake vizuri, kama kuna dosari zinapimwa kuligana na utekelezaji ndani ya sheria zinazowahusu. Kwa hiyo tumekuja na Miswada hii, kwa mfano, Muswada ambao unahusu udhibiti wa dawa za kulevya.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Dawa za Kulevya ni Mamlaka iliyoanzishwa na Serikali, iliyoanzishwa na sheria na inatekeleza majukumu yake kwa kujitegemea. Kwa hiyo, kwa nini kuna dhana ya wao kuwa na mahabusu, sheria imetumia neno may lakini sheria hii hii imetumia maneno kwa kushirikiana na vyombo vingine. Vile vile mahabusu hizi zikianzishwa Waziri mwenye dhamana lazima atahakikisha viwango vyake. Mheshimiwa Simbachawene alieleza kwa undani kueleza mazingira ya kipekee ambayo yanahitajika, ambayo mazingira hayo hayapatikani kwenye Vituo vyetu vya Polisi vya kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ni kwa minajili hii basi, ieleweke kwamba mahabusu zitakazoanzishwa kwa mujibu wa Sheria lazima zianzishwe kwa kuzingatia vile vigezo vyote. Vigezo vya mahabusu zetu ziwe za Polisi, viwe vilivyopo kwenye Magereza yetu maana yake zinajengwa kwa kuhakikisha zimezingatia yale mahitaji ya ujazo, ile nafasi kwa watu wangapi na yale mahitaji ya msingi kwa binadamu ambayo lazima yawepo. Sasa ni kwa msingi kama huu ilielezwa vizuri shida inayokuwepo kwa hawa ndugu zetu wanaoangukia kwenye biashara hii ya usafirishaji wa dawa za kulevya.

Mheshimiwa Spika, anapofanyiwa vile vipimo akapimwa na akajulikana kwa mfano ndani ya tumbo lake amebeba dawa za kulevya labda kete kadhaa utaratibu wa kuzitotoa unaendana na ujazaji wa fomu na hazitotolewi kwa wakati mmoja. Kwa hiyo mkiangalia zile sheria ndio maana kuna zile observation fomu na kuna mashahidi na kadhalika. Mahitaji ambayo ni vigumu sana kama tunafuata ile misingi ya haki za binadamu na faragha za binadamu, kuipata kwenye lockup zetu za kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine tuelewe kwamba kutokuwepo kwa lockup za Polisi mahala fulani kusizuie mamlaka kufanya kazi zake. Kwa hiyo ndio maana ya kusema kwamba pale mahitaji yanapohitajika lockup hizo zitaanzishwa na neno lililotumika ni may. Kingine ambacho ningependa vile vile kwa mashirikiano yaliyopo kisheria lockup zile kama hazina mahabusu wa dawa za kulevya haitakuwa kizuizi kwa taratibu za vyombo vyetu kutumika vilevile kwa wahalifu wengine waliokamatwa kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Mheshimiwa Mpina nikutoe wasiwasi kwa sababu hatua ya mtu kuingia mahabusu sio kitendo cha kukurupuka, lazima afike kitu kinachohusika kwa maana ya mamlaka, Mamlaka imkamate mtu, baadaye kuna lockup register ambayo mtu atasajiliwa, baadaye kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete, Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka yalipoongezwa mwaka 2008 ya kukagua mahali popote wanapozuiliwa wahalifu maana yake ni kwamba kuhakikisha kwamba nchi yetu inazingatia haki za binadamu kwa mtu ambaye hajatiwa hatiani kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo hili ningependa wote ambao walikuwa na mashaka hii, basi wajue kwamba zikitumika vinginevyo kutakuwa na changamoto nyingine.

Mheshimiwa Spika, kingine ni ile dhana kufikishwa mahakamani kwa hawa watu kutafuta sheria zetu na sheria hii imetambua hilo, ndio maana kifungu cha 32 cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai ambacho kimetambuliwa kisheria kwenye hii sheria Sura 95 kinasema mtu aliyekamatwa atafikishwa mahakamani as soon as is practicable, maana yake mapema kadri inavyowezekana.

Mheshimiwa Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Makamba ameeleza mfano wa nchi kadhaa ambazo zina utaratibu huu. Kwa hiyo jambo hili niliona niwatoe wasiwasi wote ambao huenda walikuwa na wasiwasi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kwa ujumla Sheria ile ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu, mwanzoni kufungwa haikuwa sharti la lazima, kwa hiyo tulichokifanya Serikali imeona baada ya tafiti na baada ya kuangalia mikataba ambayo Serikali imeridhia, sasa ni kuona kwamba angalau kuwe na kifungo kama adhabu ya lazima na zaidi yake sasa pale ambapo kuna sababu za nyongeza, basi kunakuwa na faini.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kama tumefuatilia Muswada na Jedwali letu mtaona kwa mfano chini ya kifungu cha nne kifungu ambacho zamani kilikuwa cha hiyari ilikuwa option miaka miwili hadi kumi sasa ni lazima, miaka 20 hadi 30, kwa maneno mengine isiyopungua 20 na isiyozidi 30. Kifungu kidogo cha 5(3) zamani ilikuwa mwaka mmoja hadi miaka saba lakini ilikuwa ni option kwa sasa ni mandatory, si chini ya miaka mitano na isizidi miaka 10. Kwa wale waliokuwa wanasema adhabu ya maisha kifungu cha 5(4) zamani ilikuwa miaka isiyopungua 10 hadi 20 kwa hiyari, lakini sasa ni lazima, miaka isiyopungua 30. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sheria inaposema isiyopungua 30 maana yake Mahakama kwa kuzingatia mazingira ya shauri husika inaweza ikapandisha kutoka 30 na kwenda juu ime-set minimum. Kwa hiyo hili nafikiri ni jambo ambalo ningesema kwamba kwa sasa ambacho kitafuatia ni kuona jinsi ambavyo tunasimamia sheria hii ili kuleta mabadiliko.

Mheshimiwa Spika, hoja ya kuona tunafanya nini sisi kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sheria yetu hii na mamlaka yetu hii na Mamlaka ya Zanzibar tumepokea ushauri na nafikiri ni jambo ambalo litaendelea kufanyiwa kazi. Hata kwenye Kamati tuliwaahidi kwamba, jambo hili tutaendea kulitolea taarifa.

Mheshimiwa Spika, suala la hoja ya bangi, mirungi kama sheria haiharamishi sheria zetu zinaharamisha vifungu kuanzia cha 12-15 cha sheria mama tunayoijadili imeongelea jinsi inavyoharamisha makosa haya. Kwa hiyo mjadala unaoendelea sasa hivi na sio Tanzania tu ni je, twende zaidi ya kifungu chetu cha 13. Kifungu cha 13 hata sasa kwa matumizi mahsusi mtu anaweza akaomba kibali kwa Commissioner General na akaruhusiwa kuwa na kiasi cha dawa hizi kwa matumizi ambayo maana yake yamerasimishwa na sheria, lakini kuingia kwenye commercial au demand kubwa na kadhalika hapana, haya yameharamishwa na sheria hii na mengineyo yatakayofuata.

Mheshimiwa Spika, tumepokea ushauri kuanzia wa Kamati na wa Bunge hili la kufanya utafiti mkubwa ili tuone jinsi ambavyo nafikiri baadaye nchi yetu itafanya maamuzi kwanza kuhusiana na mikataba ya Kimataifa ambayo sisi tumejifunga nayo, lakini baadaye kuja kuona tunafanya nini na sheria zetu. Kwa hiyo hili nalo ningependa Waheshimiwa Wabunge wasione kwamba ni jambo ambalo halitafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa ufupi nishukuru sana na nizidi kuomba tu kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama ilivyo ada kazi yetu mojawapo kati ya kazi nyingine ni kuhakikisha tuna sheria zenye tija na tutaomba sana tuendelee kupokea maoni hata baada ya hapa kwa sababu ndio kazi yetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia katika Muswada huu na kushiriki na wale wengine ambao kwa njia moja au nyingine wameufuatilia, sasa naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Katiba na Sheria
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuendelea kuhudumu kwa nafasi ambazo amependa tuendelee kuwemo humu kuwahudumia Watanzania. Nimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mahsusi kwa leo kwa jinsi ambavyo anasimamia utawala wa sheria na utawala bora. Pia nikushukuru sana wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika, Wenyeviti na uongozi wote wa Bunge kwa kuhakikisha kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatimiza wajibu wake kwa Katiba na kwa mujibu wa kanuni ambazo zipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria, Naibu Waziri, Mawaziri wengine waliopo hapa pamoja na watendaji wote Serikalini. Nimshukuru Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na viongozi wote ambao kwa upande wa Serikali wanahakikisha kwamba haki inatendeka kwa mujibu wa Katiba. Aidha, niishukuru Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge pamoja na Kamati ya Bajeti ambazo nimekuwa nikifanya nazo kazi kwa jinsi ambavyo zimekuwa zikichakata mambo mbalimbali na kuhakikisha kwamba Bunge lako pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi yangu na wengine, zinatekeleza wajibu wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sitatenda haki nisipoishukuru sana Ofisi yangu kwa kuanza na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Watumishi wote kwa jinsi ambavyo wao kama sehemu ya Wizara ambayo inaratibu mashauri yote kwa mujibu wa instrument ya Wizara wanasaidia kuhakikisha kwamba shughuli hizi zinaendelea na kwa shukrani niwashukuru sana Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, utakumbuka nilitoa dakika 15 za mwanzo kabla ya Bunge kuanza na dakika 15 baada ya Bunge kuahirishwa, kuingia Bungeni kusikiliza Wabunge walio na kero zao ambao huenda wanahitaji kuongea na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mwakilishi wa Ofisi kuu ya Utumishi wa Umma upande wa Sheria. Niwashukuru wengi wamekuwa wakiniona na nimeendelea kutimiza wajibu wangu kwa kufanya nao kazi kwa karibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika hoja na michango iliyowasilishwa katika Bunge hili na Wabunge wachangiaji ambao wote tunawashukuru sana, labda kiasi nichangie hili, kuna hoja imetolewa na Mheshimiwa Luhaga Mpina kuhusiana na usiri wa mikataba.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mpina ameeleza kwamba ana maelezo mengi zaidi ya yale ambayo ameyasema hapa na nashawishika na kumwomba hata Waziri wangu wa Katiba na Sheria, yawezekana tunahitaji kukaa naye na kujifunza mambo mengi sana ambayo huenda hayapati fursa ya kushughulikiwa kwenye michakato ya kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoongelea masuala ya mikataba, mikataba yote inayofuata sheria inaongozwa na sheria na kwa ushiriki wa Bunge hili Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, wote mnajua kabisa kwamba Bunge hili kwa Mujibu wa Ibara 63(2) na (3) ninao wajibu mahsusi kwa mambo yanayohusu mikataba. Wajibu wa kwanza ni ule wa mikataba ambayo inatakiwa kuridhiwa na Bunge hili ambayo ni kwa mujibu wa Ibara 63(3)(e). Sijaona kama kuna lalamiko kwamba kuna mikataba ya kuletwa hapa haijaletwa. Kwa hiyo mchango wangu ni kwamba Ofisi yangu itaendelea kuhakikisha kwa wajibu wake kwamba Mikataba ya kuletwa kuwasilishwa Bungeni hapa kuridhiwa na Bunge hili itaridhiwa na Bunge kwa kufuata matakwa ya Katiba na Sheria zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa wajibu wa Bunge kusimamia Serikali niamini kwamba Kamati za Bunge hili Tukufu ambazo zipo zinasimamia Wizara na kila Sekta ya Serikali na zinao wajibu kutembelea maeneo miradi iliko ambapo naamini kazi zinazoendelea kule ni pamoja na kufuata matakwa ya mikataba iliko. Kwa hiyo niamini kwamba Bunge hili na Kamati zake vile vile itaendelea kuhakikisha kwamba zile Kamati zinapewa fursa ya kuwianisha miradi iliyopo na mikataba inayohusika na naelewa katika mwaka wa kazi kuna kikao mahsusi ambacho kama sikosei ni kikao cha mwezi wa Tisa ambapo Serikali huwa inakuja na shughuli za Serikali Bungeni, lakini kikao kinachofuata ambacho ni cha mwezi wa Kumi na Moja ni Kamati za Bunge kuja kufanya mawasilisho ya shughuli ambazo zimeangalia utendaji wa kazi za Serikali.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hilo naamini kwamba kama zile Kamati za Bunge zinazosimamia maeneo ya utendaji wa Serikali kuliko na mikataba hiyo zimenyimwa fursa ya kujua mikataba hiyo ina nini, ukiachilia ile ya kuleta hapa Bungeni, basi tupo tayari kama Serikali kupokea hoja kama kuna ukiukwaji huo kuushughulikia, lakini kwa mapendekezo ya Mikataba, ni wajibu wetu kuendelea kujenga uwezo kama Serikali kuhakikisha kwamba tunao uwezo wa kufanya majadiliano na kama mnavyofahamu ile Kamati ya Serikali inayoshughulika na mradi wa LNG jana ilikuwa kwenye ziara mojawapo. Serikali haipo tupu sana kwa maana ya wataalam, lakini wajibu wetu ni kuendelea kuhakikisha kwamba Serikali yetu inao uwezo wa kutosha kuhakikisha kwamba kadri kunapokuwa na uwekezaji mkubwa basi wataalam wetu wote kutoka sekta mbalimbali wanahusishwa pamoja na kushughulika kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, lakini faraja yangu mara nyingi wanapenda kudadisi, Bungeni humu kuna Wanasheria zaidi ya 30 na hawa wote nimeshawakaribisha kuwa sehemu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mambo yote ambayo wataona wanahitaji maboresho, wote tunaijua tasnia ya sheria sio maneno matupu. Tasnia ya sheria inaongozwa na uhalisia na baadaye uhalisia kutokana na mambo yanayoibuka, basi wote tunakuwa na ile collective responsibility na hata kuona maeneo yapi ambayo yanahitaji kuboresha sheria zetu.

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa muda ulionipatia na naunga mkono hoja ya Waziri wa Katiba na Sheria. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Katiba na Sheria
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kushukuru sana kwa nafasi hii, pia nishukuru na kuwapongeza wakuu wa mihimili yetu ya dola, Mheshimiwa Rais, Spika wa Bunge letu pia Mheshimiwa Jaji Mkuu kwa kusimamia misingi ya demokrasia, haki na utawala bora. Niwapongeze sana Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati, Waheshimiwa Mawaziri na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda huu pia nitumie kuwapongeza sana Waheshimiwa Wabunge, ambao wamepata fursa kuchangia hoja, kujibu au kuongelea maeneo ambayo yamefanyiwa wasilisho na Waziri wetu wa Katiba na Sheria ambaye amefanya kazi kubwa sana kwa kushirikiana na Mheshimiwa Naibu Waziri na watendaji ndani ya Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo hoja kadhaa ambazo zimeibuliwa katika michango hiyo zikiwemo sheria zetu kupitwa na wakati. Katika hili ningeomba tu kuwaomba Waheshimiwa Wabunge, Watanzania wote na watumiaji wote wa sheria, kwa sasa sheria zote ambazo tungependa zitumike ni zile zilizokwishakufanyiwa rekebu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuingizwa kwenye tovuti ya Office of the Attorney General Management of Information System, ambako ukiingia tu unafikia online law catalogue.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hizi tumeendelea kuzitangaza kadri tunavyofanya urekebu, na itakapofika mwezi wa sita mwaka huu ningependa kutoa taarifa kwamba Serikali yetu tutatoa toleo la sheria zilizorekebiwa la mwaka 2023, ambako sheria zote kuu 446 zitakuwepo. Ni tendo la kuipongeza Serikali yetu kwa sababu toleo hili linakuja baada ya miaka 20 kupita. Toleo la mwisho la urekebu tulilonalo ni lile la 2002, na tena ambalo Serikali yetu ilipata ufadhili. Kwa hiyo ningependa kuipongeza sana Wizara ya Katiba na Sheria na Serikali yetu kwa ujumla na Bunge hili kwa kuidhinisha fedha ambazo zimewezesha kazi hiyo kubwa sana kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kazi kubwa sasa ambayo tunaendelea nayo pamoja kwa kukamilisha urekebu ni ile ya kufanya tafasiri ya sheria kuu pamoja na sheria ndogo. Tayari tumekwishakuvuka asilimia 50, na katika zile sheria ndogo 29,700 tayari sheria ndogo 211 nazo tumesharekebu. Kwa hiyo fedha iliiyoombwa na Mheshimiwa Waziri wetu ni pamoja na mambo mengine itasukuma sana kufanya hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine vilevile tunashukuru sana maelekezo ya kiti kwa maana ya Mheshimiwa Spika, ambayo yameendana sanjari sana maelekezo ya Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria na nina kila sababu ya kumpongeza. Matumizi ya Law Reform Commission, Tume yetu ya Kurekebisha Sheria, kwa sasa Serikali imekwishakuamua kwamba, Tume hii itemize wajibu wake wa msingi wa kufanya utafiti kabla ya sheria hazijaletwa humu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua kila mmoja akisimama anasema Bunge liletewe sheria, kwa hiyo kuletewa kwa sheria nyingi tunazotamani ziletwe humu iendane na uwezeshaji mkubwa ambao tunatamani sana ufanyike kwenye Tume yetu ili iweze kutuhakikishia inafanya utafiti kwa kushirikiana na wadau wote na kutuwezesha katika hilo. Kwa hiyo Mheshimiwa Massare nikuhakikishie tu kwamba kwa sheria zile zilizokwishakufanyiwa urekebu makosa yale ya ukinzani yamekwishakufanyiwa kazi. Pia nikuhakikishie kwamba kwa maelekezo ya Mheshimiwa Waziri wa Serikali sheria zote zitakazofanyiwa utafiti zikaendelea kutokuwa na makosa mengi sana ya kiufundi au kiuchapishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja pia imewasilishwa kuhusu wananchi ambao wanashinda kesi lakini wanakuwa hawajapata haki yao. Mheshimiwa Mpina ameongelea hili. Ningependa tu kueleza kwamba kwa sheria zetu zinazoongoza mienendo ya madai ni Civil Procedure Act ambako Order XI inaongelea habari ya Executions. Kwa Sheria ya Jinai (Criminal Procedure Act) Kifungu cha 353 kinaongelea namna ya kurejeshwa kwa mali iliyokamatwa kwa mtu aliyekwishakushinda kesi mpaka hatua ya mwisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa baada ya kumaliza nafuu zilizo kwenye sheria, kwa mfano kifungu cha 353, basi yule aliyeshinda na kama hajapata haki yake kuna namna ya kuwawajibisha watu wanaotatiza haki hiyo kufanyika kwa mujibu wa sheria na kama ilivyochangiwa vizuri sana na Mheshimiwa Tadayo wakati anatoa mchango wake hapa. Kwa hiyo labda, kwa sababu tuna dhamana ya kuwajibika kwa mujibu wa kazi tulizokwisha kupewa, nafikiri Mheshimiwa Mpina nitaomba kuendelea kati ya Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zetu kuona kikwazo ni kipi. Kama ni upungufu wa legal aid kwa wale wanaohusika basi ninaamini wajibu wetu ni kukwamua na kuhakikisha kwamba watu wanaohusika wanaendelea kupata haki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengine kama ambavyo Mheshimiwa Waziri amekwishawasilisha kwenye hotuba yake, ofisi yangu kupitia idara zake hasa uandishi wa sheria, itaendelea kutimiza yale ambayo tayari yamewekwa humo. Pia tuendelee kuwaahidi kwamba tutaendelea kuhakikisha kwamba, kile ambacho tumekuwa tukikifanya hata kwa Mbunge mmoja mmoja anapotuletea hoja, tutaendelea kutoa majibu ya haraka na tutaendelea vilevile kufanya kazi kwa karibu sana na Wizara ya Katiba na Sheria; na kwa mambo yote yanayohusu mikataba. Nafikiri hili ni jambo ambalo tutaendelea kulitolea maelezo kadiri ya mikataba inavyojadiliwa, inavyohitimishwa ikiendana na mashauri ambayo yako kwenye mahakama za ndani na za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukichelea wakati mwingine kuongelea kesi iliyomalizika hatua moja lakini bado inaendelea kwenye hatua zingine au kwenye majadiliano mengine ambayo bado yanaendelea kwa mujibu wa sheria. Hoja ya mwisho ya Mheshimiwa Mpina nafikiri alikuwa anaongelea standard charted; jambo hili bado kuna majadiliano ya Serikali yanayoendelea na wale walio na tuzo.

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na naunga mkono hoja na Waziri, nakupongeza sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa Bungeni kwenye Mkutano wa Kumi na Mkutano wa Kumi na Moja pamoja na Uchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Sheria Ndogo zilizowasilishwa Bungeni kwenye Mkutano wa Nane na Mkutano wa Tisa
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Kamati pamoja na wajumbe wake na wote waliobahatika kuchangia hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefurahi kusikia dosari ambazo zimetajwa hapa pamoja na maazimio. Baada ya kusikiliza yote jambo la kwanza ambalo ninapenda kukariri ni kwamba, ni kweli kwa mujibu wa mgawanyo wa madaraka ya vyombo vyetu mhimili kwa mujibu wa Ibara ya 4. Tunatambua kwamba mamlaka yote ya Serikali yanatoka kwa wananchi kwa mujibu wa Ibara ya 8.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge hili kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(d) ndiyo linalotunga sheria zetu. Pia tunatambua kuwa ustawi wa wananchi, msingi wake ni ule umewekwa kwenye Ibara ya 146 ambao madhumuni ya kuwepo kwa mamlaka zilizopo, zinazotunga sheria maana yake inafuata ule mlolongo ambao unafuata mamlaka zilizotajwa na mihimili.

Mheshimiwa Naibu Spika, yote ambayo yameelezwa hapa na dosari hizi tunatambua kwamba sheria mama zinapotungwa ndiyo zenye kutamka kuwa nani mwenye dhamana ya kutunga Sheria Ndogo na vilevile ni nani mwenye dhamana ya utekelezaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi kubwa imeendelea kufanyika na tunalipongeza sana Bunge hili kwa sababu, kila sheria zinapotungwa kati ya mambo ambayo yamekuwa yakinishughulisha Bunge hili na Waheshimiwa Wabunge ni pale ambapo kuna ugatuaji wa kutugwa kwa Sheria Ndogo au kanuni kufuata masharti ambayo yanakuwa yamezingatia Sheria Mama.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ilivyotolewa na tukiangalia hata kwa mtiririko wa miaka hii miwili. Kumekuwa na maendeleo makubwa ya kupungua kwa dosari mbalimbali. Pia tunatambua kuendelea kuwepo kwa dosari hizi lakini yapo mengi ambayo yanaendelea kufanyika ambayo tunaungana na Kamati kwamba dosari ambazo zimetajwa ni wajibu wetu kama Serikali kuhakikisha kuwa zinatatuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano Mheshimiwa Mpinga katika mchango wake ameeleza vizuri. Kwamba, tangu mwaka 1920 kanuni ya sheria ndogo ya 4151 zilifungwa lakini kwa sasa kwa zoezi linaloendelea ni kuhakikisha kwamba kuna zoezi la kuhuwisha pamoja na kubaki na zile Sheria Ndogo ambazo zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria mama 446 zilizopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kufanya hivyo kwa sasa sheria ndogo hai zilizopo kutoka hiyo 4151 zimebaki 25,000. Dosari ambazo zimekuwa zikitajwa hapa na hatua ambazo tumekuwa tukizichukua, tunatambua uwepo wa upungufu katika ngazi mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano mwaka jana tarehe 7 Novemba yalitoka maelekezo kwenda kwa watendaji Wakuu wa Halmashauri, Tawala za Mikoa na Watendaji Wakuu Serikalini, kulipo na upungufu wa wanasheria, kuhakikisha kwamba wanasheria waliopo kwenye ofisi zilizo jirani wanatumika kwenye mazoezi ili kuhakikisha kazi za kisheria zinatekelezwa kwa kufuata misingi ya Sheria Mama na matakwa mengine ya kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili limesaidia kuendelea kupunguza dosari ambazo zimekuwepo. Pia imeelezwa hapa, mafunzo na maelekezo mengine ya kiutendaji ambayo yanalenga kuboresha namna ya kuhakikisha sheria zetu zinakuwa hai na zinatekelezwa na kupunguza kero kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, natambua ingawa Mheshimiwa Mariam hajawahi kuongea na mimi, ni kweli. Lakini ninaamini kufikika kwangu na watendaji wa ofisi yangu kumechangia sana kuboresha changamoto mbalimbali zinazopatikana kuanzia ngazi za halmashauri na maeneo mengine ya kiutawala. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni wajibu wetu kuwajibika. Pia siku zote Mheshimiwa Chief Whip siku zote ameendelea kuratibu changamoto zinazopatikana na kuzisambaza kwa wadau wetu. Kwa hiyo, hizi ni hatua ambazo zitaendelea kuwa endelevu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nizidi kuomba katika hatua hii, nimeelewa kama nilivyo mimi na Waheshimiwa Wabunge kama nyinyi mlivyo na uhusika wenu kwenye mabaraza ya ngazi ya madiwani. Tuendelee kushirikiana wote kuhakikisha kwamba dosari hizi zilizosalia zinapungua kwa kuendelea kufanya kazi vizuri na Wakurugenzi, Wasimamizi wa Mamlaka katika ngazi mbalimbali na mamlaka nyingine kuhakikisha tunaendelea kuboresha mifumo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ipo mipango mingine mingi ambayo Serikali inaendelea kuifanya, maana Mheshimiwa Kenani ameuliza ofisi yetu tunafanya nini? Kwa sasa tumeendelea sana kuboresha ile division ya uandishi wa sheria. Maboresho ya sheria yanakuja ili iweze kuwa na mfumo ambao utawezesha kusimamia vizuri kazi za kisheria hasa kwenye eneo la uandishi, kutoka ngazi za chini hadi ngazi za juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii itaendana na kile ambacho Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria ameeleza, mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba Law Reform Commission na yenyewe inahusika kikamilifu kuhakikisha sheria zetu zinakuwa zinaongozwa na tafiti na zinakuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na haya yote sisi tutaendelea kuhuwisha sheria zetu na kufanya urekebu na kuhakikisha tunakuwa na sheria kwa lugha ya Kiswahili. Kama nilivyosema katika sheria mama 446 tayari sheria 258 tumeshazitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Sheria zote mpya zinazotungwa sasa zinatungwa kwa lugha ya Kiswahili ambayo nayo hii ni nyenzo muhimu sana kuwafanya wananchi wetu kuelewa hizi sheria na maana zake pamoja na madiwani wetu na watu wote wanaotumika katika mchakato wa kutugwa kwa Sheria Ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimalizie kwa kusema kwamba tunaipongeza sana Kamati pamoja na mapendekezo haya. Faraja yetu ni kwamba muda umetolewa kufikia Tarehe 2 Oktoba, basi hatua mbalimbali ziwe zimechukuliwa. Nitaendelea kufikika na nafikiri ambaye hajanifikia basi atakuwa yeye labda sababu zake. Kila mmoja hapa naamini katika kumbukumbu zangu sijawahi kufikiwa na mtu alafu nisimpatie jibu au nisimpatie huduma inayostahili. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nichukue fursa hii kukushukuru kwa nafasi ambayo umenipatia, nitumie fursa hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri lakini na Kamati yenye dhamana na Mambo ya Ulinzi na Nje na mawasilisho ambayo umewasilisha kwenye Bunge lako tukufu, ninaunga mkono mawasilisho ya Bajeti ya Wizara, lakini nina wiwa walau kuchangia kwa machache kama yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza kwa uelewa wangu Serikali yoyote makini hufanyia kazi mawazo na ushauri inaoupokea kutoka kwa wananchi wake na kupitia kwa wawakilishi wao, lakini pili Serikali yoyote makini huheshimu sana mgawanyo wa madaraka uliowekwa na Katiba yetu. Sasa ningependa kuheshimu sana mawazo ya wachangiaji wengi ambao wameyawasilisha, lakini pia hata mawazo ya wasomi wenzangu wanasheria na nitagusia hili la ushiriki wa Tanzania katika Mahakama ya Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kumbukumbu zetu ziwe sahihi kwamba Tanzania ni nchi mojawapo muasisi wa Umoja wa Afrika lakini ni mwanachama mwaminifu na hai, lakini pia nchi yetu bado ni mwanachama wa Mahakama ya Afrika na hata sasa Rais wa Mahakama hiyo ni Mtanzania. (Makofi)

Sasa inapokuja namna ya kupeleka migogoro kwenye mahakama hiyo utaratibu umewekwa na protocol zinazoiongoza Mahakama hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, protocol ya tano imeorodhesha namna ya kufika kwenye mahakama ile na kwenye Ibara ya 3 inatoa fursa kwa nchi mwanachama aliyeridhia anaweza akatoa tamko kwa asasi za kiraia yaani NGOs na watu binafsi pia kufikisha mashauri yao kwenye mahakama hiyo. Wote tunafahamu Tanzania kwa sasa iliondoa tamko lake kwa NGOs pamoja na watu binafsi kupeleka mashauri yao au migogoro kwenye mahakama hiyo, lakini hiyo haimaanishi kwamba migogoro mingine baki inayohusu Tanzania na watanzania kwa maana ya zile haki zilizotolewa na kipengele cha A – E kufikishwa kwenye mahakama hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, msingi mkubwa ni lazima tutambue kwamba kwa mujibu wa Katiba yetu Ibara ya 107A(2) (a) mpaka (e) imetaja ile misingi ambayo migogoro yetu inavyotatuliwa. La kwanza; kwa sababu nchi yetu kama nilivyosema inaoongozwa na Katiba, migogoro imepangwa migogoro ya aina ipi ipelekwe wapi na Katiba yetu pamoja na sheria zingine zote inasema kwamba kabla ya kupata nafuu nyingine au kutafuta nafuu nyingine mamlaka zingine za nje ni vizuri kupata nafuu za kisheria kwenye mamlaka ya utatuzi wa migogoro tuliyonayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kwa misingi hiyo kwa kuwa tumesema kwenye Katiba yetu Ibara hiyo ya 107 kwamba mahakama ndiyo chombo pekee, lakini kwenye Ibara ya 13(6) namna ambavyo mtu ana haki ya kupeleka shauri lake kwenye ngazi za mahakama na vyombo vingine vilivyopewa dhamana hiyo. Kwa hiyo, ni msingi wa sheria zetu kwamba wananchi na mtu yeyote anayetaka kutetea haki yake apeleke shauri kulingana na jinsi ambavyo zile sheria zilizopo zimeainisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni kwa mantiki hiyo kwa sasa tutaona kwamba yapo mpaka mashauri ya Kikatiba ambayo yanapalekwa kwenye Mahakama Kuu na yanashughulikiwa. Lakini kwa mujibu kwa mfano kwa Sheria ya Madai na Sheria ya Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai zimeanisha mashauri yapi yapelekwe wapi. Kwa hiyo, kitendo cha Serikali kuondoa lile tamko haimaanishi kwamba Serikali haina nia ya kurejesha haki ambayo kwa sasa hawapeleki, vilevile haimaanishi kwamba hao watu wanazuiwa kuleta mashauri yao kwenye mahakama hizi zingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ambalo tunawaasa wote ambao wanatafuta haki zao mahakamani; moja, ni kuzingatia mipaka ambayo tunayo na wote tunajua jinsi ambavyo hata hili Bunge lako tukufu lingependa sana migogoro ya Watanzania ishughulikiwe na mahakama kwanza ambazo zimewekwa kwa mujibu wa Katiba yetu na kwa sheria zingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ile migogoro ambayo inafikia ile hadhi ya kwenda mamlaka za nchi, mamlaka zingine kama Mahakama ya East Africa, Mahakama ya Afrika, ICC basi zitafuata kwa mujibu wa zile nyenzo zilizopo za Kikatiba zinaoongoza namna ya kufikisha mashauri kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri kipindi hiki ninaweza nikasema kwamba hakuna yoyote kati ya NGOs pamoja na watu/raia waliokwenda Mahakama ya Afrika ambao walijaribu kuleta mashauri kwenye mahakama za nchi hii na wakanyimwa fursa hiyo, na endapo ikitokea hivyo basi hilo ni jambo ambalo vilevile linaweza likatapata suluhisho ndani ya mamlaka ya sheria zetu tulizonazo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika,tunazo sheria kama nilivyosema kwa mfano, tuna Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu lakini tuna Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai kifungu cha 7 kinaeleza kila shauri lianzie kwenye ngazi ya chini. Ukienda kifungu cha 264 Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai imepanga mashauri yapi ya kwenda Mahakama ya Wilaya, ya Mkoa. Sheria ya Mahakama imeeleza mashauri ya kwenda Mahakama za Mwanzo, ukija kwenye mabaraza yetu yote yaliyotungwa vilevile yaliyoanzishwa kisheria yanaainisha migogoro hiyo iende wapi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa mantiki hii hata protocol ya tisa ya Mahakama hii ya Afrika kwa mfano inatambua kwamba shauri hata kama lingekuwa kule linaweza likaenda kwenye mashauri yaani kwenye amicable settlement na unaporudi kwenye Katiba yetu Ibara ya 107A(2) (d) utakuta inasisitiza namna ya kukuza usuluhishi. Kwa hiyo, haiji akilini kwa nini ukaanze kutafuta usuluhishi kwenye mahakama ya juu au ya nje ukiacha mamlaka iliyo ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, itoshe niseme tu kwamba ninashukuru, lakini tutaendelea kuheshimu nafikiri mawazo ya wananchi kupitia kwa wawakilishi wao na kuendelea kufanya kazi nao na kuona namna ambavyo kila mmoja ataendelea kupata haki zake kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (no. 6) Bill, 2021
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nichukue fursa hii kukushukuru sana tena kwa kunipa hii nafasi ya kufanya majumuisho ya mjadala huu wa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.6 ya mwaka 2021.

Mheshimiwa Spika, tunashukuru kwamba Muswada huu umepata jumla ya wachangiaji 10 ambao wamepata fursa kupitia kiti chako ambao ni Mheshimiwa Omari Kigua ambaye pia ni Makamu wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti; Mheshimiwa Joseph G. Kakunda, Mheshimiwa Vita Kawawa, Mheshimiwa Luhaga Mpina, Mheshimiwa Reuben Kwagilwa, Mheshimiwa Abbas Tarimba, Mheshimiwa Halima Mdee, Mheshimiwa Subira Mgalu, Mheshimiwa Njeza pamoja na Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni faraja kwamba wachangiaji wote wameunga mkono hoja na ningependa kujibu. Kulikuwa na hoja hasa iliyoletwa na Mheshimiwa Kakunda kuhusu ukomo wa kutumika kwa kifungu cha 7(3) niombe tu kujibu kwamba kwa mujibu wa masharti sasa kifungu hicho kilichoongezwa uhai wake na ukomo wake unaendana na mradi uliotajwa kwenye sheria hiyo. Kwa hiyo ndiyo maana ni mradi mahsusi umetajwa kwenye kifungu hicho na kifungu hicho hakitatumika kubeba mradi mwingine isipokuwa kwa masharti ya kifungu hiki.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ni ile iliyowasilishwa na Mheshimiwa Vita Kawawa ambaye yeye alikuwa anaongelea ni lini hasa mabadiliko haya yatatumika. Awali ya yote labda nieleze kwamba alieleza dhana ya kamati jinsi ilivyokuwa imewasilisha hoja kwenye bunge lililopita. Ningependa tu kusema kwamba baada ya Kamati ya Bajeti kufanya mawasilisho yake baadaye Bunge lilikaa kupitia kifungu kimoja baada ya kingine na mwisho lilihoji na ule Muswada ukapitishwa kuwa sheria.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, kifungu kile ni halali mpaka sasa kwa sababu kilipitishwa na Bunge hili kwa mujibu wa taratibu za utungaji wa sheria. Kwa hiyo sasa baada ya majadiliano haya nafikiri kuna hatua mbili zinakuja endapo Bunge litapitisha sasa mabadiliko yanayopendekezwa na baadaye Muswada huu kupitishwa kuwa Sheria kwa hatua zote na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali kwa mujibu wa sheria ya tafsiri ya Sheria Sura ya kwanza sheria hii itaanza kutumika mara tu baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

Mheshimiwa Spika, vinginevyo naomba tu nirudie kuwashukuru sana wote ambao wamechangia na wengine ambao hawakuchangia na kwa niaba ya Serikali niwahakikishie tu kwamba Serikali tutaendelea kupokea maoni na kutoa ufafanuzi wa maeneo mengine mtambuka kwa sababu ndiyo wajibu wetu kuhakikisha kwamba sheria zinazopitishwa na Bunge hili zinafikia malengo yake.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Halima Mdee awe na amani tu, baada ya miezi minne kupita baadaye yamekuja mabadiliko haya, kwa kuwa yamekuja kwa kufuata zile taratibu za kisheria na ni kwa manufaa ya Watanzania na Wabunge kama tunavyojua kwa mujibu wa Katiba ni wawakilishi wa wananchi, kwa hiyo sheria inayotarajiwa nafikiri itawasaidia wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo sasa niruhusu niombe kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2023
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kukushukuru kwa kunipatia tena fursa hii. Namshukuru pia Mwenyekiti wa Kamati na jumla ya wachangiaji ambao wamepata fursa ya kuchangia, ukimjumuisha Mwenyekiti na Wabunge wengine watano.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri wa Kisekta, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Biashara, na Wizara ya Elimu. Kwa sababu, kama tunavyofahamu katika utendaji kazi wa Serikali, kila Waziri ana majukumu anayopangiwa kwa hati maalum, na kila Waziri ana wajibu wa kuhakikisha sheria tulizonazo zinakuwa hai na zinatimiza malengo yake. Kwa hiyo, nawashukuru kwa sababu wao na taasisi zao ndiyo waliibua maeneo ambayo yameonekana kwenye Muswada huu ambao ulikuwa na sehemu ambazo zimejadiliwa.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa ushirikiano ambao tuliupata kwa Kamati ya Bunge. Ninawiwa kulisema hili, labda niliseme kwa muktadha ufuatao: -

Mheshimiwa Spika, unatolewa wito wa kuendelea kutoa elimu zaidi katika maeneo haya. Sisi kama Serikali tunao wajibu, na Wizara zote ziko tayari kuendelea kushirikiana na Bunge kutoa elimu kwenye maeneo yote ambayo yanaibuka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zaidi ya haya na yanayoendelea nje, na kwa uzoefu wangu, nafikiri vile vile umefika wakati hata taratibu za Bunge nazo, itolewe elimu ili hata wananchi ambao mara nyingi wamekuwa kila mmoja anasema kwa sauti ya mwananchi, kwa niaba ya mwananchi, wajaribu kuelewa jinsi Bunge linavyofanya kazi. Kwa sababu, Serikali inapokuja na Muswada kama tulivyokuja hivi, ukaungwa mkono, maana yake kazi kubwa imefanyika ngazi ya Kamati. Kwenye Kamati sisi ambao tunawajibika kule, tumekuwa tunaona kabisa Kamati zinavyowajibika kwa wananchi waliowachagua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni kwa mantiki hii mchakato wa Mbunge anavyopatikana kuanzia wakati wa Kura za Maoni, baadaye akachaguliwa na wananchi, baadaye asipingwe kwa utaratibu wa kisheria, akawepo humu na asiwajibishwe kwa kanuni za humu, maana yake wanahitaji pongezi na kupewa heshima yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namalizia kwa kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge. Ninaahidi tu kwamba, maeneo yote tuliyoyaleta, ukweli ilikuwa ni kuhuisha na kuhakikisha kwamba sheria zetu zinatimiza yale mahitaji ambayo jamii yetu na Tanzania yetu imefika leo na inakoelekea. Kwa hiyo, kama Serikali, tunaahidi kuendelea kutekeleza sheria hii ambayo sasa baada ya michango iliyotolewa, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, naomba kutoa hoja kwamba Bunge hili lipendezwe sasa kuingia kwenye hatua inayofuata.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2021
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kukushukuru sana tena kwa kunipatia nafasi ya kufanya majumuisho ya Muswada na mjadala ambao umeendelea hapa kuhusu marekebisho ya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya Mwaka, 2021.

Mheshimiwa Spika, tumepata jumla ya wachangiaji kumi ambao kwa kibali chako naomba niwatambue kwa kuanza na Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, pia, Mheshimiwa Joseph Mhagama, Mheshimiwa Edward Olelekaita, Mheshimiwa Noah Lemburis Ole-Seputu, Mheshimiwa Salome Wycliffe Makamba, Mheshimiwa Joseph Tadayo, Mheshimiwa Yahaya Massare, Mheshimiwa Khadija Taya, Mheshimiwa Geophrey Pinda (Naibu Waziri wa Katiba na Sheria) na wa mwisho ni Mheshimiwa Pauline Gekul, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri. Tumepokea maoni mazuri ambayo yanalenga kuboresha sio Muswada tu bali hata masharti mengine ya Sheria mama. Kwa ujumla maoni na ushauri uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge ni Ushahidi kwamba suala la Marekebisho ya Sheria kwa lengo la kuboresha utekelezaji Madhubuti wa Sheria zilizopo, linamhusu kila mmoja wetu katika Bunge hili na ni jambo ambalo ni endelevu. Ndio maana kila mwaka Serikali inakuja na Miswada ya aina hii ili kuboresha masharti ya Sheria zetu na kuzifanya ziende na wakati.

Mheshimiwa Spika, katika michango iliyotolewa Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Najma Giga, yeye amesisitiza suala la elimu, jambo ambalo hata sisi tunaliona kuwa ni jambo la msingi. Serikali tunalichukua na linahitaji kuwa endelevu. Kwa hiyo, alipokuwa anaongelea kwa mfano kile kifungu cha 4 ambacho kinahusu kuzuia matumizi mabaya ya makosa ya madai kwenda ya jinai au makosa ya kiutawala kuainishwa kama ya jinai. Nafikiri Serikali inapochukua dhamana ya kuhakikisha kwamba elimu inatolewa hii itasaidia kwa sababu itahusu vile vile mamlaka; kwa mfano, zile za waajiri ambazo zimekuwa hazichukui zile hatua za kinidhamu na mashtaka ya kiutumishi na kukimbilia mahakamani. Au makosa madogo madogo ya jinai kupokelewa kwenye vituo vya polisi.

Mheshimiwa Spika, wengi wameongelea sana juu ya hiki kifungu cha 91 ambacho bila shaka kikisomwa na kile cha 131A sasa ni dhahiri kama ambavyo wengi wamesema ni mabadiliko makubwa ambayo pia yataendelea kuhitaji Serikali iendelee kuhakikisha kwamba maafisa wanatekeleza na kusimamia utolewaji wa haki jinai wanatimiza wajibu wao. Kwa sababu mabadiliko haya yanatoa hakikisho kwamba endapo shauri litaondolewa kwa hati ya kuondolewa mahakamani, basi kama linarudi wakati huo lifike na kuombewa usikilizaji wa awali na kuendelea kusikilizwa mfululizo. Endapo ikitokea hata yule mshtakiwa ameachiwa lakini asirudishwe mahakamani siku siku hiyo, akirudishwa basi hapo hapo shauri lile lianze kusikilizwa ukiondoa yale makosa makubwa yaliyoainishwa kwenye kifungu cha 131(a).

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na vile vile ushauri au maoni kuhusiana na Ibara ya 63 kuhusiana na kifungu cha
297. Serikali inapokea ushauri na itafanyia kazi marekebisho haya.

Mheshimiwa Spika, jambo ambalo vilevile limejitokeza kwenye michango ni lile ambalo la kutaka vile vyombo vinavyohusika kuhakikisha sasa vinapata bajeti ya kutosha au kuwekeza katika kujenga zile stadi zao. Kwa hiyo tunaamini kwamba kwenye jambo hili Waheshimiwa Wabunge watakuwa ni wadau muhimu kwa sababu bajeti itakapoletwa moja ya mambo ambayo italenga ni maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, vilevile, pamoja na yote yatakayoendelea ni jitihada za Serikali sasa hasa katika usimamizi wa utoaji wa haki kuendelea kuwa na mwelekeo wa kuwadhibiti watoa taarifa waongo, zile taarifa za kupika, ambazo mara nyingi nazo zilikuwa zinachangia sana kuwepo kwa mashauri mengi kufunguliwa halafu matokeo yake yanakuwa hayana mantiki.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Penal Code kutoa taarifa ya uongo kwa afisa mwenye dhamana ni kosa la jinai. Kwa hiyo, nafikiri mabadiliko haya hayataishia hapa lakini yataenda kuhakikisha kwamba ile substantive justice (haki ya msingi) ipatikane. Palipo na tuhuma iripotiwe tuhuma, ifanyiwe kazi isipothibitika basi haitathibitika kwa mfumo ulio wa wazi zaidi.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na mchango wa Mheshimiwa Salome Makamba kuhusiana na kifungu cha 29. Amenishughulisha kweli kweli na nikapata hofu aliposema kile kifungu hakipo. Hata hivyo, naomba arejee kifungu cha 29(4) ndicho kinaendana na masharti haya. Kwa ridhaa yako kama tutaendelea kuwepo na sintofahamu kwa upande wa Mheshimiwa Mbunge nitakuwepo, nitabaki hapa aje nimpitishe kwenye Sheria hii na Sheria zinginezo ambazo zinaendana na maeneo ambayo alikuwa na mashaka kwamba huenda tumeleta kitu ambacho hakipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya nikushukuru sana wewe mwenyewe pamoja na kama nilivyosema kutupatia fursa hii kama Serikali, pia na dhamira njema ya Wabunge ambao wamepata fursa ya kuchangia, lakini hata wale ambao hawakuchangia.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nitoe kama rai na commitment ya ofisi yangu, ni kwamba Waheshimiwa Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wawe radhi kutembelea ofisi zetu kupata ufafanuzi na kupata miongozo yoyote inayohusiana na maeneo ambayo sisi tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba wao kama wawakilishi wa wananchi wanapata tafsiri sahihi, misimamo sahihi ya kisheria, lakini hata kutatua shida na kero za watu wao.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, sasa ninaomba kutoa hoja.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu wa Mwaka 2022
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Nami naungana na wachangia wengi. Kwanza namshukuru Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango kwa kuanzisha mchakato wa kuandaa Muswada ulio mbele yetu. Ni Muswada ambao mchakato wake nafikiri wengi wameeleze chimbuko lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niongee tu kwamba kwa Waheshimiwa Wabunge na hasa Wajumbe wa Kamati, tunawashukuru sana kwa majadiliano ambayo yaliendelea. Napenda tu kusema kwamba, kwa Mujibu wa Ibara ya 64(1) ni kazi ya Bunge hili kutunga sheria.

Kwa hiyo, mchakato wa kutungwa kwa sheria ni pamoja na kazi ambayo Wajumbe wa Kamati mlifanya. Mara nyingi inakuwa ni mazoea mabaya nafikiri kuwa na mwelekeo kwamba lazima Kamati fulani itofautiane na Serikali au kunuwia mahali fulani pachimbike. Kwa sababu dhamani hii ipo ndani ya Bunge hili pekee na siyo Bunge lingine. Kwa hiyo, tunawashukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti na Kamati yako na wote walioshiriki mwanzoni kabisa wakati mchakato huu umeanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda tu kutoa hofu kwa wale ambao wanaongelea juu ya kuongezwa kwa watoa taarifa wengine. Nitasema hivi, tulipokea sheria zetu hizi zinazoongoza mchakato wa mienendo ya makosa ya jinai katika nchi hii mwaka 1930 (Criminal Procedure Court). Tangu wakati huo wajibu wa mtu kutoa taarifa ya uhalifu au mpango wa uhalifu kutendeka uliwekwa kwa mwenye kufahamu; na kutokutoa taarifa ni kosa la jinai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mnaweza mkaona hii safari, tokea mwaka 1930 tukiwa chini ya Mkoloni Mwingereza, tumeendelea mpaka tukawa na sheria ya sasa. Kadri tulivyokwenda ni maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii, tukafika mahali ambapo kama ni makosa ya rushwa kwa mujibu wa kifungu cha 37 lazima itolewe taarifa TAKUKURU. Kama ni makosa ya kawaida, Kifungu cha 7 cha CPA yanatolewa Kituo cha Polisi au Uongozi wa Mtaa na Uongozi wa Mtaa ukipokea unapeleka Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makosa ya utakasishaji fedha, mfumo wake kwa sababu yanahitaji kuchakatwa na yanaanza na shuku, ndiyo maana sasa kifungu kikahitaji kwamba taarifa hizi zitolewe Financial Intelligence Unit. Ndiyo maana ya kuangalia ni watu wapi ambao wako kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutoa taarifa kutegemeana na shughuli zao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mantiki hii sasa ukianzia kule nyuma nafikiri sheria hii hata kabla ya mabadiliko yaliyo mbele yetu leo, mkiangalia report persons ni pamoja na cash dealers. Kwa nini hatukutaka registered cash dealers? Ni pamoja na banks and financial institutions. Kwa nini hatukutaka neno registered? Ni pamoja na customer officer, ni pamoja na Mawakili, Notary Republic na wengineo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kuongezeka kwa maneno hawa car dealers, ni maneno “car dealers” na pamoja na hawa wanashughulika na clearing and forwarding, cash reference bureaus. Ni wale ambao hata upande mwingine kama haukupeleka taarifa kwenye mfumo wa mabenki, ili mradi wakiona kuna taarifa ambazo ni vizuri kuzipeleka Financial Intelligence Unit wanakuwa na dhamana hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoa taarifa wote hawa, ukiondoa matumizi mabaya labda ya madaraka ya baadhi ya watendaji, ni watu ambao wana dhamana tu kwa shughuli zao kupeleka ile taarifa. Wao sio washukiwa na kazi ya Financial Intelligence Unit, ndiyo maana kazi yake kubwa ni kufanya analysis. Ikishamaliza kuchakata, baadaye kama kuna taarifa za kuendelea sasa kuingia hatua ya pili, taarifa zinapelekwa kwenye vyombo kuanza kufanya uchunguzi rasmi wa kijinai kwenye yale makosa ya utakasishaji wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni kwa nini kunakuwa na maongezeko haya? Inaendana na kukua kwa uchumi na maendeleo tuliyonayo. Orodha hii huongezeka na kupungua ndani ya Tanzania, Afrika na duniani kote kutegemea na maendeleo ambayo yatakuwepo. Ndipo hapo sasa Mheshimiwa Mdee tunaona kwa nini mabadiliko ya sheria, yanakuwa mengi. Yanakuwa ni mengi kwa sababu ya nini kinajiri na kinachotokea?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria hii ni kweli ilitungwa mwaka 2006 ikaanza kazi mwaka, 2007 Julai, lakini ikiwa Sheria ya Muungano. Mabadiliko ya kwanza yalikuwa ya kurekebisha dosari zilizojitokeza katika utendaji kazi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona nimepigiwa kengele, lakini kuna hoja ya Mheshimiwa Deo Mwanyika kuhusu kifungu cha 28B. Mheshimiwa Mwanyika nafikiri hupaswi kuwa na wasiwasi na wale watu, walioambiwa kwamba wanakuwa presumed mpaka wamejieleza. Sasa huku sio kule kushukiwa kwa kwenda mahakamani. Mara nyingi wao kwa nafasi yao wanatakiwa kudhibiti, kwa sababu wapo kwenye hizo Taasisi, lakini endapo hawakuhusika maana yake ni jukumu lao wao sasa kueleza walichukua hatua zipi za tahadhari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtakumbuka zipo kesi ambazo watu wengi hawajashtakiwa kwa sababu Financial Intelligence Unit inapofanya ile analysis, inakuta wahusika hakuna taarifa zingine ambazo zinakwenda upande mwingine. Vinginevyo, niseme Sheria za Ugaidi na Sheria hizi, Sheria ya Ugaidi tulianza mwaka 2002 ilipokuja mara ya kwanza hiyo dhana. Vilevile kama nilivyosema Sheria ya Utakatishaji imekuja mwaka 2006. Hazitumiki hivi hivi pamoja na hiyo Sheria ya Proceeds of Crime na tutofautishe sana, utekelezaji mbaya wa sheria unakuwa na sheria nzuri. Nafikiri wajibu wetu sasa ni kushughulika na wanaosimamia vibaya Sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa nimepigiwa kengele naomba niishie hapo. Ahsanteni, naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2022
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue fursa hii kukushukuru sana tena kwa kunipatia fursa ya kufanya majumuisho ya mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.3) wa Mwaka 2022.

Mheshimiwa Spika, tumepata faida ya kuwa na wachangiaji watano; Mheshimiwa Noah Lemburis Mollel, Mheshimiwa Yahaya Omari Massare, Mheshimiwa Agnesta Lambart Kaiza, Mheshimiwa Abdullah Ali Mwinyi na Mheshimiwa Dkt. Pindi Hazara Chana.

Mheshimiwa Spika, tunashukuru sana. Naomba nianze kwa kuishukuru sana Kamati yenye dhamana na Muswada huu. Nikiri tu kwamba tunapokuwa mbele ya Kamati, Serikali inawajibika kuliwezesha Bunge kuelewa maudhui na makusudio ya Sheria inayokusudiwa kutungwa au kurekebishwa. Kwa maoni yote ambayo yameletwa na Kamati kupitia kwa Mwenyekiti wake Dkt. Joseph Kizito Mhagama, Mbunge wa Madaba, yenye Wajumbe mahiri 23, tumeyapokea na tunawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Muswada huu ulikuwa na malengo; kusudio kubwa ilikuwa ni kuhuisha na kuongeza thamani ya sheria zilizotungwa na Bunge hili siku zilizopita kwenye vikao tofauti. Kwa hiyo, yote ambayo Wajumbe wa Kamati wamechangia ndio mambo ambayo yalijiri mbele ya Kamati. Tuliingia kwenye Kamati siyo kwa uelewano huu, lakini jedwali la Serikali linaonesha lengo la Serikali kuhakikisha inaleta Bungeni hapa Muswada unaokidhi matazamio na yale mambo yote mema ambayo Serikali yetu na Tanzania yetu inatamani yawe.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kaiza ameongelea suala la kima cha chini cha mtaji. Atakumbuka tulipokuwa mbele ya Kamati tulieleza vigezo ambavyo Benki Kuu inavitumia ili viendane na matakwa na viwango vya kimataifa kwamba ukiweka viwango bila kufuata zile standards leo, tunaweza tukajikuta uwekezaji wetu unaingia kwenye mkinzano na matakwa mengine. vilevile Serikali inaweza ikajikuta inashindwa hata kuwanyanyua hawa wawekezaji, hizo taasisi ndogo wanazozisema.

Mheshimiwa Spika, akumbuke lile kabrasha kubwa la vigezo, lakini hoja ninayoileta katika maelezo yangu ya kuhitimisha hapa ni kwamba, kanuni zinapotungwa na Waziri lazima zifuate sheria mama iliyopitishwa na Bunge. Vilevile tusiendeleze hiyo dhana kwamba Bunge halishiriki kwenye mchakato wa kuhakikisha kwamba tuna kanuni nzuri. Kanuni zinapoanza kuchakatwa kuna uhusishwaji ambao hufanyika na nafikiri ndio mwelekeo wetu wa Serikali sasa kwamba kila tukija na sheria na kanuni ziwe tayari.

Mheshimiwa Spika, pale tunapokwenda kinyume Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo na Kanuni inatukagua na kuzikagua sheria zetu. Kwa hiyo, ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba kanuni zitakazowekwa na Benki Kuu hazitakuwa kikwazo katika kuendeleza sekta na taasisi za kifedha. Kwa hiyo nimhakikishie tu Mheshimiwa Kaiza, nichukua dhamana ya Benki Kuu na Serikali kuwa wawazi kwa Kamati ya Bunge kuangalia kanuni zitakavyoweza kutungwa kwa sababu Serikali haina kitu cha kuficha, kwa sababu hata tukificha Kamati ya Sheria Ndogo itakuja kutuumbua hapa na mmeona kwa taarifa ya Mkutano uliopita tunaendelea na kiwango chetu cha kufuata masharti ya sheria mama kinaongezeka

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nishukuru sana Bunge lako kwa jinsi lilivyoshiriki kuiongoza Serikali na maboresho makubwa ambayo tunayaona. Kwa mfano, kwenye Muswada huu yapo maeneo ambayo moja kwa moja yanaonesha nia njema na kama njia ya kuhakikisha kwamba tunaenda sambamba na kufungua fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa marekebisho ya Sheria ya Malikale amesema hapa Mheshimiwa Pindi Chana, kama makumbusho ya mtu binafsi yalikuwa hayatambuliki Serikali sasa inafungua waratibiwe ili wakiratibiwa anapokuja mtalii labda anakwenda kwenye museum iliyokwishasajiliwa aoneshwe na zile za watu binafsi ili akiweza kuzifikia itaongeza kipato cha yule mtu lakini kutambulika kwao vilevile kutaiwezesha Serikali kuwajengea uwezo na elimu ya namna ya ku-handle.

Mheshimiwa Spika, yameelezwa mambo ya uchenjuaji, tumeyaweka vizuri kwenye sheria hii. Tusingejali hawa wachenjuaji wadogo kuwawekea utaratibu wa kisheria licha ya kupoteza mapato ya Serikali, lakini ni kama kuwatelekeza na kuweka milango ya wao kunyanyaswa.

Mheshimiwa Spika, eneo la local content tuliloliweka, nafikiri wote tunakubali si vizuri unakuwa na kampuni ya kigeni hapa ambayo ipo hapa kisheria na inafanya kazi zake kisheria, inunue mahitaji kama nyama, maziwa kutoka nchi nyingine wakati hivi vitu vinapatikana hapa. Kwa hiyo, Waheshimiwa wataona adhabu inayowekwa pale lengo ni kulenga hawa wote ambao wamepata leseni za kufanya kazi, basi jamii inayozunguka nayo ineemeke kupitia uwepo wao.

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kuishukuru sana Kamati, kuwashukuru Wabunge wote, lakini vilevile nikushukuru wewe mwenyewe, bila kuacha kushukuru na naendelea kusema kwamba uthubutu unaofanywa na hawa wenyeviti wa kamati waendelee kufanya hivyohivyo.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Spika, kwa upande Serikali tutaendelea kwenda na watu wote ambao wanatakiwa kutoa ufafanuzi ili Kamati zetu zipate yote.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, sasa naomba uniruhusu nitoe hoja, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naafiki.
The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2023
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nasimama mbele yako na Bunge hili Tukufu kwa mara nyingine nikishukuru sana, napenda nitambue na kuheshimu sana michango ambayo Waheshimiwa Wabunge wamewasilisha hapa wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kimsingi yalioelezwa na kuchangiwa na Waheshimiwa Wabunge ambao wamepata fursa ya kutoa mawazo yao ndio uwasilishaji halisi wa maana ya uharaka na mahitaji ya Muswada tuliowasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu. Kwa sababu kwa upande wetu Serikali bila kuwasilisha Muswada huu ni kweli wote tunajua kwamba sasa tupo Mwezi wa Tisa, quarter ya kwanza (robo ya kwanza) ya mwaka wa fedha imekwishamalizika lakini kwa Taasisi kama EPZA wameshindwa kufanya kikao cha Bodi hata kimoja kwa sababu ya hayo marekebisho ambayo tumewasilisha leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kwa hayo yote ambayo yamejadiliwa na maudhui ya Muswada huu, kingine ambacho niombe tu kuwaeleza Waheshimiwa Wabunge ni kwamba, kwa kuenzi maboresho makubwa ambayo Serikali inayafanya kwa maelekezo fasaha ya Mheshimiwa Rais, wote tunajua baada ya kuwepo kwa Plan Commission, kwa sasa kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha kwamba ile Tume ya Mipango inaleta tija ambayo inategemewa kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa haya mawazo ambayo kwa nini Katibu Mkuu hayumo, nafikiri Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo ametoa ufafanuzi. Pia, niwahakikishie tu hawa Waheshimiwa Wabunge ambao wamepata fursa ya kuongelea jambo hilo niwaeleze tu kwamba, safari tuliyonayo ni ndefu. Baada ya TIC kuhamishiwa Ofisi ya Rais, Uwekezaji; baada ya TR kuhamishiwa Ofisi ya Rais, Uwekezaji, kwa hiyo sasa na hizi EPZA na mambo yote ambayo yatawezesha Plan Commission, kwa sasa composition ilivyo, wote tunajua kabisa yupo yule Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango kama mmoja wa Wajumbe kwenye Tume hii, ambaye yeye kwa vyovyote uhusika wake ni wa maeneo yote na kuhakikisha kwamba inawezeshwa ile Tume na Wizara husika kutekeleza yale na Waziri mwenye dhamana sasa kuwajibika ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo maboresho yoyote ambayo yataendelea kuwasilishwa katika Bunge hili tukufu, naamini yataendelea kujenga zaidi mifumo yetu ya kuhakikisha kwamba suala la uwekezaji nchini linawekewa misingi imara ya kisheria, lakini ya kitaasisi na mazingira rafiki zaidi ya kuhakikisha kwamba Tume hiyo na Wizara iliyopewa dhamana inaleta mabadiliko makubwa tofauti na ambavyo kulikuwa na changamoto zilizokuwa zinakwamisha hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa Bunge lako lifikirie haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima na taadhima naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2023
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima kubwa na kwa taadhima nichukue fursa hii kwa mara nyingine nikushukuru sana wewe mwenyewe kwa jinsi ambavyo umetoa fursa ya Muswada wa Serikali wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali kujadiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sana wachangiaji sita kwa kuanza na Kamati yetu ambayo imewakilishwa hapa na Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, lakini pia Waheshimiwa Wabunge Selemani Zedi, Mheshimiwa Nusrat, Mheshimiwa Bryceson Magessa, Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki na Mheshimiwa Nape Moses Nnauye.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumefarijika jinsi ambavyo tuliushughulikia mchakato wa Muswada huu. Hatua tuliyofikia ilikuwa na majadiliano ya kina na wadau wetu kabla ya kuandaliwa kwa Muswada, lakini pia mashauriano ya kina na Kamati. Kwa hiyo jedwali la marekebisho ambalo limewasilishwa limeonesha jinsi ambavyo kulikuwa na ushiriki ambao ulituleta pamoja kati ya Bunge lako Tukufu kupitia Kamati, lakini na sisi upande wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mfano wa maboresho na maendeleo makubwa ambayo tumekuwa nayo katika namna ya kutunga sheria zetu. Sheria ya Huduma za Habari ni mojawapo ya enao ambalo nchi yetu tumepiga hatua kubwa. Tukiangalia tangu itungwe 2016 ni Sheria ambayo ililenga kufanya huduma hizi za habari sasa kuwa za kitaaluma.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili linadhihirishwa kwenye Sheria hiyo tuna Bodi ambayo Mwenyekiti wake wala siyo hatoki Serikalini. Majukumu yale ni makubwa, lakini vilevile tuna Baraza ambalo linahusisha Wanahabari wenyewe. Sasa ni nadra sana kupata hii, kwa hiyo nampongeza sana Mheshimiwa Rais, lakini pia nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Waziri ameeleza mwenyewe ambavyo amekuwa na vikao vingi na Wanahabari na kuwa na maeneo 21 ni jinsi ambavyo yameshughulikiwa. Pia kwa sababu naelewa ushiriki wa Viongozi, Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Wanahabari, nina kila sababu ya kupongeza viongozi wawe kutoka kwenye Bodi lakini na kwenye Baraza lao.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo machache ambayo yameongelewa hapa mojawapo nafikiri ni hili la leseni. La kwanza ningependa tu kumbukumbu zikae sahihi. Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana amelieleza vizuri, ni jambo ambalo linaendelea kujadiliwa kule. Hata hivyo, suala la leseni kwa wanataaluma huwa lina lengo la kuimarisha tasnia husika na kuifanya itende kazi zake kwa weledi na ndio maana Baraza la Wanahabari, kazi yake moja ni kuangalia mambo ya maudhui na wala halina ubaguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ukiangalia tuna Wanasheria wa kujitegemea ambao ni Wanachama wa TLS, wana Majengo, Wana Ofisi zao, wana Maktaba za thamani, lakini kila mwaka wanahuisha leseni zao. Sasa na wala hatuwezi tukajificha hata kwenye mwamvuli wa kimataifa kwa sababu mimi mwenyewe kwa mfano ni mjumbe kwenye International Prosecutors’ Association kwa miaka 15 na kila mwaka nahuisha uanachama wangu. Ni mjumbe kwenye Common Wealth Magistrate and Judges’ Association ambako ninahuisha uanachama wangu kila mwaka na kulipa zile ada. Kwa hiyo jambo hili ningependa nilieleze kwamba litaendelea kujadiliwa kwa kupitia majukwaa yale.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunapokuja kwenye suala la adhabu ya juu au ya chini, ningependa tu kueleza kwamba tumepiga hatua kubwa, kwa sababu kwa makosa kwa mfano yale yanayohusiana na kazi zao, kabla ya mabadiliko haya, kwa mfano kima cha chini cha adhabu kama ni ya fine ilikuwa ni milioni tanolakini cha juu ilikuwa milioni 20. Sasa kwenye kifungu cha 50 tunaporekebisha kinashuka kuwa milioni tatu kwa fine kwenda milioni 10, lakini kama ni jela kabla ya sasa ilikuwa miaka mitatu mpaka mitano, sasa ni miaka miwili mpaka mitano lakini kuna mahali kwa mfano tumetoka miaka mitano mpaka mwaka mmoja. Sasa lengo lake ni lipi?

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo lake ni kutambua kwamba wanataaluma wowote wana fursa ya kujirekebisha na kukua. Kwa hiyo nitapenda sana watakapopitia lile Jedwali la Sheria yenyewe, nafikiri watapata fursa ya kuona kwamba heshima ipi na wamezingatiwaje katika mambo ambayo yapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tujue wigo wa adhabu zote zilizowekwa ukitoa one third remission ambayo ni automatic chini ya Sheria ya Magereza, lakini vifungu vyote au adhabu hizi zinaangukia vilevile kwenye vifungo vya nje kwa yule ambaye atatimiza Sheria ile ya Community Service, Sheria ya Parole na kadhalika. Kwa hiyo, niombe sana Wanahabari kupitia mamlaka yao wendelee kushirikiana na Serikali

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko yaliyo kwenye Sheria ya Reli yakisomwa pamoja na maboresho mengine ya Sheria ya PPP, Sheria ya Uwekezaji, nafikiri ni kipindi cha kujitathmini kama Taifa na kuona namna ya watu kutumia fursa zilizopo sasa kwenye uwekezaji kupitia sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, niendelee tu kusema kwamba, kazi ya Ofisi yangu, kazi ya Bunge hili ni kuhakikisha tuna sheria nzuri na jambo ambalo siku zote tutaendelea ni sisi kufanya kazi kwa kushirikiana na Bunge na Kamati zake na Wabunge wote na wananchi wote. Mengine tuendelee kuwatakia heri na tumtakie heri Mheshimiwa Spika katika mbio za uchaguzi ujao. Ujumbe wangu ni mmoja tu, siyo yeye ni nchi na kwa kuwa ni nchi, ni lazima tumuunge mkono kwa gharama yoyote na jambo liwe la kheri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, sasa naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2023
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima kubwa na kwa taadhima nichukue fursa hii kwa mara nyingine nikushukuru sana wewe mwenyewe kwa jinsi ambavyo umetoa fursa ya Muswada wa Serikali wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali kujadiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sana wachangiaji sita kwa kuanza na Kamati yetu ambayo imewakilishwa hapa na Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, lakini pia Waheshimiwa Wabunge Selemani Zedi, Mheshimiwa Nusrat, Mheshimiwa Bryceson Magessa, Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki na Mheshimiwa Nape Moses Nnauye.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumefarijika jinsi ambavyo tuliushughulikia mchakato wa Muswada huu. Hatua tuliyofikia ilikuwa na majadiliano ya kina na wadau wetu kabla ya kuandaliwa kwa Muswada, lakini pia mashauriano ya kina na Kamati. Kwa hiyo jedwali la marekebisho ambalo limewasilishwa limeonesha jinsi ambavyo kulikuwa na ushiriki ambao ulituleta pamoja kati ya Bunge lako Tukufu kupitia Kamati, lakini na sisi upande wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mfano wa maboresho na maendeleo makubwa ambayo tumekuwa nayo katika namna ya kutunga sheria zetu. Sheria ya Huduma za Habari ni mojawapo ya enao ambalo nchi yetu tumepiga hatua kubwa. Tukiangalia tangu itungwe 2016 ni Sheria ambayo ililenga kufanya huduma hizi za habari sasa kuwa za kitaaluma.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili linadhihirishwa kwenye Sheria hiyo tuna Bodi ambayo Mwenyekiti wake wala siyo hatoki Serikalini. Majukumu yale ni makubwa, lakini vilevile tuna Baraza ambalo linahusisha Wanahabari wenyewe. Sasa ni nadra sana kupata hii, kwa hiyo nampongeza sana Mheshimiwa Rais, lakini pia nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Waziri ameeleza mwenyewe ambavyo amekuwa na vikao vingi na Wanahabari na kuwa na maeneo 21 ni jinsi ambavyo yameshughulikiwa. Pia kwa sababu naelewa ushiriki wa Viongozi, Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Wanahabari, nina kila sababu ya kupongeza viongozi wawe kutoka kwenye Bodi lakini na kwenye Baraza lao.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo machache ambayo yameongelewa hapa mojawapo nafikiri ni hili la leseni. La kwanza ningependa tu kumbukumbu zikae sahihi. Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana amelieleza vizuri, ni jambo ambalo linaendelea kujadiliwa kule. Hata hivyo, suala la leseni kwa wanataaluma huwa lina lengo la kuimarisha tasnia husika na kuifanya itende kazi zake kwa weledi na ndio maana Baraza la Wanahabari, kazi yake moja ni kuangalia mambo ya maudhui na wala halina ubaguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ukiangalia tuna Wanasheria wa kujitegemea ambao ni Wanachama wa TLS, wana Majengo, Wana Ofisi zao, wana Maktaba za thamani, lakini kila mwaka wanahuisha leseni zao. Sasa na wala hatuwezi tukajificha hata kwenye mwamvuli wa kimataifa kwa sababu mimi mwenyewe kwa mfano ni mjumbe kwenye International Prosecutors’ Association kwa miaka 15 na kila mwaka nahuisha uanachama wangu. Ni mjumbe kwenye Common Wealth Magistrate and Judges’ Association ambako ninahuisha uanachama wangu kila mwaka na kulipa zile ada. Kwa hiyo jambo hili ningependa nilieleze kwamba litaendelea kujadiliwa kwa kupitia majukwaa yale.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunapokuja kwenye suala la adhabu ya juu au ya chini, ningependa tu kueleza kwamba tumepiga hatua kubwa, kwa sababu kwa makosa kwa mfano yale yanayohusiana na kazi zao, kabla ya mabadiliko haya, kwa mfano kima cha chini cha adhabu kama ni ya fine ilikuwa ni milioni tanolakini cha juu ilikuwa milioni 20. Sasa kwenye kifungu cha 50 tunaporekebisha kinashuka kuwa milioni tatu kwa fine kwenda milioni 10, lakini kama ni jela kabla ya sasa ilikuwa miaka mitatu mpaka mitano, sasa ni miaka miwili mpaka mitano lakini kuna mahali kwa mfano tumetoka miaka mitano mpaka mwaka mmoja. Sasa lengo lake ni lipi?

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo lake ni kutambua kwamba wanataaluma wowote wana fursa ya kujirekebisha na kukua. Kwa hiyo nitapenda sana watakapopitia lile Jedwali la Sheria yenyewe, nafikiri watapata fursa ya kuona kwamba heshima ipi na wamezingatiwaje katika mambo ambayo yapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tujue wigo wa adhabu zote zilizowekwa ukitoa one third remission ambayo ni automatic chini ya Sheria ya Magereza, lakini vifungu vyote au adhabu hizi zinaangukia vilevile kwenye vifungo vya nje kwa yule ambaye atatimiza Sheria ile ya Community Service, Sheria ya Parole na kadhalika. Kwa hiyo, niombe sana Wanahabari kupitia mamlaka yao wendelee kushirikiana na Serikali

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko yaliyo kwenye Sheria ya Reli yakisomwa pamoja na maboresho mengine ya Sheria ya PPP, Sheria ya Uwekezaji, nafikiri ni kipindi cha kujitathmini kama Taifa na kuona namna ya watu kutumia fursa zilizopo sasa kwenye uwekezaji kupitia sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, niendelee tu kusema kwamba, kazi ya Ofisi yangu, kazi ya Bunge hili ni kuhakikisha tuna sheria nzuri na jambo ambalo siku zote tutaendelea ni sisi kufanya kazi kwa kushirikiana na Bunge na Kamati zake na Wabunge wote na wananchi wote. Mengine tuendelee kuwatakia heri na tumtakie heri Mheshimiwa Spika katika mbio za uchaguzi ujao. Ujumbe wangu ni mmoja tu, siyo yeye ni nchi na kwa kuwa ni nchi, ni lazima tumuunge mkono kwa gharama yoyote na jambo liwe la kheri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, sasa naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.