United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
OFISI ya Bunge imepokea msaada wa vifaa vya zahanati. Msaada huo ulitolewa Mjini Dodoma jana kutoka Kampuni ya Jaffery Ind. Sainiz Funiture na kupokelewa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Akikabidhi
msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Vishal Singh Saini alisema Kampuni hiyo ilipewa zabuni ya
kutengeneza samani mbalimbali za
Bunge na kwamba baada ya kumaliza kazi hiyo ikaamua kutoa sehemu ya mapato waliyoyapata kutoa msaada huo.
Alivitaja
vifaa vilivyotolewa kwamba ni vitanda viwili vya kulaza
wagonjwa,
pazia la kijani, stendi ya kutundikia dripu za wagonjwa na kabati dogo la wodini.
Mbali
na kutoa msaada huo, Kampuni hiyo pia ilitumia nafasi hiyo
kuonyesha
samani mbalimbali zinazotengenezwa na Kamapuni hiyo.
Kwa
upande wake Naibu Spika mbali na kushukuru kwa msaada huo lakini pia aliipongeza kwa kutengeneza samani zenye ubora
ikiwemo madawati.
Aliitaka
Kampuni hiyo kuangalia uwezekano wa kupunguza bei za samani zao ikiwemo kwa madawati hasa kwa wale ambao
watahitaji kununua samani
hizo kwa
wingi.
Aidha,
alizihamasisha taasisi mbalimbali ikiwemo wananchi mmojammoja kununua samani za ndani ili kulinda viwanda vya ndani
na kutoa ajira kwa Watanzania.
Awali
Mbunge wa Iringa Mjini, Mh. Peter Msigwa akizungumza katika hafla hiyo alIitaka
bei ya
madawati ipunguzwe ili wabunge waweze kununua na kusaidia maeneo yao yenye upungufu.