Parliament of Tanzania

Bunge kufanya Kikao maalum cha kumuaga Marehemu Sitta

BUNGE kesho litafanya Kikao Maalum cha Bunge kwa ajili ya kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa, Mheshimiwa Samuel Sitta.

Akizungumzia kikao hicho Bungeni leo, Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema kikao hicho ni cha kihistoria na kwamba hakijawahi kutokea katika historia ya nchi.

Alisema mwili huo unataraijiwa kupokelewa na baadhi ya wabunge katika uwanja wa Ndege Mjini Dodoma majira ya saa 8 mchana na kuletwa Bungeni ambapo utaingizwa ndani ya Ukumbi wa Bunge.

“Wabunge mtapata nafsi ya kutoa salamu za rambirambi na baadaye kutakuwa na utaratibu maalum wa kutoa heshima za mwisho ambao tutaongozwa na Waziri Mkuu na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,” alisema.

Alisema kutokana na muda kuwa mchache hakutakuwa na zoezi la kuuga mwili mmoja mmoja na kwamba utaratibu uliondaliwa utaonyesha heshima kubwa kwa Spika huyo mstaafu.

“Tutajenga msingi mzuri ambao viongozi wetu wa kitaifa wakipatwa na jambo la namna hii watapata heshima hizo sio tu katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam au mahali popote lakini kwa kuletwa Bungeni ambapo ndio nyumba ya wananchi wote wa Tanzania ilipo,” alisema.

Mheshimiwa Spika alisema baada ya shughuli hiyo kukamilika mwili wa marehemu utasindikizwa hadi Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Urambo Mkoani Tabora kwenye mazishi yanayotarajiwa kufanyika keshokutwa.

Alisema Bunge litawakilishwa na wabunge kumi watakaochaguliwa kwa kuzingatia uwakilishi wa vyama wakiongozwa na yeye mwenyewe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama alitoa hoja ya kutengua Kanuni ili kikao hicho maalum cha kumuaga Marehemu Samuel Sitta kiweze kufanyika.

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's