Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Nancy Hassan Nyalusi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NANCY H. NYALUSI K.n.y. MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:- Je, lini Serikali italeta Muswada wa Sheria Bungeni ili kudhibiti ujazo wa lumbesa kwenye mazao?

Supplementary Question 1

MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Sheria imeweka wazi na inakataza lumbesa, lakini lumbesa bado inaendelea: Je, Serikali ina mkakati gani wa ziada kuhakikisha kwamba inakomesha ujazo wa lumbesa? (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli lumbesa ni jambo ambalo siyo la kisheria. Nitoe wito tu kwa wasimamizi wa hizi biashara za vijijini hasa maeneo hayo ambayo wananchi wanakiuka utaratibu, hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wale ambao wanaweka nje ya kipimo halisi na hasa kwenye mamlaka hizo za Halmashauri ambako Maafisa Biashara wanasimamia mazoezi haya.