Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 51 Industries and Trade Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara 674 2023-06-20

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. NANCY H. NYALUSI K.n.y. MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:-

Je, lini Serikali italeta Muswada wa Sheria Bungeni ili kudhibiti ujazo wa lumbesa kwenye mazao?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Vipimo, inasimamia vipimo katika ununuzi na uuzaji wa mazao kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Na. 340 mapitio ya 2002 na marekebisho yake ya mwaka 2018, kupitia The Weights and Measures Act (Amendment) Order, G.N. No. 725 of 2018, iliyorekebisha Sheria ya Vipimo kufuta majedwali ya 10, 11 na 12 na kuingiza jedwali jipya la 10 ambalo chini ya kifungu cha 2 (2) (b) cha Jedwali hilo, mazao ya mashambani yatafungashwa kwa uzito usiozidi kilogramu 100. Hivyo, lumbesa ni ufungashaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya kifungashio kwa uzito zaidi ya ule unaokubalika kisheria.