Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakuja na mpango wa ujenzi wa vizimba vya ufugaji wa samaki katika Ziwa Duluti?

Supplementary Question 1

MHE.JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri kutoka Serikalini lakini napenda kuuliza swali moja la ziada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya uvuvi inaonekana kama sasa hivi ina mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa nchi. Je, Serikali haioni sasa wakati umefika wa kujengwa mabwawa maeneo ya Malula na maene ya Majengo ambako kila mwaka mvua zinaleta mafuriko, yale maji yavunwe yajengwe mabwawa kwa ajili ya kufugia Samaki?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA UVUVI NA UFUGAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Kwanza nibampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kutambua mchango wa Uvuvi katika uchumi wetu na hata maoni ambayo Mheshimiwa Mbunge ameeleza hapa kwamba tuanze sasa kujenga mabwawa kwa ajili ya kuboresha sekta ya uvuvi ni sehemu ya mpango tulionao sasa hivi. Kwa hiyo, tunachokifanya sasa hivi ni kutafuta fedha ili kuhakikisha kwamba tunafika kwenye maeneo yote hususan maeneo ambayo hayana maji mengi kwa maana ya Maziwa na Bahari, ahsante sana.