Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zaynab Matitu Vulu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAINAB M. VULU (K.n.y MHE. ALLY S. UNGANDO) aliuliza:- Kuendana na kasi ya Mheshimiwa Rais kutaka kumaliza kabisa urasimu wa upatikanaji wa hati za kimila na hati za ardhi mpaka sasa bado ni tatizo kwa Wilaya ya Rufiji:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Afisa Ardhi Mteule? (b) Je, Serikali haioni kwamba ina kila sababu ya kupeleka vifaa vya kisasa vya kupima viwanja na mashamba?

Supplementary Question 1

MHE. ZAINAB M. VULU: Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante. Namshukuru pia Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Nina maswali mawili ya nyongeza:-
La kwanza, kufuatana na maelezo ya Wizara husika kwamba mashamba yasipimwe viwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba. Je, hawaoni kwamba wananchi watanyimwa haki zao kwa sababu mtu anapokuwa na mashamba yake ana ndugu zake, ana watoto wake, ana wake zake atataka awagawie maeneo ya kuweza kujiendeleza na kukwepa ujengaji holela katika miji yetu, Serikali haioni kwamba itamnyima haki huyo mhusika wa hilo shamba?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kutokana na tatizo la mgogoro wa mipaka kati ya Ikwiriri na Nyamwage kwa maana ya Kata ya Mbwara na ni wa muda mrefu. Je, Serikali haioni sasa ni wakati wa kuutatua mgogoro huo na kuwawezesha wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuweza kuwa na mji mdogo katika Jimbo la Rufiji? Naomba majibu na tuambiwe lini wananchi hao watatatuliwa mgogoro huo na kupewa majibu.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge kulingana na swali alilouliza kwamba mashamba yasipimwe, kutopimwa mashamba hayo kufanywa viwanja kutanyima haki ya watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuelewe kwamba tamko la Wizara lililotolewa ni kwa ajili ya faida na manufaa ya halmashauri zetu wenyewe kwa sababu watu wamekuwa wakitumia njia hiyo kujinufaisha katika kupima, kununua mashamba baadaye wanapima viwanja na wanaviuza katika bei kubwa sana, square meter moja inauzwa 20,000 na kuendelea na ni baadhi ya Wabunge pia wamelalamika katika hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa na wakati mwingine pia unaporuhusu hiyo, watu wanaanza kuanzisha miji ambayo haiko katika utaratibu wa mipango miji kulingana na mipango kabambe ambayo imewekwa katika maeneo hayo. Kwa hiyo, hatuwezi kuruhusu hilo liendelee, kama kazi hiyo itakuwa iko ndani ya mpango wa Halmashauri inaweza ikafanyika hivyo ,lakini suala kubwa hapa ni kwamba, halmashauri zetu zinaibiwa au Serikali inaibiwa na haipati pesa. Hakuna tatizo lolote la yeye kupeleka mpango wake halmashauri na halmashauri ikafanya kazi hiyo ya ugawaji viwanja na mapato ya Serikali yakaingia kuliko yeye kudanganya kwamba anataka shamba baadaye anapima na kupunja wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, kuhusu mgogoro wa Kijiji cha Ikwiriri na Nyamwage, samahani Mheshimiwa kama nitakuwa nimetaja vibaya. Nyamage?
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Nyamwage! Naomba niseme migogoro hii iko mingi kama ambavyo tumeelekeza sasa inakuwa ngumu sana kwenda leo, kwenda Ikwiriri, kesho unarudi unaitwa tena kulekule katika eneo lingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana tunafanya uratibishi kama Wizara kuweza kujua migogoro yote hii ili timu inapokwenda kufanya utatuzi wa mgogoro huu wa Ikwiriri ikatatue na migogoro mingine katika maeneo hayo badala ya kwenda mgogoro mmoja baada ya mwingine ambayo inagharimu Serikali pesa nyingi ya mtu kwenda na kurudi kwa hiyo tutafanya utatuzi huu katika migogoro yote kama jinsi ambavyo tutakuwa tumeikusanya ambavyo tumeleta kitabu na bado mnaendelea ku-update taarifa zilizoko humu.