Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwanakhamis Kassim Said

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Magomeni

Primary Question

MHE. MWANAKHAMIS KASSIM SAID aliuliza:- Je, kwa nini Jeshi la Polisi haliondoi zuio la kuwahudumia wananchi wanaokwenda kupata huduma kwenye vituo nje ya maeneo yao?

Supplementary Question 1

MHE. MWANAKHAMISI KASSIM SAID: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Kuna wananchi wanapata matatizo panapokuwa na kesi za jinai, lakini wanapokwenda baadhi ya vituo wanakuwa hawapati huduma hizi wanaambiwa pale hawahusiki, waende kituo kingine.

Je, Serikali iko tayari kukifuta kifungu hiki ili wananchi pale wanapopata matatizo wapate huduma? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, hatuna kifungu chochote cha kisheria kinachozuia mwananchi aliyebaini uwepo wa kosa la jinai kuzuiwa kuripoti kwenye Kituo chochote cha Polisi.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kuelekeza kwamba ikiwa itatokea raia au mwananchi anapewa majibu hayo na askari wetu yeyote, atoe taarifa kwa Mkuu wa Kituo au Ofisa Upelelezi wa Wilaya au Mkuu wa Polisi wa Wilaya.

Mheshimiwa Spika, kupitia Bunge lako tukufu nielekeze IGP atoe mwongozo kwa Makamanda wote wa Polisi wa Mikoa ili kama kuna udhaifu wa namna hii uelekezwe kwamba kuondolewe msingi wa kuzuia mwananchi kutoa taarifa kwenye Kituo chochote cha Polisi, nashukuru.