Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa Barabara ya Matala – Mwanhuzi – Lalago kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa kipande hiki kilichobaki ndio kinaunganisha mkoa wa simiyu na Mkoa wa Arusha na ni muhimu sana katika kufungua uchumi wa wananchi wa Karatu lakini wananchi wa Mkoa wa Arusha kwa ujumla wake.

Je, Serikali haioni umuhimu sasa kuanza ujenzi wa kipande hiki cha Karatu-Orudeani Matara hadi Lalago kwa kiwango cha lami?

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Swai, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii ya Karatu-Odoyani hadi Mataralalago kujengwa kwa kiwango cha lami. Serikali imekwisha fanya tayari upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, na sasa kazi iliyobaki ni kutafuta fedha ili barabara hii ijengwe.