Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwantum Dau Haji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza: - Je, lini Serikali itaongeza gari lingine la polisi wilaya ya Kusini Unguja kwani gari moja lililopo halikidhi mahitaji?

Supplementary Question 1

MHE. MWATUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kujibu maswali yangu yenye kina na ambayo mimi mwenyewe nimeyaelewa. Napenda kumuuliza swali langu hivi, je, ni lini sasa hizo milioni 15 ambazo zimekisiwa kwenda kununuliwa mapikipiki pamoja na hayo magari katika wilaya nyingine pamoja na Mikoa, lini sasa Serikali itapeleka pesa hizo ili zifanyike kununulia magari hayo? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwatum Dau Haji, Mbunge wa Viti Maalum, kama Ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, shilingi bilioni 15 sehemu ya fedha hiyo tayari imekwisha tolewa na gari hizo tayari zimekwishaagizwa. Tunatarajia mwezi Agosti, 2023 tuweze kupokea magari hayo utaratibu wa Serikali ambao tunanunua magari hayo kupitia GPSA. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba sehemu ya fedha hizo tayari zimeshatolewa na sehemu ya magari hayo yamekwishaagizwa na mara yatakapowasili basi tutaanza utaratibu wa kuyagawa katika wilaya kama ambavyo tumepanga.