Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Njalu Daudi Silanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Itilima

Primary Question

MHE. NJALU D. SILANGA K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Stendi na Soko la kisasa katika Mji wa Makambako?

Supplementary Question 1

MHE. NJALU D. SILANGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa niulize swali dogo la nyongeza. kwa kuwa Mji wa Makambako ni mji mkubwa unaokuwa kwa kasi na unaunganisha nchi ya Zambia na nchi jirani ya Congo. Ni utaratibu upi wa haraka utakaofanyika kuhakikisha hayo majibu ya Mheshimiwa Waziri yatakamilika kwa muda muafaka ili wananchi wa Makambako wapate huduma iliyo bora?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI): Mheshimiwa Spika, Mji wa Makambako upo katika Tier III katika mradi huu wa TACTIC. Tier One, ndiyo sasa wakandarasi wamepatikana, michakato imekamilika na wanakaribia kusaini mikataba ya kuanza kazi na wale wa Tier II design ya miradi ndiyo inafanyika hivi sasa tunavyozungumza, na tayari wale consultants wamepatikana. Hii Tier III ambayo Mji wa Makambako upo, nayo wanapatikana wataalam kwa ajili ya kuangalia Master Plan na feasibility study ya mji ule. Kwa hiyo, muda siyo mrefu mradi huu utaanza pale katika Mji wa Makambako.