Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 235 2023-05-05

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. NJALU D. SILANGA K.n.y. MHE. DEO K. SANGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Stendi na Soko la kisasa katika Mji wa Makambako?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makambako, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Mji wa Makambako ipo kwenye Mradi wa kupendezesha Majiji, Manispaa na Miji (Tanzania Cities Transformation Infrastructures and Competitiveness – TACTIC) ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia. Kupitia mradi huo, Mji wa Makambako utajengewa Stendi na Soko la Kisasa.