Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ramadhan Suleiman Ramadhan

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuajiri Askari wa Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba?

Supplementary Question 1

MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kutokana na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri kwenye swali langu la msingi nina swali moja la nyongeza.

Kwenye jibu lake la msingi amekiri kwamba upo uhaba wa Askari Polisi katika Mkoa wa Kusini. Je, ni ahadi gani ya Serikali kwamba watatoa kipaumbele kwenye hizo ajira 4,103 alizozitaja maalum kwa ajili ya Mkoa wa Kusini Pemba? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ramadhan Suleiman Ramadhan Mbunge wa Chakechake kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi ahadi yetu ni kwamba hawa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Polisi 4,103 watagawiwa maeneo yote yenye upungufu ikiwemo Mkoa wa Kusini Pemba. Kama tulivyokubaliana Mheshimiwa Ramadhan nitakwenda huko baada ya Bunge hili ili kuangalia pamoja na mambo mengine upungufu huo na kiwango kinachohitajika kusaidiwa. Ahsante sana. (Makofi)