Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza: - Je, Serikali haioni umuhimu wa kununua gari la utawala na gari la Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma?

Supplementary Question 1

MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimia Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi nyingine.

Mheshimiwa Spika, hospitali za Wilaya za Mkoa wa Ruvuma pamoja na vituo vyake vya afya vina changamoto kubwa ya magari ya kubebea wagonjwa, kutoka kwenye vituo vya afya kwenda kwenye hospitali za Wilaya au kwenda hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Serikali ina mpango gani wa kupeleka magari ya kubebea wagonjwa katika vituo hivi vya afya au hospitali zake za Wilaya Mkoa wa Ruvuma? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mhehsimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwamba anafuatilia vizuri sana masuala yanayoendelea kwenye Wilaya zao kwa kushirikiana na Wabunge.

Mheshimiwa Spika, unaona kwamba kuna magari ya kubebea wagonjwa zaidi ya 727 maana yake ni kwamba hakuna Wilaya ambayo itakosa gari. Tutashirikiana na wenzetu wa TAMISEMI kuyatizama yale maeneo specific yenye uhitaji maalum ambayo yanahitaji kupewa magari zaidi ya moja na nadhani eneo lake la Mkoa wa Rukwa ni mojawapo ya hiyo mikoa Lindi, Mtwara, Kigoma na sehemu zingine ili tuone ni namna gani tunatatua hilo tatizo kwa wakati ambao tumeusema hapa.