Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itazuia Mamba wanaoua watu na kujenga uzio wa nondo maeneo ambayo watu huchota maji Jimboni Buchosa?

Supplementary Question 1

MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni kweli Mamba wawili walikutwa wamekufa ziwani, si kwamba walivunwa kama ambavyo Mheshimiwa Waziri amesema, na kwa kuwa akina mama wananchi wa Buchosa bado wanaendelea kuliwa na Mamba mpaka sasa; swali la kwanza;

Je, Waziri anaweza kuchukua hatua kwa watumishi wake ambao nina uhakika kwamba wamemdanganya ili jambo hili lisitokee siku nyingine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; wananchi wa Buchose wanahitaji commitment ya Serikali ya kwamba ni lini sasa vizimba hivi vitajengwa ili kuokoa maisha yao wakati wanateka maji? Ahsante sana.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Eric James Shigongo Mbunge wa Jimbo la Buchosa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Erick Shigongo kwa kuendelea kufatilia eneo hili ambalo kumekuwa na changamoto ya wanyama wakali hususan mamba. Ni kweli alikuja na alimwona Mheshimiwa Waziri, lakini pia tulipeleka askari kule, wamekuwa wakifatilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikidhibitika kweli kwamba hawa askari wamedanganya kwamba hawakwenda na wale mamba wamekutwa wako pembeni wamekufa, hatua za kinidhamu na za kiutumishi ninamwelekeza Katibu Mkuu azichukue haraka mara moja; kama itathibitika tu kwamba hawa askari wamedanganya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la pili nimwahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii tumekuwa tukijenga vizimba vya mfano kuonyesha namna ambavyo hawa wanyama wanaweza wakadhibitiwa na wananchi wakaendelea na shughuli zao za kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwahidi tu kwamba tutapeleka wataalamu wataenda kujenga kizimba cha mfano ambacho kanda ya ziwa pia wataenda kujifunza pale. Lakini kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, ni kwamba kwa kuwa haya maeneo kwa asilimia kubwa yanamilikiwa na Serikali za Mitaa zikiwemo Halmashauri. Tunazielekeza Halmashauri ziweze kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vizimba ili kusaidia hawa wananchi waendelee na shughuli za kibinadamu, ahsante.

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itazuia Mamba wanaoua watu na kujenga uzio wa nondo maeneo ambayo watu huchota maji Jimboni Buchosa?

Supplementary Question 2

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Tangu mwaka 2019 mpaka sasa watu watatu wamethibitika kufa kwa sababu ya tembo kwenye kata za Mkomazi na kata za Mkumbara kule Korogwe Vijijini na sasa hivi tunapozungumza hali ya uharibifu wa mazao ni kubwa sana. Ni upi mkakati madhubuti wa Serikali kuhakikisha kwamba tunawasaidia wananchi wetu kudhibiti tembo na wanyama wengine wasiendelee kuathiri mazao lakini na maisha ya wananchi wetu? Nakushukuru.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Timotheo Mnzava Mbunge wa Korogwe Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali la yote nimpongeze Mheshimiwa Mbunge. Ni kweli wiki iliyopita tu tulikuwa tuna changamoto ya tembo ambao walivamia katika maeneo ya mashamba ya katani na mashamba ya mipunga, lakini tulipeleka askari.

Changamoto iliyopo ni kwamba wale askari walikuwa ni wachache. Lakini nimuahidi Mheshimiwa Mnzava wananchi wa Korogwe zoezi linalofuata sasa hivi ni kwamba tumeamua kutafuta askari wa ziada ambao tutakuwa tunawaajiri kwa muda ili kuongeza nguvu katika maeneo ambayo yana changamoto ya wanyama wakali ili hawa wananchi katika kipindi cha mwezi wa nne mpaka wa saba waweze kuvuna mazao yao bila tatizo. Hili naliweka ni commitment ya Serikali tunaenda kulitekeleza mara moja.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itazuia Mamba wanaoua watu na kujenga uzio wa nondo maeneo ambayo watu huchota maji Jimboni Buchosa?

Supplementary Question 3

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuulizwa swali la nyongeza.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuzuia simba na tembo wanaoharibu mazao pamoja na mifugo katika Kata ya Magugu pamoja na Vilima Vitatu Jimbo la Babati Vijijini pamoja na Jimbo la Kiteto? Ahsante.

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asia Halamga Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba katika Kijiji cha Magugu tulikuwa na changamoto ya simba ambayo sisi tuliiona ni changamoto ngeni sana kwa sababu tumezoea ni tembo, mamba na viboko; lakini tulipeleka askari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto tunayoipata ni kwamba hawa wenyeji baada ya kuonesha kwamba mipaka ya hifadhi inakuwa maeneo fulani wenyeji wanasogea karibu sana wanaweka mazizi kando kando ya hifadhi. Sasa Simba anapotoka cha kwanza anaona kitoweo kiko karibu, kwa hiyo ‘mimi niwaombe wananchi wanaoishi maeneo hayo kwamba tunapoweka kando kando ya hifadhi beacon hii unaweka zizi la ng’ombe hapa. Na hili limekuwa ni changamoto kubwa kwa sababu hao hao wanatega ikifika maeneo kadhaa basi anaingiza hata ng’ombe hifadhini anaweza wanapata chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niwaombe wafugaji, kwamba kuweka zizi kando kando ya hifadhi ni kuleta hatarishi ya wanyama wakali kusababisha kuliwa hii mifugo na wanyama hatarishi kama simba. Lakini tumeendelea kutoa ushirikiano na askari wataendelea kuwepo katika maeneo hayo ili kudhibiti simba wanaotamani kula mifugo.

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itazuia Mamba wanaoua watu na kujenga uzio wa nondo maeneo ambayo watu huchota maji Jimboni Buchosa?

Supplementary Question 4

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa. Kumekuwepo na ongezeko kubwa la kima, ngedere na nyani kwa vijiji vinavyopakana na Mlima Kilimanjaro na wanyama hawa wamekuwa wanasababisha uharibifu mkubwa sana wa mazao ikiwa ni pamoja na kula kuku na kusababisha umaskini.

Je, Serikali ina mpango gani kusaidia wananchi wetu kukabiliana na changamoto hii?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Moshi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna changamoto ya ngedere, nyani na kadhalika katika maeneo ya Mlima Kilimanjaro; lakini tumeanzisha utaratibu wa kugawa miti ambao tunatarajia kuanza ili kuwepo na upandaji wa miti katika maeneo ambayo tunaamini haya tukiweza kuyazuia na kuyahifadhi vizuri basi wanyama hawa wataweza kuishi maeneo salama zaidi kuliko ilivyo sasa ni kweupe zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa wakati huo huo tulishaahidi kwamba hawa ngedere tutatafuta namna ya kwenda kuwapunguza na kupeleka katika maeneo mengine ya hifadhi. Hilo nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutalitekeleza. Ahsante.

Name

Emmanuel Lekishon Shangai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Primary Question

MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itazuia Mamba wanaoua watu na kujenga uzio wa nondo maeneo ambayo watu huchota maji Jimboni Buchosa?

Supplementary Question 5

MHE. EMMANUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri swali; kwamba kwenye kata za Swaiti Sambao, Lweipiri na Ololosopan, tembo wamekuwa wakiharibu mazao pamoja na kuumiza wananchi.

Je, Serikali ina mkakati upi wa kuhakikisha kwamba wananchi wale wanafidiwa?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Emmanuel Shangai Mbunge wa Ngorongoro kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu mwanzo, kwamba sasa tuna mpango wa kuangalia namna ya kuwa na askari wa kutosha ili kipindi kile ambacho ni cha migogoro kati ya binadamu ya wanyama wakali, basi hawa askari waweze kuelekea katika maeneo hayo na kudhibiti hawa wanyama wakali. Ahsante.