Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali italipa fidia wananchi waliotwaliwa ardhi yao kwa ujenzi wa viwanda maeneo ya Liganga na Mchuchuma?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri yaliyotolewa na Serikali, ila nina swali moja dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imekuwa na dhamira ya kutengeneza ajira maeneo haya yenye uwekezaji kwa kutenga vitalu vya wachimbaji wadogo; na kwa kuwa katika eneo lile la Mkomangā€™ombe, eneo lote lenye makaa ya mawe limeshikiliwa na Serikali kupitia Wizara hii: Je, Serikali haioni haja ya kukaa na wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakiomba muda mrefu kugaiwa maeneo ya kuchimba makaa ya mawe ili nao waweze kutengeneza ajira?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zachariuz Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Zacharius kwa ufuatiliaji kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu katika Jimbolake la Ludewa. Ni kweli dhamira ya Serikali ni kuona sasa tunashirikisha wachimbaji wadogo katika maeneo yote au katika biashara zote ambazo zinafanyika kwenye maeneo husika.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, kwa sababu mradi huu ni mkubwa, kwa sasa bado tunakamilisha majadiliano na huyu mwekezaji mkubwa. Kwa hiyo, naamini atakapoanza kutekeleza na hao wengine wachimbaji wadogo nao naamini watashiriki katika kuhakikisha wanafaidika na uwepo wa mali asili au madini haya katika maeneo hayo ya ludewa.

Mheshimiwa Spika, tunalichukua hili kwa uzito wake ili kuhakikisha local content nayo inachukua nafasi yake.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.