Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amour Khamis Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbe

Primary Question

MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK aliuliza: - Je, Tanzania inapokea watalii wa aina ngapi kutoka nje na sekta hii inachangia kiasi gani katika Pato laTaifa kwa mwaka?

Supplementary Question 1

MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, ninashukuru majibu ya Mheshimiwa Waziri ila nina swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa, wapo watalii wanaokuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta matibabu na tunao waganga wa jadi ambao wanaweza kutibu COVID kama vile Mheshimiwa Shekilindi. Swali langu ni kwamba Serikali ina mpango gani kwanza kuwawezesha waganga wa jadi kama hawa wenye ujuzi wa hali ya juu na kuwatangaza pia ili Pato la Taifa liongezeke? Nakushukuru sana. (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nafikiri kama nimelisikia ni kwa namna gani tunaweza tukawasaidia waganga wa asili. Moja ni kwamba na kwa sababu kuna ushirikiano kweli na Wizara ya Maliasili kwa sababu baadhi ya vitu ambavyo vinatumika na watu wetu kama mizizi na vingine vipo kwenye maeneo ya maliasili.

Mheshimiwa Spika, kikubwa ni kwamba tunaanza kuiweka rasmi na kuna tafiti zinazofanyika kuthibitisha hivyo vitu ambavyo waganga wa asili lakini tunajenga ukaribu na Wizara ya Maliasili kwenda kwa pamoja ili tuweze kuwasaidia. (Makofi)