Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. MWANAKHAMIS KASSIM SAID aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatatua mgogoro wa ardhi kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzana na Wakazi wa Kijiji cha Dunga – Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mgogoro kama huo huko vilevile katika Jimbo la Kigamboni katika Kata ya Kimbiji eneo la Kijaka.

Je, ni lini Serikali itatatua mgogoro huo.

Name

Dr. Stergomena Lawrence Tax

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika ahsante sana. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Ndugulile kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana kwa kulifuatilia suala hili kwa karibu, kwa niaba ya wananchi wa Kigamboni na ninapenda kumfahamisha kwamba mgogoro huu tayari na wenyewe unashughulikiwa na upimaji ulishafanyika, kwa hiyo tunasubiri tupate hati na baada ya hapo hatua zinazofuata zitaendelea. (Makofi)