Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA K.n.y. MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga Hospitali ya Wilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa kuwa hospitali iliyopo ina hadhi ya kituo cha afya na haikidhi mahitaji?

Supplementary Question 1

MHE. LEAH J. KOMANYA. Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Kwa kuwa miundombinu iliyopo ni chakavu na ina hadhi ya kituo cha afya, Halmashauri ya Wilaya ya Meatu imetenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuanza miundombinu mipya.

Je, Serikali haioni haja ya kujenga miundombinu mipya inayokidhi hadhi ya Wilaya kwa kuwa hospitali hiyo ina eneo la hekari za ziada 17?

Mheshimiwa Spika, hospitali hii ina upungufu mkubwa wa watumishi kwenye eneo la wauguzi wenye degree na wenye weledi; mahitaji ni wauguzi 24 tuliye naye ni mmoja. Je, Serikali haioni haja ya kutuletea wauguzi wenye weledi ukizingatia tumejenga Jengo la ICU? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Jimbo la Meatu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuwapongeza Halmashauri ya Meatu kwa kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuendelea na ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Halmashauri ya Meatu, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imefanya tathmini nchini kote hospitali chakavu 50 ambazo zinaupungufu wa Miundombinu zimeanza kutengewa fedha shilingi bilioni 16.5 mwaka huu wa fedha, lakini hospitali 39 ikiwemo ya Meatu zinatengewa fedha kwa mwaka ujao wa fedha. Kwa hiyo nimhakikishie kwamba kazi ya ujenzi wa Majengo hayo itafanyika.

Mheshimiwa Spika, pili, ni kweli kwamba Halmashauri ya Meatu ni miongoni mwa Halmasahuri zenye upungufu wa watumishi. Hata hivyo Serikali kwenye mwaka wa fedha uliopita imeajiri jumla ya watumishi wa afya 10,462 na Halmashauri ya Meatu imepata jumla ya watumishi 104 wakiwemo wauguzi, lakini pia na madaktari na zoezi hili tutaendelea kulitekeleza kwa awamu, ahsante sana.