Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuwapatia Wananchi maeneo ya kulima kutoka kwenye mapori na Hifadhi ambazo hazina wanyama kwa sasa?

Supplementary Question 1

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Nina swali moja;

Kwa kuwa robo tatu ya Pori Tengefu la Lwafi la Wilayani Nkasi halina wanyama na wananchi wameshaingia wanafanya shughuli zao za kiuchumi; na mipaka hiyo tangu 1948 kipindi cha ukoloni iliwekwa, lakini baadaye ikaja ikabadilishwa ikasogezwa kwa wananchi.

Je, Mhesimiwa Waziri haoni kuwa ni kukwamisha juhudi za wananchi wa Wilaya ya Nkasi wanaojitafutia riziki zao?

Je, ni lini tutakuja kupitia upya ili mipaka irekebishwe, wananchi wameongezeka ili wapate maeneo ya kulima? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vicent Mbogo, Mbunge wa Nkasi, akiwakilishwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Aida Khenani, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nataka tu nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Wilaya ya Nkasi haina uhaba wa maeneo, isipokuwa kuna changamoto ya mtawanyiko. Wananchi wanaishi pale ambapo wanahitaji kukaa, kitu ambacho tunaipa mzigo Serikali kupeleka huduma kwa wananchi tukiendelea kuwaruhusu waendelee kutokomea kwenye maeneo ya hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoelekeza Serikali ni kwamba wananchi wapangwe kwa kuangalia matumizi bora ya ardhi ili kuwepo na miundombinu inayowezesha huduma bora za wananchi ziweze kuwafikia wananchi. Hili swali analolisema kwamba robo tatu ya Lwafi haina wanyama. Ili eneo lihifadhiwe vizuri na ili liwe na madhari nzuri ni pale tu ambapo litaachana na shughuli za kibinadamu. Ndiyo maana yale maeneo ambayo tunayatunza vizuri wanyama huwa wanarudi taratibu na uhifadhi unakuwa ni endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nataka niwaambie tu wananchi wa Nkasi kwamba maeneo ambayo tunayahifadhi mengine tunayachukua yakiwa hayastahili kuwa hifadhi; lakini yanapotunzwa kwa muda mrefu uoto wa asili unarudi, madhari inarudi na wananyama wanaanza kurudi. Kwa maana nyingine wanyama wanatoweka baada ya shughuli za kibinadamu kuingilia maeneo ya hifadhi. (Makofi)

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuwapatia Wananchi maeneo ya kulima kutoka kwenye mapori na Hifadhi ambazo hazina wanyama kwa sasa?

Supplementary Question 2

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa sababu kwa sasa kuna migogoro mingi inayoendelea nchini ambayo inapelekea mpaka mauaji kwenye maeneo ya hifadhi na wananchi;

Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kupitia upya sheria za uhifadhi ili ziweze kuendana na nyakati za sasa na kupunguza migongano kati ya wananchi na wahifadhi? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamoto hizi Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Pombe Magufuli aliunda Kamati ya Mawaziri nane ambao walipita nchi nzima. Na utekelezaji wake ni kama ambavyo umeona, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imetekeleza kwa kwenda kijiji kwa kijiji, kata kwa kata, wilaya kwa wilaya, kutoa ufafanuzi. Yale maeneo ambayo yameonekana wananchi wanaweza kuachiwa; tumeachia jumla ya vijiji 975 vimerudi kwa wananchi. Kuna yale maeneo ambayo ni ushoroba wa wanyama, ni mahitaji mahsusi kwa ajili ya uhifadhi endelevu yamerudishwa kwa Serikali; na ndiyo maana maeneo ambayo tumeyaachia wananchi walishangilia na tulivyokuwa tunapita wananchi wamefurahi kwamba Serikali imewasikiliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya machache ni kwa ajili ya uhifadhi mahsusi ili kutunza vyanzo vya maji lakini kuhifadhi mazingira pamoja na uhifadhi endelevu, ahsante.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuwapatia Wananchi maeneo ya kulima kutoka kwenye mapori na Hifadhi ambazo hazina wanyama kwa sasa?

Supplementary Question 3

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza ninaipongeza Wizara, walituma timu kwa ajili ya kutatua mgogoro kwenye Hifadhi ya Kitulo na Mpanga Kipengele. Swali langu; ni lini wananchi hawa wa maeneo ya Ipelele, Ikovo na Mfumbi ambao wanapakana na Hifadhi ya Kitulo pamoja na Pori la Mpanga Kipengele mtawapatia barua, kwa sababu mlionesha nia ya kuwaongeza maeneo, ili waanze kufanya shuguli zao za kichumi kwa kuwa muda mrefu sasa wameendelea kusubiri barua lakini hawajapata maamuzi ya Serikali? (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo hili kwamba, Serikali iliunda Kamati ambayo ilienda kufanya tathmini uwandani, na Kamati hii imeshapita maeneo takribani nchi nzima, ikiwemo eneo la Mheshimiwa Sanga. Kwa hiyo, sasa hivi kinachofanyika ni utekelezaji wa uchambuzi uliofanyika uwandani. Wakati wowote naomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge na wananchi wanaozunguka Hifadhi ya Kitulo kwamba kuanzia sasa utekelezaji wake utafanyika na tutawajulisha wananchi maeneo husika, kwamba sasa tathmini imeenda hivi. Tutapita pia kijiji kwa kijiji, hifadhi kwa hifadhi, tunashirikiana kuweka vigingi ili kuondoa hii taharuki ya wananchi kutofahamu mipaka halisi. (Makofi)

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuwapatia Wananchi maeneo ya kulima kutoka kwenye mapori na Hifadhi ambazo hazina wanyama kwa sasa?

Supplementary Question 4

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa Hifadhi ya Serengeti na Kata za Nyanungu, Goroma na Kuhihancha, ni mgogoro wa muda mrefu na mipaka iliwekwa mwaka 68 bila kushirikisha wananchi. Naomba nijue Wizara ya Maliasili; ni lini sasa itaenda katika kata hizo ikae na wananchi pamoja bila kutumia mzinga na bunduki wasikilize wajadiliane kumaliza mgogoro katika eneo hilo. (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Waitara, Mbunge wa Tarime, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna changamoto kubwa katika Jimbo la Mheshimiwa Waitara; na hivi karibuni tu askari wetu ameuwawa kwa kupigwa mshale. Hili kwa kweli sisi kama Serikali tunasikitika sana wananchi wanapojichukulia mamlaka ya kudhuru wahifadhi ambao wanalinda rasilimali zetu sisi kwa faida yao wenyewe. Hili naomba niliseme hadharani kwamba wale askari wako kwa ajili ya kulinda rasilimali za Taifa na si vinginevyo. Kwa hiyo tunaomba tuheshimu mipaka, tuheshimu hifadhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapomuua askari hauwezi kuibadilisha ile ramani. Askari atakufa lakini ramani itaendelea kuwepo; ni mpaka pale Serikali itakaporudi kuutatua huu mgogoro. Kwa hiyo tunaomba wananchi wasijichukulie sheria mkononi, hilo ni la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala la pili, nataka nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaenda wenyewe kwenda kutatua ana kwa ana na wananchi na kuwatahadharisha kwamba kuendelea kuua askari wataishia jela, kwa sababu lazima sheria ichukue mkondo wake. (Makofi)

Name

Joseph Kasheku Musukuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuwapatia Wananchi maeneo ya kulima kutoka kwenye mapori na Hifadhi ambazo hazina wanyama kwa sasa?

Supplementary Question 5

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Ningependa kumuuliza swali la nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri. Naipongeza Serikali kwa kumaliza Mgogoro wa Ngorongoro vizuri kabisa kwa kuwahamisha wale wananchi waliokuwa Kata ya Ngorongoro kwenda Kilindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Nyatwali iliyopo Bunda ni sawa sawa na kata iliyoko Ngorongoro. Ile kata ina hamishwa yote ikiwa na miundombinu ya shule, hospitali na vitu vyote, na ni kata ya enzi na enzi. Hata hivyo, kuna double standard ya Serikali. Inaonekana kule watalipwa milioni mbili ilhali kule watu walihamishwa kistaarabu mpaka na ng’ombe wakabebwa kwenye gari.

Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza Mgogoro wa Nyatwali?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Musukuma, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Nyatwali na vijiji jirani vinavyozunguka kata hiyo, Serikali ilitoa mapendekezo ya kulichukua eneo hilo kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza katika eneo hilo. Wananchi hawa wako kihalali na hii sentensi Serikali kila siku tumekua tukiiongelea; wako kihalali sio wavamizi na vijiji vilivyoko pale vimesajiliwa kihalali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu uliopo, Serikali inapoona kuna umuhimu wa eneo lile kulichukua kwa maslahi ya Taifa, hapa nikisema maslahi ya Taifa, tuna resources nyingi ambazo tunazitumia kwa maslahi ya Taifa. Kwa hiyo, hata hili eneo tunaliangalia kwa upana zaidi na si kwa wananchi wachache.
Kwa hiyo, tunachofanya, tumefanya uthamini na wananchi waliomba mapendekezo kwamba badala ya heka kulipwa milioni mbili basi wanaomba milioni tatu. Ahadi tuliyoitoa ni kwamba tathmini ifanyike watathmini waingie uwandani waone halafu Serikali itaona nini kifanyike na tutarejesha kwa wananchi mrejesho ambao utakuwa ni muafaka kati ya wananchi na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa tahadhari tu, hawa wanaohamishwa ni kwa mujibu wa sheria za nchi. Ngorongoro imekuwa treated tofauti na maeneo mengine. Mara nyingi Waheshimiwa Wabunge wanadai pale ambapo wananchi wanahamishwa wanataka walinganishe na Ngorongoro. Suala la Ngorongoro lipo tofauti kabisa na maeneo mengine, ahsante.