Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Shabani Hamisi Taletale

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini Mashariki

Primary Question

MHE. HAMISI S. TALETALE aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kukuza kilimo cha mazao ya viungo katika Wilaya ya Morogoro Vijijini?

Supplementary Question 1

MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Moja ya changamoto kubwa ya wananchi wa Morogoro Kusini Mashariki na Morogoro Vijijini kwa ujumla ni ukosefu wa mitaji. Je, Serikali ina uratatibu gani wa kutuletea mitaji wana Morogoro Vijijini?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Hamisi Shabani Taletale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mitaji kwa wakulima ni suala ambalo tunalipa kipaumbele Serikali, tupo tayari kukaa na Mheshimiwa Mbunge pamoja na ushirika wa wakulima hawa ili tuangalie fursa ambayo wanaweza kuipata kuimarisha mitaji yao.