Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Khadija Shaaban Taya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kuinua ushiriki wa Watu wenye Ulemavu katika michezo ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa wavu na pete?

Supplementary Question 1

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jibu zuri: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza; kwa kuwa, Serikali inafahamu fika michezo sanaa na tamaduni ni moja ya suluhu ya kuongeza ajira katika nchi yetu. Sasa Serikali haioni sababu ya kuipa kipaumbele michezo, sanaa, ili waweze kutatua tatizo la ajira kwa watu wenye ulemavu?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khadija, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa naibu Spika, ahsante. Swali lake la kwanza alipenda kufahamu ni kwa kiasi gani Wizara tunahakikisha kwamba, tunaendelea ku- promote michezo hii ya wtu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yetu inahakikisha na tunashirikiana na vyama mbalimbali, katika miundombinu tunahakikisha watu wenye ulemavu wanapewa kipaumbele, hata katika ujenzi wetu wa shule 56, miongoni mwa shule ambazo tumezitenga zipo za watu wenye ulemavu. Kwa hiyo, tunaendelea kuwashirikisha na kuwajengea miundombinu.