Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje katika kupambana na changamoto ya upungufu wa Wataalam wa Mazoezi Tiba na huduma ya Utengamao nchini?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kupata nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa vile bado tuna upungufu mkubwa wa wataalam wa mazoezitiba na utengamao: -

Je, hawaoni sababu ya kuanzisha course hii kwenye vyuo kama UDOM ambapo inachukua watu wengi ili angalau tupate wahitimu wa taaluma hiyo kwa wingi? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Mbunge, Dkt. Kaijage kwa namna anavyoshirikiana na Wizara ya Afya kwa karibu hasa kwenye kushughulikia huduma ya mama na mtoto kwenye Mkoa wa Pwani. Vilevile nimwambie tu kwamba, siyo tu Chuo Kikuu cha UDOM, kuna mkakati wa vyuo zaidi ya vitano sasa tunaongeanao na kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kuanzisha kada hizi ili kusaidia kupunguza upungufu wa wataalam kwenye soko la ajira. Ahsante sana.