Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: - Je, ni lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Simiyu utaanza baada ya kukamilika zoezi la uthamini wa eneo la Uwanja utakapojengwa?

Supplementary Question 1

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa majibu yanaendelea kutolewa haya haya kila tukiuliza swali; je, nini kauli ya Serikali kuhusu lini uwanja huu utaanza kujengwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Esther Lukago Midimu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge atakubaliana nami kwamba Serikali imeshakwenda hatua kubwa mbele, tayari tumeshathamini na tayari maandalizi ya malipo ya watakaopisha mradi huu yako yanafanyiwa kazi na tumeahidi kama Serikali kwamba baada ya kukamilisha suala hilo, ujenzi wa Uwanja wa Simiyu utaanza. Ahsante.