Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE K.n.y. MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuiwezesha TASAC iweze kuhudumia meli nyingi?

Supplementary Question 1

MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Usalama wa vyombo vya majini ni lazima kwa maisha ya watu na mali zao. Je, Serikali inafanyaje kila baada ya muda kuvifanyia ukarabati kisheria?

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba usalama ni jambo la msingi na ni lazima lifanyike. Kwa sheria yetu tunafanya ukaguzi kila mwaka kwa vyombo vyote vya majini na kwenye maziwa makuu, na huwa tunatoa cheti kinachoitwa seaworthiness certificate. Hata hivyo, hatulazimiki tu kwa mwaka, tunaweza tukafanya pia kwa wakati wowote inapobidi shirika lijiridhishe na vyombo hivyo. Ahsante.