Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kurekebisha miundombinu ya Skimu ya maji katika Kijiji cha Mbuganyekundu?

Supplementary Question 1

MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Mto wa Ngainanyuki katika Wilaya ya Longido ni muhimu sana kwa kusaidia kilimo cha umwagiliaji: Je, Serikali ina mkakati gani wa kusanifu miundombinu ya mto huu ili kuwasaidia wananchi wa Longido? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika moja ya mikakati ambayo Wizara tunayo ni kuhakikisha ya kwamba tunatumia ipasavyo vyanzo vya maji katika maeneo yote ya mabonde ili tuweze kufanya kilimo cha umwagiliaji. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa hili ambalo limewasilishwa litakuwa ni sehemu ya mipango yetu na tunaielekeza Tume ya Umwagiliaji kuweza kufika na kuliangalia eneo hilo mara moja kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine.