Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 66 2022-09-16

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kurekebisha miundombinu ya Skimu ya maji katika Kijiji cha Mbuganyekundu?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai, Mbunge wa Karatu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kujenga miundombinu ya umwagiliaji ya skimu zilizopo katika bonde la Eyasi zenye jumla ya hekta 5,000 ikiwemo skimu ya Mbuganyekundu. Taratibu za kuwapata wakandarasi wa ujenzi wa skimu hizo unaendelea ambapo zabuni zimeshatangazwa.